Waraka toka Ikulu: Hebu tuujadili...

huu sasa ni upuuzi; kama kweli walichoandika Ikulu ni cha kweli kutoa tamko ni kuthibitisha hofu yetu sisi wengine. Kuna watu hawana kazi isipokuwa kufikiria kila siku watoe tamko gani.

Honestly, sioni kosa. Kwa sababu:-

Kwanza,hawajasema kwamba hawatamtafuta au ya kwamba ndio issue imeishia hapo. Pili, they did it out of caution. I'm pretty sure kama kadi hizo au taarifa ya kwamba kuda kadi zinatembelea huku mchangishaji akiwa Mke wa Rais, nina uhakika kwamba watu bado wangesema, "Mke wa Rais aanza utapeli".
Pia, wangekaa kimya ingeonekana pia kuwa ni uzembe za kwamba Mke wa rais anahusika katika jambo hilo.

Ina maana kweli hakuna mtu huko Ikulu ambaye angewashauri NINI hasa cha kufanya badala ya kutoa tamko?

Sidhani kwamba ikulu itaishia hapo kutoa tamko tu na kumuacha aende zake. Hatuna uhakika vile vile kama hawajashauriwa cha kufanya. nadhani moja kati ya hatua za kushughulikia tatizo ni kwanza kuwatahadharisha watu ili damage isiwe kubwa then waendelee na kumtafuta mhusika. Wameshapata jina lake, sehemu alipo na hata kazi yake na mahala pale pa kazi. tusubiri baada ya muda tuone kama amechukuliwa hatua au la then ndio twaweza sema ikulu imeshindwa.
Unless otherwise, it's not safe to say kwamba ikulu haina kitu hasa cha kufanya kuhusu tatizo lenyewe.
 
tanzania utaipenda kweli ikulu inashindwa kumshughulikia mtu kama huyu. Serikali inayomiliki dola na kila aina ya mawasiliano kweli sijawahi ona maajabu ya aina kama hii. Na salima kikwete ni nani kwenye taifa? tujadililini maneno ya maendeleo wala sio huu ujinga wa ikulu wakushindwa kutumia akili kutatua hata matatizo yaliyo ndani ya uwezo wao.
 
Ukweli ni kwamba huyu mkurugenze pale Ikulu hana kazi yoyote ya maana hivyo ni mtu wa kujishuku na kuona anapwaya.Maamuzi yake yametawaliwa na wasiwasi mwingi na sintofahamu ya yale anayosimamia/kuyatoa, huwa si mtu wa kufikirisha akili kujua mbivu ni zipi na mbichi ni zipi .Amekuwa akitoa matamko hata kwa vitu visivyo na vichwa wala miguu,huu ni uzaifu mwingine wa taasisi kubwa kama ikulu .Taasisi yoyote ikashakuwa na watu wasio na upeo /maono ya mbali matokeo yake ndio haya.
Kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni!!
 
,Bwana Kabambara anatumia jina la Mheshimiwa Salma Kikwete, Mke wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nembo ya Taifa kuonyesha kuwa Mheshimiwa Mama Kikwete ndiye mchangishaji na Mgeni Rasmi kwenye matembezi ya shughuli yakuchangia maendeleo ya shule yake.Aidha, amekuwa anadai kuwa Mama Kikwete ndiye atakuwa Mgeni Rasmi kwenye shughuli hiyo.

Inawezekana ni makubaliano na mama bila dingi kujua.

Sasa dingi kafahamu
na mishen imejamba. Duh, wewe kweli hauendi kuishi na Viking?
 
TAARIFA KUTOKA IKULU

Kumekuwepo na wimbi la vijana wasio waadilifu hasa kutoka jukwaa la MMU(JAMII FORUMS) wanaojinadi kumtokea na kukubaliwa mtoto wa mkuu mheshimiwa mwa#asha.tunapenda kuuarifu umma kuwa taarifa hizi si za kweli kwani mheshimiwa mwa#asha ni mdogo na anaendelea na masomo na kamwe hawezi kuwakubali warugaruga wa jf,kwanza wamezidi ujuaji sana.

IMETOLEWA NA WAZEE WA IT
MAGOGONI.

ha ha ha ha ha ha ha aaaaaaaaaa daaaah Jackbauer!!nimekubali umeamua kutuvunja mbavu!!ni sawa maana ikulu sasa imegeuka pango la walanguzi na wachumia tumbo!!acha ikulu kwakila watakachojisikia kusikilizisha umma basi watupe tu!!
 
Mwisho wa tamko wamemalizia " Hili ni kosa la jinaimbali na kwamba vitendo vya namna hii husababisha usumbufu kwa jamii na kwa viongozi husika" natumaini hizi taarifa amepewa na mkuu wa polisi sehemu iliposhule
 
Tangazo lenyewe lina makosa kibao, ukweli utabaki kuwa hadhi ya Ikulu imeshuka vibaya sana. 2015 ni mbali jamani!
 
huu sasa ni upuuzi; kama kweli walichoandika Ikulu ni cha kweli kutoa tamko ni kuthibitisha hofu yetu sisi wengine. Kuna watu hawana kazi isipokuwa kufikiria kila siku watoe tamko gani. Ina maana kweli hakuna mtu huko Ikulu ambaye angewashauri NINI hasa cha kufanya badala ya kutoa tamko?

