Waraka toka Ikulu: Hebu tuujadili...

Waraka toka Ikulu: Hebu tuujadili...

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,506
THEUNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

[/TD]
[TD="width: 118, bgcolor: transparent"][/TD]
[TD="width: 284, bgcolor: transparent"]
PRESIDENT'S OFFICE,

THE STATE HOUSE,

P.O. BOX 9120,

DAR ES SALAAM.

Tanzania.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku chachezilizopita, Mkurugenzi wa Shule ya Chekechea ya Moses Nursery ya Yombo Vituka,Dar es Salaam, Bwana Moses Kabambara amekuwa anasambaza kadi kwa watu binafsi,makampuni, mashirika na ofisi za ubalozi zilizoko nchini akisaka michango kwaajili ya ununuzi wa madawati na ujenzi wa madarasa na uzio wa shule yake.

Katika kadi yake yakuomba michango na kwenye taarifa anazozisambaza kwenye vyombo vya habari,Bwana Kabambara anatumia jina la Mheshimiwa Salma Kikwete, Mke wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nembo ya Taifa kuonyesha kuwa Mheshimiwa Mama Kikwete ndiye mchangishaji na Mgeni Rasmi kwenye matembezi ya shughuli yakuchangia maendeleo ya shule yake.
Aidha, amekuwa anadai kuwa Mama Kikwete ndiye atakuwa Mgeni Rasmi kwenye shughuli hiyo.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kuuarifu umma wa Tanzania kama ifuatavyo kuhusu suala hili:
(a) Kwamba Mama Salma Kikwete kamwe hajapata kuridhia kuwa Mgeni Rasmi katika matembelezi hayo
(b) Kwamba Mama Salma Kikwete hajapata kukubali kuwa mchagishaji ama hata mshiriki wa aina yoyote katika uchangishaji fedha kwa ajili ya shule hiyo.
(c) Kwamba Bwana Kabambara anaufanyia udanganyifu umma ili uweze kuamini kuwa Mama Salma Kikwete amekubali kushiriki katika shughuli za uchangiaji fedha shule yake.

Tunapenda kupitia taarifa hii kuutahadharisha umma kuwa macho na vitendo vya baadhi ya watu wanaotumia majina ya Viongozi wa Kitaifa kuchangisha ama kukusanya fedha ama hata kufanya mambo mengine yenye kulenga manufaa au maslahi binafsi. Hili ni kosa la jinaimbali na kwamba vitendo vya namna hii husababisha usumbufu kwa jamii na kwa viongozi husika.

Imetolewa na:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dares Salaam
.

8 Mei, 2012

Je: NI SAHIHI KWA IKULU KUTOA WARAKA WA AINA HII?
 
huu sasa ni upuuzi; kama kweli walichoandika Ikulu ni cha kweli kutoa tamko ni kuthibitisha hofu yetu sisi wengine. Kuna watu hawana kazi isipokuwa kufikiria kila siku watoe tamko gani. Ina maana kweli hakuna mtu huko Ikulu ambaye angewashauri NINI hasa cha kufanya badala ya kutoa tamko?
 
Huyo anayeitwa Mama Salma ni nani pale magogoni Ikulu mpaka kurugenzi ya habari ikulu imtolee tamko? Hivi nikikabidhiwa ofisi ya umma nini mamlaka ya mke wangu kwenye hiyo ofisi? Taarifa inatahadharisha umma kuwa makini na watu wanaotumia vibaya majina ya viongozi wa kitaifa, well & good, je Mama Salma kikwete naye ni kiongozi wa kitaifa? Nini cheo chake ktk nchi hii?
Tanzania, unajengwa na wasiyo na kisomo kamwe huwezi endelea, wasomi wenye nafasi ya kukusogeza hatua mbele wanafikiri matumbo yao na ya familia zao tu, wasomi wenye uchungu nawe hawana nafasi ya kimaamuzi na kukukomboa!
 
Nionavyo mimi huyo mmiliki wa hiyo shule alishafanya mazungumzo na Salma na huenda alikuwa na tumaini la kukubaliwa. Sasa along the way hata kabla ya formal acceptance notification yeye akaanza kutembeza bakuli. Ikulu ndo imeishia hapo.....
 
