Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Mimi naungana na Mh Kingunge kupinga WARAKA huo wa wawakatoliki. Tunafahamu wazi kuwa waraka huo una baraka zote za Pengo, baraza la maaskofu, balozi wa Vatican na hatimaye Papa.

sasa kama hilo baraza lina hamu ya kufanya hao basi wavue majoho yao na kuingia kugombea uongozi wa kisiasa kama alivyofanya Dr Slaa.

HONGERA SANA KINGUNGE
 
Huyu Kingunge Ngombale Mwiru asitubababaishe na maneno yake ya kinafiki hapa. Mpagani huyu ndiye kwa unafiki ambaye alijifanya kuwa kaisahau katiba ya nchi ambayo haiongozwi na misingi ya dini bali kila mtu ana uhuru wa kamini na kuabudu dini aitakayo ili mradi asivunje sheria. Sasa iweje maswala ya OIC na mahakama ya kadhi yawe ya kitaifa??? Kama waislam wanataka hayo mambo waingie kama wao through BAKWATA na si kama nchi. Sijui ni kwa nini tunapenda kupindishapindisha mambo Tanzania only for the sake ya ku win kura za watu.

Ni mnafiki huyu huyu ambaye kwa unafiki mkubwa walishiriki katika azimio la Zanzibar la kupindisha Azimio la Arusha ili viongozi wajipatie utajiri kwa ufisadi, na matokeo yake tunayaona kwa kuzaliwa kwa matabaka Tz na tunakoelekea tutazidi yale matabaka yaliyoko India. Kama kuna mkuu hapa ambaye amesoma au ana ufahamu wa tamaduni wa India atakubaliana na mimi jinsi gani kule kuna matabaka. Kwa Tz itakuwa even worse, akina mzee matonya watakuwa na kundi lao, slums zitaongezeka, sijui nielezeje. Naumia kwa kuwa tumekubali kuibadili Tz na kila kitu. Sikatai Mtanzania kuwa na mali au utajiri ila utajiri huo chanzo chake ni nini??? Hebu fikiria matajiri kama Chenge, Idrisa Rashidi, Rostam, Somaias, Patels, Manjis, Mrambas, Yonas, Mkapas, Kingunges (kupitia hasa tender za manispaa za DSM na shares), Chandes, Nonis, Balalis, Lukazas, Njakes, Makubos, .....nth. The list is endless.

Wewe Kingunge ambaye ulistahili kupumzika, unaenda Bungeni na vikao vya Chama kusinzia na kusubiri mgawo wa sitting je umechangia kuipotezea Tanzania mwelekeo kiasi gani??? Hebu niambie tender unazopewa na manispaa zote tatu za DSM kwa kazi zile za kisaniii za Stand ya Ubungo, Uzoaji taka, n.k je unailipa serikali vilivyo au unatoa chochote ili pate tender zile ili hali wanafahamu pia wewe si mtendaji mzuri?? Ulizika Azimio la Arusha ili mkumbatie Rushwa vilivyo halafu leo mnafanaya usanii eti mna Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, wakati mliiibariki Rushwa?? You are not serious man. Acha wakristo waamke wawape dosi ya electric shot ili muweze kuamka huo usingizi fofo mliolala. Ndiyo maana umeamua kukurupuka kuanza kupigia magoti Wakatoliki na huku ukihofia pengine other denominations may do the same. Yes, they may as they are fed up with your longolongos, ufisadi, rushwa kwa haki au stahili za wazalendo, uonevu kwa wananchi kuchukua ardhi zao kwa nguvu bila fidia za maana, yaani watanzania wanakuwa homeless and refugees in their own country. You are not serious man.

