Lukansola
JF-Expert Member
- Sep 5, 2010
- 5,435
- 1,611
Wewe Fadrashid; acha kuupotosha umma. Unajua maana ya vita vya badri??? kwa hiyo unataka kusema kuwa hapo mnapigana vita ya badri? kwa minajili na mafundisho sawia ya kupigana vita vya badri, ndicho mnachokifanya?????
Na mimi pia ni Muislam tena sio wa kuburuzwa. Nina tenda, nina abudu kwa elimu na si kibubusa.
Acheni kuiharibu dini, hayo mnayofanya hayako kwenye mafundisho ya dini. mwenye elimu safi ya dini hawezi fanya hivyo kama mnavyofanya kwa kisingizio cha dini.
Dini ya kiislam inaendeshwa kwa elimu na hekima, na sio kwa ghadhabu na ujinga.
Kwa haya mnayoyafanya mkasababisha mtume wetu na Mungu wakatukanwa, hakika nyinyi ndio mtakuwa mmewatukanisha na mtaubeba mzigo wake, kwa hayo yaliyosababishwa kwa mikono yenu.
Leo mnasingizia mafundisho ya kiislam ili kuhalalisha hayo???? mwalimu mkuu wetu mkuu na kiigizo chetu sisi waislam ni Mtume, kwa hayo myafanyayo kwa kisingizio cha uislam ni kumsingizia mtume, kwani hakufundisha hayo myatendayo. Na dhambi ya kumsingia mtume ni kubwa sana. Hayo mnayoyafanya kwa kisingizio cha uislam hayapo popote katika mafundisho ya dini yetu.
Busara imetawala
Mawazo yako mleli, ubarikiwe sana mkuu.