Wanu Ameir: Halmashauri ziendelee kutenga fedha kuwalipa Walimu wa Kujitolea

Wanu Ameir: Halmashauri ziendelee kutenga fedha kuwalipa Walimu wa Kujitolea

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,280
Reaction score
3,946
Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Salma Kikwete, kuhusu mkakati wa serikali juu ya malipo kwa Walimu wanaojitolea ili walau waweze kukidhi mahitaji yao.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh, amesema kuwa, kwa mujibu wa ufafanuzi wa awali uliotolewa na Waziri Mkuu, Halmashauri ziendelee kutenga fedha kulingana na uwezo wao kuwalipa walimu wanaojitolea katika halmashauri husika, akiongeza kuwa hakuna kiwango maalum kilichowekwa ka ajili ya Malipo.


​
"Lakini katika swala hili nadhani Mheshimiwa Waziri Mkuu alishalitolea maelekezo kwamba halmashauri ziendelee kutenga fedha kwa ajili ya walimu wanaojitolea katika maeneo yao. Kwa hiyo, Mheshimiwa Spika, na mimi nasimama na msimamo wa Waziri Mkuu kwamba halmashauri ziendelee kutenga fedha.

Na alitoa maelekezo kwamba hakuna kiwango maalum ambacho kimekuwa fixed kwa ajili ya walimu hao, lakini halmashauri zilipe kwa mujibu wa uwezo wao kuona kwamba walimu wanaojitolea nao walau wanapata chochote."

Soma pia Walimu wa kujitolea Shule za Msingi, Sekondari - Morogoro waboreshewe maslahi, malipo hayaendani na hali halisi ya sasa
 
Aiseee hapa mafisi wamekabidhiwa bucha sasa hao waliku wa kujitolea wajiandae kupokea pesa ya nauli tu
 
Hivi Salma si alipaswa kujiendeleza kielimu angalau kutoa zaidi tongotongo za uelewa wa mambo, baada yake akaridhika na cheo cha u first ledi.
 
Aiseee hapa mafisi wamekabidhiwa bucha sasa hao waliku wa kujitolea wajiandae kupokea pesa ya nauli tu
Litaenda vizuri iwapo kutakuwa na mfumo mzuri wa ufuatiliaji, else ni mlango mwingine wa upigaji
 
Back
Top Bottom