Naishangaa Ikulu...... Hivi inashindwa kumkamata mtu huyu Na kumpeleka mahakamani.
 
Hii taarifa inashangaza sana....namfahamu Kabambara vizuri toka enzi za miaka ya tisini akimiliki shule ya Chekechea known as SAINT MOSES...Kama kawaida yake sherehe za shule yake zilihudhuriwa na wakuu wa nchi na mikoa kama A.H.Mwinyi,James Luhanga n.k.
Mara kwa mara huwa anaonekana hata kwenye sherehe za ikulu....na amekuwa akiambatana na viongozi (hata kwenye msiba wa Regia,alikuwa na viongozi na aliaga maiti pale walipoitwa wakuu kwanza.
Kwanza huwa sijui kama ni usalama wa taifa au? Pili iweje msumbue wananchi kwa mtu ambae mnamjua?
Na tutaamini vipi kama kweli hawajaongea na mama Salma?
 
whatever the case kama ikulu wameona ni tatizo kwa umma-wanamlalamikia nani awasaidie? maana msaada wa umma ni kwenye ballot huku ni kushindwa kazi
 
huu sasa ni upuuzi; kama kweli walichoandika Ikulu ni cha kweli kutoa tamko ni kuthibitisha hofu yetu sisi wengine. Kuna watu hawana kazi isipokuwa kufikiria kila siku watoe tamko gani. Ina maana kweli hakuna mtu huko Ikulu ambaye angewashauri NINI hasa cha kufanya badala ya kutoa tamko?

IKULU inajiweka katika level ya chini kabisa kwa kutoa matamko kama haya. Hapa kuna mambo yamejificha sana, huenda mama Salma kweli alikuwa approached na akakubali na jamaa ameamua kutumia kukubali huko kuchangishia kitu ambacho kimewaudhi Ikulu na kuona wanadhalilishwa na kuamua kumtupa bwana Kabambara nje ya basi.

Kama ninachoongea hapo juu si cha kweli basi bwana Kabambala ana qualify kabisa kuwa mhalifu wa kughushi na kutoa taarifa za uwongo zinazoidhalilisha Ofisi kuu ya uongozi wa nchi. Lakini pia hili ni ombwe lililopo kwenye sheria zetu za public fundraising. Katika nchi zenye kujua umuhimu wa hili 'Public Fundraising' huwa inaambatana na organisation kuwa na Charitable status ambayo ni lazima usajiliwe na mamlaka husika na fedha zinazokusanywa ziwe ni kwa manufaa ya umma (Public benefit) kama kuhudumia watoto yatima, wagonjwa masikini etc kwa Tanzania nafikiri ni NGO, sasa sijui kama sheria ya NGO ya mwaka 2002 http://www.tnnc.go.tz/onlinedocuments/NGO Act 2002.pdf inaelezea mambo haya.

Ni marufuku mtu kufanya fundaraising for private use nchi zote zile duniani zilizo na sheria ya Nonprofit oreganisations. Kitendo cha Kabambara si cha kiungwana kama kweli anachangisha fedha kwa shule yake binafsi anayoitumia kama biashara, ila kitendo cha IKULU kuja na kauli hii ni kibaya zaidi, maana kinafanya nchi ionekane haina vyombo vya kusimamia sheria. Kabambara alikuwa ni wa kukamatwa na kushitakiwa na Jeshi la polisi ndilo hasa lingepaswa kutoa tahadhari hiyo si Ofisi kuu ya uongozi wa nchi.
 
salma kikwete ni mke wa Rais a.k.a First Lady so mtu yoyote binafsi akitumia jina la first lady kwa shuhuli zake binafasi bila kupata idhini kwa either mama mwenyewe au ofisi ya mke wa rais then ikulu ina haki ya kutoa hilo tamko... mitchelle obama angefanyiwa hivi white house inge release a statement coz first lady ni mke wa Rais and anakua protected na usalama wa taifa na ikulu in general

Usimfananishe Salma Kikwete na Michelle Obama kwani utofauti wao ni mkubwa sana kielimu na hata mazingira wanapoishi!! Marekani Michelle Obama hawezi kuwa na taasisi kama WAMA ya Salima KIkwete ambayo inatembeza bakuri kupata misaada lakini hakuna accountability yeyote jinsi ya misaada hiyo inavyotumiwa. Salma Kikwete amejihusisha sana katika harambee za kuchangisha fedha kusaidia shule mbalimbali na nadhani kwa misingi hiyo hiyo huyo bwana akataka amtumie kupata ufadhili wa shule yake. It is unfortunate kuwa huyu bwana mwenye shule amedhalilishwa kiasi hicho kwani nadhani huyu mama lazima hapo awali alionesha dalili za kutaka kusaidia na ndio maana jamaa akaanza kutembeza bakuli!!
 
Back
Top Bottom