Waraka wangu kwa viongozi wa CHADEMA

Waraka wangu kwa viongozi wa CHADEMA

............Na Mataifa makubwa yote tokea Roman Empire hadi utawala wa Marekani leo wameanguka ama kupata mtihani mkubwa pale wanapojaribu kuwatenga watu kwa kutumia dini, kabila au tamaduni zao hivyo ni muhimu sana kwa chama hiki kuzingatia pamoja na kwamba serikali haina dini lazima tukumbuke wananchi wetu wana dini zao na makabila yao, wana maumbile yao hivo ni lazima vienziwe na sio kupigwa vita. Tunapiga vita wale wanaojaribu kukwaza wengine, wale wanaojaribu kuleta Ukabila na Udini (kudharau wengine) lakini sio wale wanaoitaka haki ya kuabudu kama alivyosema Ibambasi kwa utetezi wa waumini wa jadi..

Waheshimiwa, Inabidi nikomee hapa ktk waraka huu ambao unasisitiza zaidi kujitazama upya. Kutazama makundi ya jamii zetu kama sehemu ya Utaifa wetu badala ya kujaribu kuwabadilisha ama kuwakwaza. Chadema ktk hali hii inahitaji sana nguvu ya Watanzania wapiga kura ambao kwa nafasi zao hawawezi kushawishika na Utaifa ulojaa KUJUANA na sii rahisi wanaongoa watu wasikuwa na Imani.

Hivyo, Tuache UNAFIKI, tuache kujidanganya kwa unafiki wa wapambe wa vyama wanaotumia siasa kaa uwanja wa kujuana. Sisi sote ktk nafasi tulizopo na kutambua kwamba Utanzania wetu unajumuisha tofauti zetu za maumbile, makabila na imani za dini na yeyote atakaye jaribu kumdharau hata mmoja wetu ni kielelezo cha Ubaguzi ambao hautakiwi kupewa nafasi bali kuupiga vita. Hizi ndio ngao zetu, ndizo zinazo tu identify kama jamii ya Kitanzania na lazima tuzilinde dhidi ya siasa za chuki na uutengano. Bila utayari wa kuwajumuisha watu wote kwa tofauti zao kama sehemu ya Utanzania wetu itakuwa vigumu sana kupata ushindi mwaka 2015 maana CCM wanaifanya kazi yao ipaswavyo – Kushambulia nasi ktk kujilinda lazima tuwe na kinga zetu kwa kufanya vitu sawa – Doing things right !

Nawakilisha..

mmmmhh........Mkuu this is very sophisticated issue/matter.....Chama chochote inabidi kuwa waangalifu sana na huu ushauri wako......kwa sababu wakibugi stepu tu......"kwishnei"!!.......both CUF and Chadema wanaonekana kunaswa kwenye mtego....na ndio maana CCM wanatupiga bao......kwa sababu wananchi wanaona bora/afadhali Magamba tunawafahamu na angalau haki zetu za "utofauti" zinaangaliwa.........

Tuna safari ndefu sana kwa kweli......bado sijawa na imani na level ya Education kwa wananchi wetu.......education imekuwa taken hostage na ushabiki..........na Magamba wame-capitalise kwenye hilo..........vyama vya siasa hata viwe na SERA nzuri kiasi gani....bila ya wananchi kuwa na elimu ya kutambua/kung'amua....tutakuwa tunapiga ngumi hewani........

......kuna sehemu nimesoma......eti wananchi wametoa maoni ya katiba.......iwekwe limit ya umri wa kupiga kura iwe miaka 60......duuuhhh!

Naona sasa tuna "M4C" na "Mchakamchaka".......duuhh.......vyote hivyo vimenasa kwenye mtego uliouweka kwenye post yako.......
 
Kwa sehemu ndogo niliyokupata umemaanisha watu wanaojipambanua kwa dini zao wapewe nafasi ya kubembelezwa!!!!

Mimi nawaambia viongozi wangu wa chadema; ni heri kutokuingia ikulu kuliko kuingia kwa upendeleo wa wanaojitambua kwa imani zao.

