Waraka wangu kwa JWTZ, Watanzania

Waraka wangu kwa JWTZ, Watanzania

sijui kama una ujasiri wa kumwitw Manyerere mjinga !!! Labda kana huishi TZ!!!
Manyerere amekaa ikulu ya Nyerere miaka 20!!

pointless kabisa! Yaani ukikaa ikulu ndo huwezi kuwa mjinga? Pinda mpaka leo yupo huko lakini ni mjinga tu!
 
Nikukumbushe, Majeshi yetu yapo nchini Congo kwa bandera ya UN.
Pili, ni rahisi kusema uliyosema kwakuwa Tanzania bado hayajatukuta.
Jaribu kuvaa viatu vya wakongo kisha tazama swala hili tena.
Nikuulize, unaunga mkondo mambo anayoyafanya Kagame na jeshi lake nchini DRC?
Unahabari kabla ya kua under mwavuli wa UN walikua wamejipanga kama SADC? wakiwa na mpango wakuishambulia rwanda,lakini UN ikaliona hilo ikaiweka under UN ili wasiweze vuka mipaka na kuleta vita kubwa katika eneo la maziwa makuu hilo rwanda inalijua,wameandaliwa materahamwe wengi nakuvalishwa manguo ya wanajeshi wa FIB hilo nalo linatambuliwa,sasa nyie hamjui kinacho endelea waachieni pk na jk watayamaliza,au muulizeni jk anajua alipolikoroga,msimsingizie pk.
 
Unahabari kabla ya kua under mwavuli wa UN walikua wamejipanga kama SADC? wakiwa na mpango wakuishambulia rwanda,lakini UN ikaliona hilo ikaiweka under UN ili wasiweze vuka mipaka na kuleta vita kubwa katika eneo la maziwa makuu hilo rwanda inalijua,wameandaliwa materahamwe wengi nakuvalishwa manguo ya wanajeshi wa FIB hilo nalo linatambuliwa,sasa nyie hamjui kinacho endelea waachieni pk na jk watayamaliza,au muulizeni jk anajua alipolikoroga,msimsingizie pk.
Hebu nijubu hili, unakubali kuwa kuna uhusiano na ushirikiano kati ya M23 na Kagame? tuanzie hapo.
 
sijui kama una ujasiri wa kumwitw Manyerere mjinga !!! Labda kana huishi TZ!!!
Manyerere amekaa ikulu ya Nyerere miaka 20!!

Kwahiyo kukaa Ikulu ndo kuzifahamu haki za watanzania na mahitaji yao? Hata Ramadhani Ighondu ni mkaazi wa Ikulu na amefanya nini kuhusu Ulimboka?. Lazima tujifunze kuukubali ukweli hatakama ni mchungu.
 
Manyerere Jackton, kuna makundi mangapi ya waasi Kongo? Kwa nini watoe kundi moja tu? Why do you undermine the military power of Rwanda? Hujui Angola, Namibia na Zimbabwe walichemsha? Mataifa gani makubwa yako nyuma ya haya makundi? Silaha zilizokuwa zikishushwa Mwanza airport (kumbuka kashfa ya silaha na mapanki) zilipelekwa kwa waasi gani?
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye red nilikuuliza jana hicho kisingizio cha FDLR kimeshachuja.....nitajie ni kiongozi gani wa FDLR ambaye either alikamatwa au alijisalimisha ambaye amefunguliwa mashtaka Rwanda...? Viongozi wote wa FDLR wameishia kupewa madaraka Rwanda, na wapiganaji wa zamani wa FDLR waliojisalimisha mmeishia kuwarudisha kwenye mapigano Congo kwa kutumia proxy forces zenu CNDP = M23. Mfano wa viongozi wachache wa FDLR niliokwambia ambao umekacha kujibu ni hawa Major General Paul Rwarakabije, Lieutenant-Colonel Samuel Bisengimana, Lt. Col. Idrissa Muradadi, n.k .......! Kama kweli FDLR wangekuwa ndio wote wahusika wa genocide kwanini hao waliojisalimisha hamjawafungulia mashtaka? Leo hii Mpiranya akijisalimisha popote alipo atapewa kazi UN au atapelekwa Arusha ICTR.......?

Kikubwa ni kuwa kwa kutumia jina la genocide na mafuvu ya watu walioawa bila hatia na FAR pamoja na RPF, Kagame na kagenge chake cha wahuni bado wana kiu ya damu ya kuua watu wasio na hatia na dunia imesema basi. Kagame na kagenge chake cha wahuni walianza mauaji tangu wakiwa Uganda, waliua watu wengi sana kule Northern Uganda mpaka Museveni akaona imetosha, wakahamia Rwanda wakaendelea kuua...! Ndio maana hata alipoulizwa na Gen. Romeo kwanini hasitishi mapigano Kigali na kuokoa maisha ya watu hata Watutsi wenzake yeye Kageme alijibu 'acha hao watutsi wafe kwa vile hiyo nayo ni sacrifice yao katika vita'.....hii ipo kwenye records..!

