mokala1989
JF-Expert Member
- May 4, 2013
- 2,236
- 728
inategemea unatetea nini!
ni ngumu sana kuweka asili yako hadharani hasa kama unatetea mauaji, ubakaji na wizi wa mali asili za watu wengine.
inategemea unatetea nini!
Wanalazimisha kuwa wabongo...Kuna wanyarwanda na Pro Kagame lukuki humu JF ,Subiri utawaona miongoni mwao ni
@R.B
@Adolay
@Koba
@Mukamasimba
Manyerere,
Hivi kweli Rwanda hana maslahi Congo? Mnyonge mnyongeni haki yake mpe. Mwaka 1994 kulitokea genocide. We unawaonea huruma waliokufa kwenye ndege ya rais, na sio wanawake, watoto, nk. walliouwawa kikatili sana na wahutu wenye msimamo mkali, ambao baadae walienda Congo, ambako wapo hadi leo. Na viongozi wao ni walewale waliopanga na kufanya genocide.
FDLR kazi yao ni moja, kuja kumaliza kazi. Hivi pale Congo kungekuwa na kikundi chenye msimamo wa kuiangamiza Tanzania tungekaa na kusubiri tu? Nadhani Rwanda kuwa na mkono wake Congo kuna self-defence justification.
Kuhusu wizi wa madini, ndio, lakini uje kuwa haya madini yanaenda ngambo, yanachimbwa na watu wenye mtaji na teknologia, sio wana-mgambo wa M23 wenye afya mbaya.
Kuhusu EAC, some Treaty inasemaje, kasha uishauri Tanzania cha kufanya, usi-argue kama watoa maoni wa JF. Kuhusu bandari, hili sio suala la uzalendo, ni suala la biashara, watanzania wengi hupitisha magari yao Mombasa, then Horiri.
Kuhusu Watutsi, sioni kama ni jukumu lako kama mwandishi kushambulia kabila Zima, kama Kagame ana siasa ambazo hazikupendezi, basi shughulika nae.
Sidhani kama ni sahihi kuwashambulia Wakwere kwa makosa ya JK, hiyo ndo inachochea genocide. Ndege ya rais ilivyotunguliwa, wahutu walisema imetnguliwa na Watutsi, wakaua hadi motto mchanga, wakati maskini labda alikuwa ni Kagame na jeshi lake.
So, ninaposema ume-nidsappoint, ni kwamba mwandishi mwenye hadhi yako, hapaswi kuandika akiwa na hasira, anaandika kwa hoja kuisaidia jamii kufanya maamuzi sahihi. Au la, usiitumikie jamii kama mwandishi, nenda omba kazi jeshini, fanya mambo ya kizalendo zaidi, au hata mgambo.
Lakini kumbuka kalamu yako inaweza kuanzisha vita saa yoyote, ndoo maana waandishi wa Rwanda wamehukumia ICTR, yule Joshua Arap Sang wa Kenya yupo the Hague, etc. Leo hii humu ndani kuna uchochezi, mgao wa umeme Kagera wanasema ni Kagame, Bandari watu walitunga uongo, vichwa vya habari eti ni kagame., etc. hata kama hatumpendi waandishi wa habari lazima wawe weledi sio wachochezi
Usitake kuleta itikadi kiraia kwenye Jeshi,unafikiri ni hizo kazini za kiraia,hujui wanakula kiapo gani?,usituletee jeshi la mbu hapa,ndio mnapelekwa mafunzo muondolewe uraia..nenda nawewe ukaichukue hiyo thawabu kubwa! mkuu hebu acha kejeli kwa wafiwa hujui wategemezi wao wanabaki katika hali gani! unachefua sana! nilikuwa nakuheshimu sana kabla!
Unataka kuniambia uchumi hauruhusu kwa iyo ukishikwa makalio we cheka tu,inama uitikie ndio afande.,we akili zako nukta,shujaa ni yule anaejitetea mpaka tone la mwisho..Nimesoma waraka wako nimeshindwa kuelewa;
1.0 Kichwa cha habari na content yenyewe. Kwa nini uliamua kuuita waraka kwa JWTZ??
2.0 Vita ni fedha. Kwa hali ya sasa ya Tanzania hatutakiwi kupigana vita yoyote ile. Nchi iliyoshindwa kujitegemea kibajeti tokea uhuru mpaka leo, bado inategemea misaada ku "subsirdise" bajeti yake halafu ikapigane vita!!!
Nashindwa kuelewa mwandishi kama wewe unameshindwaje kuelewa kuwa Tanzania ya JK hali ya uchumi ni mbaya labda kuliko hata Mkapa alipokuwa akiondoka. Kama serikali inashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kukosa fedha itawezaje kugharamia vita ambayo ni ghari kuliko miradi ya maendeleo??? Deni la Taifa kila siku linakuwa kama mimba lakini hatuoni kinachofanyika kisha tukapigane vita!!! Ni jambo la kushangaza sana.
Ukweli kama hujui tukusaidie, serikali ya sasa imebaki kulipa mishahara tu na kupiga propaganda kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia fulani huku mwananchi wa chini akizidi kuzama katika dimbwi la umaskini.
3.0 Umeshawahi kujiuliza athari za vita tuliyopigana ya kumng'a Iddy Amini?? Ile vita ilikuwa haikwepeki lakini uchumi wa nchi ulitetereka sana, itakuwaje leo Taifa la kujisifu kwa kupewa misaada tukapigane vita??