Waelimisheni wajitambue kwa utanzania wao ndipo wawape ridhaa ya kuwaongoza.
Haihitajiki mistari miiiiiiiiiingi unazunguka zunguka kisa unataka waislamu wapewe aproach ya kiislamu.

kwenye ukombozi huu wanatakiwa watanzania-waislamu pamoja watanzania wa imani zingine na wala si waislamu-watanzania . . . .
Mkuu inawezekana jana wakati unaisoma hii ulikuwa na usingizi. Jaribu kutulia kisha soma tena huo waraka pengine leo utauelewa.
 
teh teh..mbona hiyo paragra[h ina pasonality mbili?..kuna tu-kama sisi, ki-kama chama.

Kweli CDM kama honeybadger, wanaweza indure maultiple attacks...JF nayo ni kiboko kwa kunusa traces za vitu haramu.
Mkuu Nicholas, hizo nukuu za red ni summary ya bandiko la Mkandara na sio maneno yangu.

Ila sio siri, kwanza naomba nikupongeze, unazama deep, ila pia unakuwepogo wapi?, leo ndio nimekuona na niliposoma status yako, nikakuta ni ya 2006!, unajichimbiaga wapi?.

Namshukuru Mkandara kukuibua,

Kikweli mimi sio mfuasi wa chama chochote ila nakiri kuwa ni mmoja wa wakosoaji wakuu wa Chadema humu jamvini mpaka watu kunidhania ni gamba!. Kinachomkumba Mkandara ndicho nilichokitegemea maana naelewa matokeo ya ukosoaji wowote wa Chadema humu jukwaani!.

Ukija kupata muda, nitakuomba mchango wako kwenye hizi baadhi ya hoja zangu, japo nyingine zimepitwa na wakati, lakini nyingine ziko still valid!.

  1. CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!
  2. Yametimia!, CCM Imechokwa!, Chadema Njia Nyeupe 2015!-Jipangeni ...
  3. Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
  4. Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM!.
  5. Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward ... - JamiiForums
Nimependa hoja zako jinsi unavyobanana na Mkandara, nilichopenda zaidi ni jinsi unavyojiaminisha kuwa Chadema imesimama na 2015 ushindi ni wazi, Mkandara katoa angalizo kuwa japo sasa Chadema imesimama, kusimama huku ni kwa muda tuu, CCM ikimsimamisha mtu makini, Chadema haitafua dafu kutokana ma mapungufu aliyoyaorodhesha.

Mimi naungana na Mkandara kwa hoja kuwa "Anayejidhania Amesimama, na Aangalie Asianguke", nachelea kusema kuwa watu wamehamanika na too great expectations kuwa 2015 ni Chadema!, ikitokea vinginevyo, just try to imagine, mtaliaje?!. Sasa mnaambiwa, ndio kwanza mnabisha!, jee tusubirie mpaka hiyo 2015 mkishalizwa ndipo muambiwe mapungufu yenu, au bora muambiwe sasa ili likitokea la kutokea, kulia mtalia, lakini angalau "mliambiwa"!.

Pasco.
 
Hongera sana Mkandara (Lufufu) kwa mada nzuri, iliyochambuliwa kwa kina na kitafiti.

Mie ushauri wangu wa siku zote, ni kuwaomba wanachama wa CHADEMA waache fikra za "bila fulani chama kitakufa". Naomba wanaCHADEMA wote wajione wana wajibu sawa na haki sawa. Viongozi waliopo madarakani sasa, nao wasijione kuwa ndio kila kitu na kufikiri bila wao chama kitakufa. Amini nawaambia, kuna Watanzania, mamia kwa maelfu, ndani na nje ya nchi, mijini na vijijini, wenye uwezo mkubwa wa kukiongoza chama.