Mzee wetu Kingunge, tafadhali pumzika, sijaona mchango wowote wa maana kwa nchi hii kwa lengo la kumtetea mzalendo, ulichofanya ni kushiriki kwa asilimia 100 kuleta Azimio la Zanzibar la kuleta matabaka ya kisiasa na matajiri. Ni nyie ambao mtaisababisha Tz imwage damu siku zijazo. Fahamuni kuwa kila ovu lina mwisho wake na kila uonevu ni lazima ufike mwisho, msitake wazalendo waingie msituni, msitake hapa pawe kwa Savimbi, msitake hapa pawe kwa Makaburu, msitake hapa..... sina la kusema zaidi. Wakati huo mtatukimbia na mtaenda uhamishoni kwenye majumba mlionunua nje na vitega uchumi, mtaacha ndugu akimkata mwezake kichwa, mtatujeuza mauaji ya kimbari. Kingunge omba msamaha watanzania kwa niaba ya wote mlioshiriki kutufikisha hapa tulipo na mkiahidi kuwa mtaleta tena Azimio lingine ambalo litotoa ufumbuzi wa matabaka yaliyopo kwa sasa.

Aluta continua JF kwa kutupa nafasi ya kutoa hisia zetu hapa. Wazalendo watasoma bila ubishi. Mafisadi, vibaraka wa mafisadi, watoto wa mafisadi, ndugu wa mafisadi, wala rushwa watataka wanipige mawe au wanijibu kuwa nimeandika utopian, ni sawa una uhuru wa kuona utakavyo ila nimesema.
 
Thanks Mkuu, pia sikumbuki kuona sehemu yoyote ya waraka ikisema chagua mkatoliki, nilichoona ni sifa za kiongozi bora!!! sasa kama huyo mtu hupo dini yoyote au hata kama hana kini kama yeye KINGUNGU, basi ndio huyo huyo

afterall sio lazima kutekeleza waraka kwani mwanajumuiya halazimiki!!! inawachoma sana wale wasio safi...

Ningependa kusikia pia waraka wa dini na madhehebu mengine ili viongozi wachafu wawekwe kando
Tuweni wakweli kuliko kung'ang'ania dini kuzifanya ndio utawala. Wale wenye majukumu ya kuongoza jamii katika namna nyingine tofauti na siasa wafanye majukum yao kwa mtindo huo na sio kisiasa. Vipi viongozi wa kisiasa wakianza kusema Padri au sheikh fulani hafai kwa sababu anatumia misamaha ya kodi vibaya au sababu nyinginezo, waumini simtaona mmehukumiwa. nadhani siasa si mahali pake otherwise machafuko yale pale hayapo mbali nasi tujiandae tu.
 
Msiandikie mate na wino upo. Mbona waraka huo upo hapa JF siku nyingi tu?

5161d1246544359-kanisa-katoliki-laandaa-waumini-uchaguzi-2010-ilani_kanisa.jpg


Angalia hapa kupata attachments zote

Mkuu, umefanya kazi takatifu. Ilikuwa kidogo na mimi niutume tena hapa JF.

Waraka huu unapaswa kutunzwa hala tuanze kuujadili na kuusambaza utakapokaribia uchaguzi! Tena hakuna haja ya kuomba copyright maana nasikia wakatoliki wamekubali uchapishwe na usambazwe na yeyote anayeweza kuusambaza. Ukizani nabisha piga simu kwa walioundaa yaani Chama Cha Wanataaluma Wakatoliki na namba yao hii hapa (022-2127675)
 
Lazima Kingunge aogope naweza kusema that man is a big hypocrite aliyewahi kutokea Tanzania.

Enzi za mwalimu aliiishi kinafiki sana na immidiately baada ya mwalimu kuondoka kamekuwa kafisadi kwelikweli na kanabebwa kwenye mbeleko ya mafisadi.
Mwalimu walimwogopa kumbe hawakumheshimuuu....ndo chanzo cha unafiki wao viongozi waaandamizi wa CCM na serikali mpaka leo...

muda wao kuumbukaa umewadiaaaa.....

mwongozoo huu nimeusomaa hauna chembe ya udini hata kidogo zaidi ya ukweli mtupu..