Inshallah....with JWTZ tutakunywa chai Kigali...!
Kwahilo rwanda imelitatua kabisaa kwa FDLR anaye rudi na kuomba msamaha na kujitenga na itikadi za kimbari na kutambulika kua hana hatia ya mauaji anapokelewa na kua integrated in society ndio hao unaosema,sasa hao waliobaki ni wale ambao either wanamakosa makubwa walitenda rwanda au wanaitikadi za kimbali ambazo hawataki kuachana nazo,nafikiri unajua hatakama unakesi ya mauaji ukakiri na kuomba msamaha unaweza hurumiwa au kupunguziwa kifungo,sasa rwanda haiwezi kulazimishwa kuongea na hao wauaji wakati wao hawataki kutubu dhambi zao na kukubali kuachana na hiyo itikadi ya kimbali,hiyo wanyarwanda hawawezi kuikubali nisawa na kupatia zawadi mtu aliye kufanyia ukatili.
 
Ni upuuzi kudhani kuwa wananchi wa Congo waendelee kuteseka na majirani zake hasa Tanzania tuendelee kubebe mzigo wa wakimbizi kisa ni Rwanda.......! UN na SADC zimesema sasa basi...! Hiyo convincing unayoona wewe kuwa haijafanyika ni kujidanganya, intervention brigade ina mandate ya kumtwanga RDF kwanza kwa kupitia proxy force yake ya M23 then akishambulia FIB, tunavuka mpaka kupitia Kagera na South Kivu...! Membe ameshatoa onyo kwa UNSC majuzi...!

Inshallah with JWTZ tutakunywa chai Kigali....!
....si chai peke yake lazima iwe na kitafunwa ambayo ni mishikaki ya kagame pamoja na na binti yake Ruta
 
306681_10151063016359743_1581996414_n.jpg
 
Manyerere,

Kweli una mawazo ya al-qiada. kweli kuna mfugaji ambaye amewahi kuchoma nyumba na mashamba? huu ni uchochezi kabisa, uliza mtu yeyote kutoka Kagera, hawa watu wanaishi kwa kuliwa. Wanaliwa na police, immigration, idara ya wanyamapori burigi, nk. Walikuja kwasababu kwao hakuna ardhi, huo ndo ukweli, wakati mipaka inawekwa walipewa ardhi kidogo, basi.

Lakini usieneze chuki eti wanachoma mashamba, etc, nenda kafanye utafiti ache jaziba, na usilifanye gazeti lako kuwa la itikadi la ki-nazi, we ni mwandishi wa habari una wajibu wa wananchi, wasomaji na kuleta utengamano wa kijamii na maendeleo sio kuchochea chuki, make makala yako imejaa jazba sana

haswaa!
 
HEBU ANGALIENI ITIKADI ZA HAO WANAOITWA INTERAHAMWE(GENOCIDERS) DHIDI YA WATUSI JE UNAFIKIRI NIHAKI FIB KUWAUNGA MKONO?

[h=1]Hutu Ten Commandments[/h] From Wikipedia, the free encyclopedia
Jump to: navigation, search
The "Hutu Ten Commandments" (also "Ten Commandments of the Bahutu") was a document published in the December 1990 edition of Kangura, an anti-Tutsi, Hutu Power Kinyarwanda-language newspaper in Kigali, Rwanda. The Hutu Ten Commandments are often cited as a prime example of anti-Tutsi propaganda that was promoted by extremists in Rwanda following the 1990 invasion by the Rwandan Patriotic Front and prior to the 1994 Rwandan Genocide.[SUP][1][/SUP][SUP][2][/SUP][SUP][3][/SUP][SUP][4][/SUP] The chief editor of Kangura, Hassan Ngeze, was convicted of genocide and crimes against humanity in 2003 by the International Criminal Tribunal for Rwanda and was sentenced to 35 years' imprisonment.[SUP][5][/SUP]

[h=2]Text[/h]
The Hutu Ten Commandments

1. Every Hutu should know that a Tutsi woman, whoever she is, works for the interest of her Tutsi ethnic group. As a result, we shall consider a traitor any Hutu who