Si sahihi...Hivi wake za viongozi nao ni viongozi wa umma? Mama Salma Kikwete si kiongozi wa kitaifa ila anaweza kuwa kiongozi wa familia yake na si vinginevyo.

Kama hii taarifa ni ya kweli basi kuna watu pale Ikulu hawana kazi za kufanya na pili Ikulu hiyo haina washauri kwa maana ya watendaji wanaojua nini cha kufanya. Kama kulikuwa na ulazima wa kutoa waraka huo basi ungetolewa kupitia asasi yake WAMA na si Ikulu!
 
Huyo anayeitwa Mama Salma ni nani pale magogoni Ikulu mpaka kurugenzi ya habari ikulu imtolee tamko? Hivi nikikabidhiwa ofisi ya umma nini mamlaka ya mke wangu kwenye hiyo ofisi? Taarifa inatahadharisha umma kuwa makini na watu wanaotumia vibaya majina ya viongozi wa kitaifa, well & good, je Mama Salma kikwete naye ni kiongozi wa kitaifa? Nini cheo chake ktk nchi hii?
Tanzania, unajengwa na wasiyo na kisomo kamwe huwezi endelea, wasomi wenye nafasi ya kukusogeza hatua mbele wanafikiri matumbo yao na ya familia zao tu, wasomi wenye uchungu nawe hawana nafasi ya kimaamuzi na kukukomboa!

1st lady!!!
 
hii kurugenzi ya habari ya ikulu haina tofauti na takukuru they dont know their right from their left!!
 
Viongozi wa kitaifa?
Mheshimiwa?
Mbona ni sawa huyo mama kumsaidia raia mwenzake?
Kama ingekuwa ni rais tungefanyaje?

Naamini ccm imefika mwisho.
 
huu sasa ni upuuzi; kama kweli walichoandika Ikulu ni cha kweli kutoa tamko ni kuthibitisha hofu yetu sisi wengine. Kuna watu hawana kazi isipokuwa kufikiria kila siku watoe tamko gani. Ina maana kweli hakuna mtu huko Ikulu ambaye angewashauri NINI hasa cha kufanya badala ya kutoa tamko?
Ebu imagine, Ikulu ya Marekani (White House) inatoa tamko lenye mwelekeo wa aina hiyo!!! Aibu gani hii jamani!!! Wanaacha kutoa matamko ya maana yanayohusu mambo mengi yenye utata yanayowagusa watanzania kwa ujumla wao, wanaandika upuuzi huu wa eti kukanusha kukubali mwaliko!! Nchi hhiiiii mmmhhhh ptuuuuu!!! Najisikia hata kichefuchefu.
 
Ina maana ikulu imeshidwa kwenda kumkamata mtu mmoja hadi watoe tamko? nina wasi wasi hii shule ni yao wanaipa promo...
 
Ina maana ikulu imeshidwa kwenda kumkamata mtu mmoja hadi watoe tamko? nina wasi wasi hii shule ni yao wanaipa promo...

Kumbe madikteta mpo wengi? kwani Ikulu kazi yake ni kukamata watu?
 
TAARIFA KUTOKA IKULU

Kumekuwepo na wimbi la vijana wasio waadilifu hasa kutoka jukwaa la MMU(JAMII FORUMS) wanaojinadi kumtokea na kukubaliwa mtoto wa mkuu mheshimiwa mwa#asha.tunapenda kuuarifu umma kuwa taarifa hizi si za kweli kwani mheshimiwa mwa#asha ni mdogo na anaendelea na masomo na kamwe hawezi kuwakubali warugaruga wa jf,kwanza wamezidi ujuaji sana.

IMETOLEWA NA WAZEE WA IT
MAGOGONI.
 
Tatizo la viongozi wetu wanapiga kelele watu wajiajiri,raia wanapojiajiri na kutaka msaada ili wajikwamue wanawakimbia na kuwapeleka ktk vyombo vya dola.sioni sababu ya ikulu kupinga jambo la kheri elimu kwa watoto
 
Back
Top Bottom