Muhimu zaidi ni kushikamana na kukwepa mtego wa makundi, ambao CCM imeuasisi na kuufadhili. Sifurahishwi, kwa mfano, na polls za "nani zaidi kati ya Zitto na Slaa, nani zaidi kati ya Mbowe na Slaa, n.k. Spendi kusikia kauli za "fulani ni Rais tu 2015, fulani hana mpinzani 2015, n.k. Hizi zote ni mbinu za kukidhoofisha chama kwa kuyajenga makundi na kuwafanya viongozi wetu washindwe kuaminiana na kuifanya kazi kubwa iliyo mbele yao. Tusiwe na haraka, na kwa kuwa CHADEMA ni chama kilichojengwa katika misingi imara ya demokrasia, muda ukifika aliye zaidi atachaguliwa kwa njia halali zinazotambuliwa na chama.

Wanachama ndio chama; pamoja tutashinda.
 
Mkuu wangu labda nikwambie tu ya kwamba watu wengi wamechoka na utawala wa Kikwete na sio CCM. watu wengi bado wana imani na chama hiki kama akipatikana kiongozi wamtakaye. Subiri kama watamsimamisha Mwandosya au Rose Migiro utaona jinsi upepo utakavyo badilika. Hii ni tahadhari tu mkuu wangu tusijikite ktk kushambulia watu badala ya sera za CCM. Pili, tujihadhari na propaganda za CCM na CUF tayari zimeisha ingia watu vichwani iwe wakristu au waislaam halafu what about those who are not Christians or Muslims wao wamesimama wapi? nini nafasi yao - hakuna mshindi hapa.. Chuki tayari imeshajenga na huwezi kuiondoa majukwaani..
Mkuu Mkandara, nakushukuru wewe umeliona hili, kama CCM itamsimamisha mtu safi asiye na mawaa ni kweli Chadema itakuwa na kazi kubwa 2015. Prof. Mark Mwandosya they've already done him!, Asha Rose ni msafi na hana mawaa yoyote ila binafsi yangu, sipendi asimamishwe yeye kwa sababu zile zile ambnazo sipendi simamishwe Dr. Shein. Japo mgombea wangu kwa CCM, 2015 ni EL, inside trends zinaelekezwa kwa Benard Membe!.

Nimewashauri Chadema waachane na politics of confrotations, wapunguze mashambulizi kwa CCM as an entity, waconcentrate na watu ambao ndio wapiga kura!. Nikasema determinant ya ushindi wa Chadema 2015, lies with who will stand on CCM ticket, with M4C, there is hope but msipokuwa makini, 2015 Ikulu mtaishia kuisikia tuu kwenye bomba!.

Pasco.
 
Nashauri JF tuanzishe utaratibu wa kuwa na abstracts. Kuna posts ndefu mno kiasi cha kuweza kumfanya mtu afukuzwe kazi (kumbuka kuna mambers wengi wanaaccess JF wakiwa kazini).

Ukiandika post ndefu itengenezee abstract ya maneno kama 150 iweke pale juu, ili wadaua wa fasterfaster wapate picha nini kinazungumziwa...

Mimi nikiona nipo fasta siwezi kuusoma na kuudigest haraka huwa naucopy then nikitulia naufuatilia hata nikiwa offline. Jaribu hii Mkuu.
Ni utafiti mzuri nimeupenda.
 
Tuombe Mungu 2015 CHADEMA iibuke mshindi kwani isiposhinda sina uhakika kama itasimama imara kama ilivyosimama baada ya uchaguzi wa 2010.
Mkuu Ndiba, 2015 ni do or die!, ushindi hauji kwa kuomba Mungu, ushindi unapangwa kwa the right plans, using the right strategies and the right time!. Mada ya Mkandara inaleta angalizo jingine muhimu sana la "doing the right thing" and "doing things right", ambapo what Chadema is doing now with M4C, its the right thing, na ameanisha madhaifu fulani kuwa Chadema is yet to do "the things right"!
 
