Malawi pia wanayo Ilala kwa taarifa yako,Inabidi urudi darasani ukajifunze historia ya lugha ya kiswahili na lugha ya kibantu kwani nina uhakika hujasoma hayo mambo ukisoma nahisi utachanganyikiwa sana.Nilikuwa nchi flani ya kusini mwa Afrika,Nilikuwa nime-chill somewhere na wadada flani wa nchi hiyo katika mazungumzo yao yaliyotawaliwa na lugha ya asili ya kabila lao (Ovambo) nikasikia wakitamka neno m-a-s-a-b-u-r-i nikashtuka sana,nikajikuta nacheka na kuyaingilia mazungumzo yao,nikawauliza tena.."come again,did you say m.a.s.a.b.u.r.i?" wakasema ndiyo kwa kujiamini wakidhani sikuelewa maana ya lile neno.Nikawaambia hilo neno kwa maana ya kiingereza wakashangaa sana then nikaja kuelewa kuwa kumbe maneno ya kibantu yapo mengi sana na yanatumika katika mawasiliano yetu ya kila siku sehemu mbalimbali za Afrika.Wazambia na Wamalawi wanaoongea lugha ya kilozi unaweza ukawaelewa vizuri kutokana na maneno yaliyomo kwenye lugha hiyo pia kutumika kwenye ya kiswahili.Soma sana historia mbalimbali ili upanue ufahamu wako mzee.