THEUNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
[/TD]
[TD="width: 118, bgcolor: transparent"][/TD]
[TD="width: 284, bgcolor: transparent"]
PRESIDENTS OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku chachezilizopita, Mkurugenzi wa Shule ya Chekechea ya Moses Nursery ya Yombo Vituka,Dar es Salaam, Bwana Moses Kabambara amekuwa anasambaza kadi kwa watu binafsi,makampuni, mashirika na ofisi za ubalozi zilizoko nchini akisaka michango kwaajili ya ununuzi wa madawati na ujenzi wa madarasa na uzio wa shule yake.
Katika kadi yake yakuomba michango na kwenye taarifa anazozisambaza kwenye vyombo vya habari,Bwana Kabambara anatumia jina la Mheshimiwa Salma Kikwete, Mke wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nembo ya Taifa kuonyesha kuwa Mheshimiwa Mama Kikwete ndiye mchangishaji na Mgeni Rasmi kwenye matembezi ya shughuli yakuchangia maendeleo ya shule yake.Aidha, amekuwa anadai kuwa Mama Kikwete ndiye atakuwa Mgeni Rasmi kwenye shughuli hiyo.
Tunapenda kuchukua nafasi hii kuuarifu umma wa Tanzania kama ifuatavyo kuhusu suala hili:
(a) Kwamba Mama Salma Kikwete kamwe hajapata kuridhia kuwa Mgeni Rasmi katika matembelezi hayo
(b) Kwamba Mama Salma Kikwete hajapata kukubali kuwa mchagishaji ama hata mshiriki wa aina yoyote katika uchangishaji fedha kwa ajili ya shule hiyo.
(c) Kwamba Bwana Kabambara anaufanyia udanganyifu umma ili uweze kuamini kuwa Mama Salma Kikwete amekubali kushiriki katika shughuli za uchangiaji fedha shule yake.
Tunapenda kupitia taarifa hii kuutahadharisha umma kuwa macho na vitendo vya baadhi ya watu wanaotumia majina ya Viongozi wa Kitaifa kuchangisha ama kukusanya fedha ama hata kufanya mambo mengine yenye kulenga manufaa au maslahi binafsi. Hili ni kosa la jinaimbali na kwamba vitendo vya namna hii husababisha usumbufu kwa jamii na kwa viongozi husika.
Imetolewa na:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dares Salaam.
8 Mei, 2012
Je: NI SAHIHI KWA IKULU KUTOA WARAKA WA AINA HII?