Mkuu Mkandara, nakushukuru wewe umeliona hili, kama CCM itamsimamisha mtu safi asiye na mawaa ni kweli Chadema itakuwa na kazi kubwa 2015. Prof. Mark Mwandosya they've already done him!, Asha Rose ni msafi na hana mawaa yoyote ila binafsi yangu, sipendi asimamishwe yeye kwa sababu zile zile ambnazo sipendi simamishwe Dr. Shein. Japo mgombea wangu kwa CCM, 2015 ni EL, inside trends zinaelekezwa kwa Benard Membe!.

Nimewashauri Chadema waachane na politics of confrotations, wapunguze mashambulizi kwa CCM as an entity, waconcentrate na watu ambao ndio wapiga kura!. Nikasema determinant ya ushindi wa Chadema 2015, lies with who will stand on CCM ticket, with M4C, there is hope but msipokuwa makini, 2015 Ikulu mtaishia kuisikia tuu kwenye bomba!.

Pasco.

Hapo kwenye red, inaonekana wapo wengi, kuna gari (bus) la Dar -Mtwara limendikwa 'My president EL', mi simo naenda kazin bana
 
Mkuu Nicholas, hizo nukuu za red ni summary ya bandiko la Mkandara na sio maneno yangu.

Ila sio siri, kwanza naomba nikupongeze, unazama deep, ila pia unakuwepogo wapi?, leo ndio nimekuona na niliposoma status yako, nikakuta ni ya 2006!, unajichimbiaga wapi?.

Namshukuru Mkandara kukuibua,

Kikweli mimi sio mfuasi wa chama chochote ila nakiri kuwa ni mmoja wa wakosoaji wakuu wa Chadema humu jamvini mpaka watu kunidhania ni gamba!. Kinachomkumba Mkandara ndicho nilichokitegemea maana naelewa matokeo ya ukosoaji wowote wa Chadema humu jukwaani!.

Ukija kupata muda, nitakuomba mchango wako kwenye hizi baadhi ya hoja zangu, japo nyingine zimepitwa na wakati, lakini nyingine ziko still valid!.

  1. CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!
  2. Yametimia!, CCM Imechokwa!, Chadema Njia Nyeupe 2015!-Jipangeni ...
  3. Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
  4. Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM!.
  5. Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward ... - JamiiForums
Nimependa hoja zako jinsi unavyobanana na Mkandara, nilichopenda zaidi ni jinsi unavyojiaminisha kuwa Chadema imesimama na 2015 ushindi ni wazi, Mkandara katoa angalizo kuwa japo sasa Chadema imesimama, kusimama huku ni kwa muda tuu, CCM ikimsimamisha mtu makini, Chadema haitafua dafu kutokana ma mapungufu aliyoyaorodhesha.

Mimi naungana na Mkandara kwa hoja kuwa "Anayejidhania Amesimama, na Aangalie Asianguke", nachelea kusema kuwa watu wamehamanika na too great expectations kuwa 2015 ni Chadema!, ikitokea vinginevyo, just try to imagine, mtaliaje?!. Sasa mnaambiwa, ndio kwanza mnabisha!, jee tusubirie mpaka hiyo 2015 mkishalizwa ndipo muambiwe mapungufu yenu, au bora muambiwe sasa ili likitokea la kutokea, kulia mtalia, lakini angalau "mliambiwa"!.

Pasco.

teh teh....sounds kama wale wanaodai hawana dini halafu soon wanandika dini zao...kwanini unadhani nimeibuka?Na kwanini mkandala aniibue?Very strange.

Well,tembelea profile yangu halafu uangalie thread zangu majibu yote hayo yapo.mengine directly mengine indirectly.By the way kwanin mnahofia sana CDM wakati CCM inaweza isifike 2015 bila kuvunjika yenyewe.Hilo rundo la wazee ambao wanagombania "the only golden chance" hujaona kuwa ni tishio la kutosha bomoa CCM?hujasikia bastola wanazoshikiana?hujaona mpaka leo hawajaweza vunja makundi?Hujasikia balaa la UVCCM?Hujasikia ya 6?Nani wa kumhofia mwenzake.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...hine-za-catapiller-kwa-mlima.html#post4590161
 