  • marries a Tutsi woman
  • befriends a Tutsi woman
  • employs a Tutsi woman as a secretary or a concubine.
2. Every Hutu should know that our Hutu daughters are more suitable and conscientious in their role as woman, wife and mother of the family. Are they not beautiful, good secretaries and more honest?
3. Hutu women, be vigilant and try to bring your husbands, brothers and sons back to reason.
4. Every Hutu should know that every Tutsi is dishonest in business. His only aim is the supremacy of his ethnic group. As a result, any Hutu who does the following is a traitor:
  • makes a partnership with Tutsi in business
  • invests his money or the government's money in a Tutsi enterprise
  • lends or borrows money from a Tutsi
  • gives favours to Tutsi in business (obtaining import licenses, bank loans, construction sites, public markets, etc.).
5. All strategic positions, political, administrative, economic, military and security should be entrusted only to Hutu.
6. The education sector (school pupils, students, teachers) must be majority Hutu.
7. The Rwandan Armed Forces should be exclusively Hutu. The experience of the October 1990 war has taught us a lesson. No member of the military shall marry a Tutsi.
8. The Hutu should stop having mercy on the Tutsi.
9. The Hutu, wherever they are, must have unity and solidarity and be concerned with the fate of their Hutu brothers.
  • The Hutu inside and outside Rwanda must constantly look for friends and allies for the Hutu cause, starting with their Hutu brothers.
  • They must constantly counteract Tutsi propaganda.
  • The Hutu must be firm and vigilant against their common Tutsi enemy.
10. The Social Revolution of 1959, the Referendum of 1961, and the Hutu Ideology, must be taught to every Hutu at every level. Every Hutu must spread this ideology widely. Any Hutu who persecutes his brother Hutu for having read, spread, and taught this ideology is a traitor.[SUP][1][/SUP]
Hizi commandments ndizo zinatumiwa na watu wengi humu kuendeleza chuki dhidi ya watusi!
 
Na wakati yote hayo yanatokea, Mwenye Nchi anazurura...this time kujumuika na wanafunzi huko Austria ktk mkutano tuliopaswa kuwakilishwa na balozi au waziri.

Yea, mpo sahihi kutanguliza uzalendo lakini let's not put emotions in front of common sense. Tuna matatizo makubwa ndani ya nchi yetu, last thing we need is war. Ni mtu asiye na busara pekee anayeweza kushauri tuingie vitani (au kuishambulia Rwanda by proxy kwa jukumu letu la ulinzi wa usalama DRC).

TUPO VITANI DHIDI YA MAFISADI NA WAUZA UNGA, and we all know who's winning the war....na kwa kusikitisha zaidi, which side our Dear President Kikwete is on.

Turejee nasaha za Sun Tzu katika Art of War (google): vita iwe last resort.
 
Manyerere,

Hivi kweli Rwanda hana maslahi Congo? Mnyonge mnyongeni haki yake mpe. Mwaka 1994 kulitokea genocide. We unawaonea huruma waliokufa kwenye ndege ya rais, na sio wanawake, watoto, nk. walliouwawa kikatili sana na wahutu wenye msimamo mkali, ambao baadae walienda Congo, ambako wapo hadi leo. Na viongozi wao ni walewale waliopanga na kufanya genocide.

FDLR kazi yao ni moja, kuja kumaliza kazi. Hivi pale Congo kungekuwa na kikundi chenye msimamo wa kuiangamiza Tanzania tungekaa na kusubiri tu? Nadhani Rwanda kuwa na mkono wake Congo kuna self-defence justification.

Kuhusu wizi wa madini, ndio, lakini uje kuwa haya madini yanaenda ngambo, yanachimbwa na watu wenye mtaji na teknologia, sio wana-mgambo wa M23 wenye afya mbaya.

Kuhusu EAC, some Treaty inasemaje, kasha uishauri Tanzania cha kufanya, usi-argue kama watoa maoni wa JF. Kuhusu bandari, hili sio suala la uzalendo, ni suala la biashara, watanzania wengi hupitisha magari yao Mombasa, then Horiri.

Kuhusu Watutsi, sioni kama ni jukumu lako kama mwandishi kushambulia kabila Zima, kama Kagame ana siasa ambazo hazikupendezi, basi shughulika nae.

Sidhani kama ni sahihi kuwashambulia Wakwere kwa makosa ya JK, hiyo ndo inachochea genocide. Ndege ya rais ilivyotunguliwa, wahutu walisema imetnguliwa na Watutsi, wakaua hadi motto mchanga, wakati maskini labda alikuwa ni Kagame na jeshi lake.

So, ninaposema ume-nidsappoint, ni kwamba mwandishi mwenye hadhi yako, hapaswi kuandika akiwa na hasira, anaandika kwa hoja kuisaidia jamii kufanya maamuzi sahihi. Au la, usiitumikie jamii kama mwandishi, nenda omba kazi jeshini, fanya mambo ya kizalendo zaidi, au hata mgambo.