Kwangu mimi huu ni waraka wa kishabiki na kipuuzi kabisa.
rutajumbukirwa[font=&]kuna wanyarwanda na pro kagame lukuki humu jf ,subiri utawaona miongoni mwao ni[/font]
[font=&]R.B[/font]
[font=&]adolay[/font]
[font=&]Koba[/font]
[font=&]MUKAMASIMBA[/font]
Tumeanza kuwatambua watutsi humu JF. Tujadili mada, kejeli na matusi tuviweke pembeni.
Ukifa wakati ukiwatetea wanyonge wenzako ni thawabu kubwa. Mungu akipenda tutaushuhudia ukombozi wa Wacongo kabla ya kufa kwetu.
Unataka kuniambia uchumi hauruhusu kwa iyo ukishikwa makalio we cheka tu,inama uitikie ndio afande.,we akili zako nukta,shujaa ni yule anaejitetea mpaka tone la mwisho..
Sikutaka kukujibu, lakini ngoja nijaribu. Hoja yako ya kwanza sijajua wapi huelewi. Unaweza kuwa sahihi kwa sababu headline za kifilosofi huwa zinawasumbua wengi pale wanapojaribu kuunganisha na hoja iliyo ndani. Pili, hii vita inagharimiwa na UN, ndiyo maana kuna majeshi hadi kutoka Afrika Kusini. Tunachojaribu kukifanya hapa ni kuhakikisha tunakuwa na minimum causalities kwa askari wetu. Tatu, kuna maeneo ambayo amani haiji isipokuwa kwa ncha ya upanga! hatushangilii vita, lakini tuangalie namna Kagame anavyosumbua eneo hili la maziwa makuu.
Nimekusoma vizuri nadhani yote uliyoyaandika yana ukweli nimesikitishwa na habari za Rais wetu kutaka kikao cha usuluhishi kitu ambacho nikosa sana!!https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kuitisha-kikao-cha-usuluhishi-ahuna-kosa.htmlSioni kwanini tusianzishe Jumuiya yetu kwa kuwakaribisha DRC na Burundi. Sisi ni taifa kubwa. DRC ni taifa kubwa pia. DRC na Tanzania tuna rasilimali nyingi mno. Faida za kujitoa EAC ni kubwa kwetu kuliko kuendelea kuhangaika na hawa wapenda vita. Tuwaache waanzishe yao, na sisi tuanzishe yetu. La, hilo kama haliwezekani, tujikite zaidi SADC ambako kuna soko pana kuliko EAC.
Tukijitoa EAC atakayeumia zaidi ni Kenya maana bidhaa na uwekezaji wake mkubwa kauelekeza Tanzania. Soko lake kubwa lipo Tanzania. Wanajidanganya tu.
Tusiendelee kuwabembeleza watu wasiokuwa na shukrani. Tuwatakie heri katika ndoa yao hii mpya ambayo sioni uhai wake. Hizi ni hasira za mkizi ambazo mara zote humnufaisha mvuvi. SADC ni bora zaidi. Tupeleke nguvu zetu kwenye SADC.
Kagame na Museveni walisaidiana kuichukua Uganda. Museveni alimsaidia Kagame kuitawala Rwanda. Sasa wanasaidiana wachukue sehemu ya DRC. Museveni anamsaidia Kagame katika hili. Tutambue kuwa inayofuata ni Tanzania. Si ajabu wale Wanyarwanda waliokuja siku nyingi sasa wakadai wanabaguliwa, na kwa sababu hiyo wakaanzisha vita ya kutaka kutambuliwa au kujitenga na kuwa sehemu ya Rwanda na Uganda (Bahima Empire).
Njia pekee ya kumwondoa Rais Kagame ni hii aliyotusaidia kuiweka, yaani vita. Kuichokoza Tanzania ni njia ya kuelekea ukingoni mwa utawala wake. Amepigana kwa muda mrefu na wasiojua vita. Amejaribu kuitisha Tanzania akidhani atafanikiwa. Kinachotakiwa sasa ni kumwonyesha kazi. Safari iliyoanzia Goma inastahiki ihitimishiwe Kigali. Kama kasahau, arejee kwenye historia ili ajue kilichompata nduli Iddi Amin Dadaa. Buriani Kamanda Khatibu Mshindo.
manyerere@hotmail.com
[/COLOR][/SIZE]
Wewe ndio unaonyesha jinsi gani hata form two hujamaliza,kama issue nikumng'oa M23 hizo troops za PK alizopeleka mpakani anataka kuhalalisha nini?,JWTZ walioko DRC ikitokea Pk anarusha makombora DRC hata wapiga hata kama wanailinda Goma bali atawapiga Wanajeshi wa Congo,na ikitokea kawaua Jwtz tukae kimya sio...idiotHaya ndiyo matatizo ya kujibishina hoja na vijana waliomaliza Form Four mwaka jana. Hivi umesoma between line au mekurupuka tu???
Pigana vita isiyoepukika mfano vita za uvamizi wa nchi, kudhalilisha utaifa wa mtu na maslahi lakini siyo kama hiyo mnayotaka kutetea.
Hapo jambo la msingi ni kuwapiga M23 kisha kulijengea Jeshi la DRC uwezo wa kulinda mipaka yake na watu wake na siyo kwenda kupambana na Kagame pasipo na ulazima.
Nimekusoma vizuri nadhani yote uliyoyaandika yana ukweli nimesikitishwa na habari za Rais wetu kutaka kikao cha usuluhishi kitu ambacho nikosa sana!!https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kuitisha-kikao-cha-usuluhishi-ahuna-kosa.html