Umesoma lakini hujanielewa na ndilo tatizo la Watanzania hamtaki kusoma isipokuwa amnajua sana kuuchonga ktk ujinga..Sijazungumzia vyeo wapewe kina nani isipokuwa kutokuwepo mfumo huo utumike maana unatumika. Swala ni kutambua uhuru, haki na usawa wa jamii zetu. Huwezi kuleta usawa mahala popote kwa kuzuia (kukwaza) isipokuwa kwa kuwawezesha. Hata katika uzalishaji hatuwezi watu wote kuwa Wakulima wa kilimo, isipokuwa wapo wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na Wafanyakazi , wawekezaji na kadhalika. Hawa wote wanataka kuwezeshwa na sio kukwazwa ktk nafasi zao za Uzalishaji kwa sababu kiongozi fulani anapendelea zaidi Ukulima.

Labda nikuulize wewe UTANZANIA ndio nini? nini mila na desturi zao, wanafananaje? wana mahusiano gani tofauti na watu wengine au unataa kunambia ukisha zaliwa Tanzania basi unalazimika kuwa kinyambiro kisichokuwa na identity. hata Mweneyezi Mungu katuumba tofauti kwa maumbile, makabila na kadhalika leo wewe nani wa kusema hakuna tofauti hizi.

BOLDED...mindset------
Unaamini kuwa Vyeo hupewa watu kutokana na dini zao. If you believe that then we have a problem.
Unaamini kuwa kuna watu wanakwaza. Lakini ungetaja kabisa nani wanakwazwa. Tuwe open kote, kama wewe hauwi muwazi nani anakwazwa itakuwa ni hisia kuwa unaogopa kusema ukweli.

Tufike mahali tukubali kuwa Serikali iwe haina dini wala ukabila, watu waende kanisani au msikitini na mambo yao yaishie huko huko na nyumbani kwao.

Ni kweli kabisa Chadema ni Chama Mbadala kwa Nchi hii lakini vile vile kuna matatizo; the main problems yapo kwenye public relation communication (including media relationship), intergration, intelligence etc.
 
Waache basi kutangaza wanatupeleka "nchi ya ahadi" waache kutwambia wanaanza na "Mungu wanamaliza na Mungu" kwanini siku zote Mungu tu? lini wataanza na Allah au Buddha au Rama au Krishna au Mzimu wa Pande? si wote wanaoamini Mungu wa chadema wala "nchi ya ahadi".
 
Zombie you need to grow up!
 
Waache basi kutangaza wanatupeleka "nchi ya ahadi" waache kutwambia wanaanza na "Mungu wanamaliza na Mungu" kwanini siku zote Mungu tu? lini wataanza na Allah au Buddha au Rama au Krishna au Mzimu wa Pande? si wote wanaoamini Mungu wa chadema wala "nchi ya ahadi".
Allah/Krishna anaitwaje Kiswahili?
 
Nimekukubali mkuu, kukaa kimya kunahalalisha misconceptions ambazo zinaendelea kuwaweka magamba madarakani.
Inabidi zijibiwe promptly and aggressively.

Kuwatuhumu Chadema kwamba wameshambuliwa wamekaa kimya si sahihi hata kidogo Kurugenzi ya Habari chini ya Mnyika, Makene na wakati mwingine hata Slaa na Mbowe wamejitokeza kujibu tuhuma mbalimbali juu yao. Suala ukanda limefeli kwani kila mtu anajua leo who Tundu Lissu, mch. Peter Msigwa, Kabwe Zitto na wengineo.
 
Kwa sehemu ndogo niliyokupata umemaanisha watu wanaojipambanua kwa dini zao wapewe nafasi ya kubembelezwa!!!!

Mimi nawaambia viongozi wangu wa chadema; ni heri kutokuingia ikulu kuliko kuingia kwa upendeleo wa wanaojitambua kwa imani zao.