Lakini kumbuka kalamu yako inaweza kuanzisha vita saa yoyote, ndoo maana waandishi wa Rwanda wamehukumia ICTR, yule Joshua Arap Sang wa Kenya yupo the Hague, etc. Leo hii humu ndani kuna uchochezi, mgao wa umeme Kagera wanasema ni Kagame, Bandari watu walitunga uongo, vichwa vya habari eti ni kagame., etc. hata kama hatumpendi waandishi wa habari lazima wawe weledi sio wachochezi

mkuu mimi nakusapoti sana
 
Hii ni makala ya kichochezi. Manyerere hapa anaonyesha uzalendo uliopotoka (misplaced patriotism).

Tofauti kati ya Tanzania na Rwanda bado kabisa hazijafikia hata chembe ya hatua ya kuzilazimu nchi hizi kwenda vitani. Hivi endapo ingekuwa nchi zikiwa na tofauti kidogo tu kati yao basi inabidi ziende vitani hii dunia ingekalika kweli?

Kama watu wote wangekuwa na mawazo kama ya Manyerere basi saa hizi China ingekuwa inapigana na Japan (mgogoro kuhusu visiwa vya Senkaku au Diaoyu), India ingekuwa inapigana na Pakistan (mgogoro kuhusu eneo la Kashmir), Urusi ingekuwa inapigana na Japan (mgogoro kuhusu visiwa vya Kuril), Kenya ingekuwa inapigana na Uganda (suala la kisiwa cha Migingo), Marekani ingekuwa inapigana na Urusi (suala la Edward Snowden), Ethiopia ingekuwa inapigana na Misri (mgogoro kuhusu maji ya Mto Nile)….orodha ni ndefu.

Sitashangaa Manyerere, kutokana na uchungu alionao kwa Tanzania, akishauri tupigane na Rwanda na Malawi kwa wakati mmoja. Haya mambo ya vita yamepitwa na wakati. Tulipigana na Uganda zaidi ya miaka 30 iliyopita na athari zake tunaziona hadi leo. Anachofanya Paul Kagame ni kupiga kelele tu na sidhani kama makelele yake ni tishio kwa Tanzania kwa namna yoyote ile.
 
Hebu nijubu hili, unakubali kuwa kuna uhusiano na ushirikiano kati ya M23 na Kagame? tuanzie hapo.

Kwahiyo mke wajirani yako akitembea nje ya ndoa yake wew huenda kumdhibiti ?? ya M 23 sisi watanzania yanatuhusu vipi? Yes kwasasa kwasababu tumewafuata kwenda wachokonoa lazima wajihami kutushambulia itakuwa haki yao.

Hebu nawewe tueleze sababu za msingi kabisa kutufanya watanzania kuingia vitani tukiacha watanzania wakiteswa na umasikini, maradhi na ujinga na wengi wakipoteza maisha ni zipi ili tuendelee.
 
ahahahhaa,kwani jf niyawabongo tu?mimi ni pro-intelligent people,PK ni mwanaume washoka bwana,yani anawa challenge hao wazungu wenu mpaka unaona nywele zao zina simama kichwani na pua kugeuka nyekundu,jk anaweza?ahahaha nakumbuka hotuba yake wakati waziara ya OBAMA mmmh ni aibu kwa mwafrika,yani kuombaomba tu,hivi watu dunia nzima wanahaha kagame,rwanda,kagame,rwanda ahahhaha achana na ile namba pk nikichwa cha kipekee afrika kama tungekua na pk kama 10 afrika nafikiri tusingekua tunatiwa vidole na hao wazungu.
Kama yeye kidume kweli hayo majeshi yake aliyoyapeleka mpakani na DRC aue wanajeshi wa JWTZ tujue anatisha...
 
Hii nayo ni mpya uhuru wa kuongea umefanya tujue mengi hata kama hayana maana.
 
Manyerere Jackton,

..naomba nigusie suala la EAST AFRICAN COMMUNITY.

..hapa nitakurejesha kwenye Tume ya kukusanya maoni ya PROFESSOR. SAMWEL WANGWE.

..wa-Tanzania walio wengi walikataa ushirikiano ambao uko too binding kama huu wa sasa hivi.

..zaidi, wananchi wa maeneo ya MIPAKANI ndiyo waliokuwa more vocal kupinga Federation.

..serikali iliamua kuwapuuza wananchi na kufanya wanavyotaka wao, sasa wameanza kushuhudia VITUKO vinavyoendelea ktk EAC.
 
Last edited by a moderator:
Huu waraka inabidi uhifadhiwe kwani unaweza kutumiwa kama ushaidi wa uchochezi dhidi ya watusi,Hata yule hasan ngeze mwandishi aliye chapisha 10 hutu commandments hivi sasa yuko ananyea ndoo arusha.
 
Back
Top Bottom