Waraka toka Ikulu: Hebu tuujadili...

kumbe salma nae ni kiongozi wa kitaifa?kachaguliwa na nani?haya mamlaka yake yapo kikatiba kwel?yapi majukumu yake?
 
Samaki siku zote hujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe,tume experience siku zote ukiona Ikulu kupitia kurugenzi yake ya habari ina kimbilia kwenye vyombo vya habari kukanusha jambo kwa haraka ujue kuna kosa lqa ufundi limefanyika na kinachofanya ni kuupotosha ukweli halisi.

Ipo wapi idara ya usalama wa taifa iliyojijengea heshima wakati wa utawala wa mwalimu,au kazi yake ni kudhibiti vyama vya upinzani?
 
THEUNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,

THE STATE HOUSE,

P.O. BOX 9120,

DAR ES SALAAM.

Tanzania.
TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku chachezilizopita, Mkurugenzi wa Shule ya Chekechea ya Moses Nursery ya Yombo Vituka,Dar es Salaam, Bwana Moses Kabambara amekuwa anasambaza kadi kwa watu binafsi,makampuni, mashirika na ofisi za ubalozi zilizoko nchini akisaka michango kwaajili ya ununuzi wa madawati na ujenzi wa madarasa na uzio wa shule yake.

Katika kadi yake yakuomba michango na kwenye taarifa anazozisambaza kwenye vyombo vya habari,Bwana Kabambara anatumia jina la Mheshimiwa Salma Kikwete, Mke wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nembo ya Taifa kuonyesha kuwa Mheshimiwa Mama Kikwete ndiye mchangishaji na Mgeni Rasmi kwenye matembezi ya shughuli yakuchangia maendeleo ya shule yake.
Aidha, amekuwa anadai kuwa Mama Kikwete ndiye atakuwa Mgeni Rasmi kwenye shughuli hiyo.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kuuarifu umma wa Tanzania kama ifuatavyo kuhusu suala hili:
(a) Kwamba Mama Salma Kikwete kamwe hajapata kuridhia kuwa Mgeni Rasmi katika matembelezi hayo
(b) Kwamba Mama Salma Kikwete hajapata kukubali kuwa mchagishaji ama hata mshiriki wa aina yoyote katika uchangishaji fedha kwa ajili ya shule hiyo.
(c) Kwamba Bwana Kabambara anaufanyia udanganyifu umma ili uweze kuamini kuwa Mama Salma Kikwete amekubali kushiriki katika shughuli za uchangiaji fedha shule yake.

Tunapenda kupitia taarifa hii kuutahadharisha umma kuwa macho na vitendo vya baadhi ya watu wanaotumia majina ya Viongozi wa Kitaifa kuchangisha ama kukusanya fedha ama hata kufanya mambo mengine yenye kulenga manufaa au maslahi binafsi. Hili ni kosa la jinaimbali na kwamba vitendo vya namna hii husababisha usumbufu kwa jamii na kwa viongozi husika.

Imetolewa na:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dares Salaam
.

8 Mei, 2012

Je: NI SAHIHI KWA IKULU KUTOA WARAKA WA AINA HII?


Ni sahihi. Ila mbona CHANETA wamemuuzisha sura MAMA PINDA na mpaka sasa fedha zilizobaki hazijulikani ziko wapi...

Wajitahidi kumkamata mtuhumiwa sio kutuletea upuuzi wao.
 
For public consumption na kuweka mambo in proper perspective walivyofanya Ikulu ni sawa; BUT then kama wanadai ni jinai wamechukua hatua gani kwa mhusika au ni untouchable?
Vyombo vinavyohusika na kuchukua hatua vimeshajua pa kuanzia
 
Salma kikwete kiongozi wa kitaifa?! Hivi hawa magamba wataacha lini kutuchefua?!
 
ndio kazi ya Rweyeemamuu.....tusishangae huyu wa chekechea kesho utamsikia anakanusha la mwalimu wa primary mtondogoo uasikia la mwalimu wa Secondary....... yetu majicho..
 
Tiba sahihi ni kurudisha heshima ya ikulu ambayo imepotea katika kipindi karibia chote cha awamu ya nne. Tofauti na awamu zilizopita, tukio kama hili ni jambo la kawaida sana, na wahusika huonyesha kwa mbwembwe ruksa walizopata kupitia simu za viganjani. Kukemea au kutoa kauli kama hizi sio tiba, tiba ni kuwekeza katika kurudisha heshima ya ikulu kama taasisi.
 
Ndugu zangu ukiwa makini unatakiwa upuuze taarifa zote toka Ikulu manake ni mipasho juu ya mipasho.
Hivi ni Salva anayefanya huu upuuzi? au ni housegirl wa Ikulu anayetoa hizi taarifa?
Taarifa toka Ikulu kuhusu kuachiwa huru kwa wauaji wa Imran Kombe ilinifanya nikajitapikia!
Hawako makini hata kidogo, mipasho kila siku, bosi anatalii, nchi iko hoi, wao mipasho!
 
Ikulu.. Ikulu Against a single pipo.. Only a mere kids kinder-care owner.. Eehe.. !! Kesho mtakanusha yote ya Salma2015
 
Back
Top Bottom