Waelimisheni wajitambue kwa utanzania wao ndipo wawape ridhaa ya kuwaongoza.
Haihitajiki mistari miiiiiiiiiingi unazunguka zunguka kisa unataka waislamu wapewe aproach ya kiislamu.

kwenye ukombozi huu wanatakiwa watanzania-waislamu pamoja watanzania wa imani zingine na wala si waislamu-watanzania . . . .

Mkuu siyo lazma ukopi uzi wote, wengine tunatumia vimeo vya mobile mnatuchosha bana
 
Waache basi kutangaza wanatupeleka "nchi ya ahadi" waache kutwambia wanaanza na "Mungu wanamaliza na Mungu" kwanini siku zote Mungu tu? lini wataanza na Allah au Buddha au Rama au Krishna au Mzimu wa Pande? si wote wanaoamini Mungu wa chadema wala "nchi ya ahadi".

Nakushangaa sana, issue ya 'nchi ya ahadi' ni popular humu JF, huku nje watu hawana neno kama hilo wao wanachojua wanataka nchi free from economic bandits na yenye utawala bora. Kuhusu kuanza na Mungu dini zote zinatambua neno hilo ni sahihi unaweza refer hata tu kamusi ya kiswahili. Kung'ang'ania Allah kuwa kiswahili sahihi ni kutulazimisha wote tuwe watumwa wa kiarabu kama wewe.
 
Nimeshasikia viongozi wa chadema kwenye mikutano wakitangaza hilo na nimeshamsikia Halima Mdee bungeni akitangaza hilo. Funguka. Si wote tunaoamini mafundisho hayo, bila wana siasa wenu kubadilika, nchi mtaisikia tu hii. Na kwa "kupigana" ndio kabisa maana ikiwa kwa maneno hayo kwa kura za wengi hamuwezi.
 
Kuwatuhumu Chadema kwamba wameshambuliwa wamekaa kimya si sahihi hata kidogo Kurugenzi ya Habari chini ya Mnyika, Makene na wakati mwingine hata Slaa na Mbowe wamejitokeza kujibu tuhuma mbalimbali juu yao. Suala ukanda limefeli kwani kila mtu anajua leo who Tundu Lissu, mch. Peter Msigwa, Kabwe Zitto na wengineo.

Unaweza kutupa asilimia ngapi? kutoka kanda tofauti kwenye uongozi na ubunge wa chadema.
 
Mhe.Mkandara;
Nimesoma andiko lako lote kwa utulivu mkubwa,Nimefuatilia michango yote ya wadau wengine na majibu yako kwao. Naomba kuikubali kwa namna ya kipekee michango ya Mr.Nicholas. Naelewa na kukubali kuwa umetumia muda mrefu sana kuandika uliyoandika. Kama kawaida ni lazima kuna kilichokusukuma hadi kuandika 'Waraka' huu. Nilichogundua ni kwamba ungependa ushauri wako uchukuliwe wote bila kuhojiwa au kuonyeshwa kuwa pengine ulichoandika kilishatekelezwa na chama kipo Imara kuelekea kuchukua dola 2015. Ukiwa na mawazo ya aina hiyo ni dhahiri kuwa unaweza ukakwazika kuishauri CHADEMA kama 'Alivyokwazika' Mr.Pasco. Chama chochote cha Siasa kina mikakati mipya kila siku. CHADEMA imekuwa na mikakati ya kila siku yenye mafanikio makubwa. Ukitaka kwenda kukabiliana na adui yako unapaswa kubeba silaha zako na si kusubiri yeye arushe mshale uudake na kuutumia kama silaha yako. Kauli za udini na ukabila kwangu mimi ni nyimbo za zamani zisizosikilizika tena! Ni nyimbo za Nape ambazo aliziimba zikakosa nafasi kwenye masikio ya wananchi. CHADEMA kama chama kukubali kuzibeba kauli hizo na kuhangaika kuzijibu ni kupoteza muda badala ya kuendelea na harakati za kujikita kujenga imani kwa wananchi waishio vijijini. Nitakuwa na hamu ya kuona majibu official kutoka kwa uliowalenga kwenye waraka huu (Kama wataona inafaa kujibu).
 
Back
Top Bottom