U shall know the truth and the truth shall set u free...
 
Mmmmmhhhhhh. Hivi ni yule Kingunge mpagani?
Sasa wakatoliki wapi na wapi na yeye?
Wao wametoa waraka kwa followers wao na yeye atoe wa kwake kwa ajili ya pagans kama yeye. asilalame bure.

Hana lolote huyu Mzee keshachoka kisiasa,hapa anapiga kelele kwa kuwa anajua watanzania wengi wakielimika watachagua viongozi bora.Ufisadi na utapanyaji wa mali za Tanzania kwa sasa ni kwa sababu ya ukosefu wa uongozi bora.

Hilo Mzee Kingunge analielewa fika kwamba waraka huu ukisambaa vijijini wabunge wengi wa sasa hawatarudi bungeni.Inawezekana hata Rais aliyemchagua akashindwa kurudi ofisini.Sasa hali ikiwa ni hiyo nani atakayelinda maslahi yao.Hofu imewaingia mioyoni mwao na kwa hali ilivyo mafisadi ndio wenye hofu zaidi na sasa wanatapa tapa.

Mzee Kingunge wewe na familia yako na marafiki zako mmeshakula vya kutosha rasilimali za Tanzania.Waacheni wananchi wanyonge wa Tanzania nao wafaidi matunda ya uhuru,hofu ya nini, hii yote ni kwa sababu ya masililahi tu na hakuna kingine.
 
Hana lolote huyu Mzee keshachoka kisiasa,hapa anapiga kelele kwa kuwa anajua watanzania wengi wakielimika watachagua viongozi bora.Ufisadi na utapanyaji wa mali za Tanzania kwa sasa ni kwa sababu ya ukosefu wa uongozi bora.

Hilo Mzee Kingunge analielewa fika kwamba waraka huu ukisambaa vijijini wabunge wengi wa sasa hawatarudi bungeni.Inawezekana hata Rais aliyemchagua akashindwa kurudi ofisini.Sasa hali ikiwa ni hiyo nani atakayelinda maslahi yao.Hofu imewaingia mioyoni mwao na kwa hali ilivyo mafisadi ndio wenye hofu zaidi na sasa wanatapa tapa.

Mzee Kingunge wewe na familia yako na marafiki zako mmeshakula vya kutosha rasilimali za Tanzania.Waacheni wananchi wanyonge wa Tanzania nao wafaidi matunda ya uhuru,hofu ya nini, hii yote ni kwa sababu ya masililahi tu na hakuna kingine.
Tunawasakama wanasiasa bura nani kasema hawa viongozi wa dini si mafisadi? Harambee zote makanisani nani huzifanya? Taifa linapoteza asilimia 30% ya mapato yake kwenye misamaha, ni nani anaiba kama si hawa viongozi? Waache ufisadi kwanza ndio waweze kuwanyooshea vidole wengine. Wajitenge na siasa vingenevyo na wao wataumbuka kwa madudu wanayoyafanya
 
Hivi huo waraka kuna mtu anao nasi tuusome kabla hatuja changia? Kama waraka ulisha wekwa hapa naombeni link. Maana kwa ninavyo jua kuna watu humu wataanza kuchangia kwa hisia au kufuata mkumbo bila kujua kwanza nini kilicho semwa dani ya waraka huo. Je waraka unaelezea vigezo vya kiongozi bora? Au unatoa maagizo kuchagua watu wa kundi fulani? Maana isije ikawa inasema msichague mafisadi hapo lazima tutajua "mafisadi" nao wanaona "wanatengwa".[/B]


Hilo ndilo tunalolitaka mkuu, mafisadi watengwe kabisa mbali na jamii ili mbegu ya ufisadi isizidi kuenea miongoni mwa wanajamii.
 
Njia moja ya kuusambaza vitabu hivi vilivyotolewa na kanisa katoliki ni kutumia message za simu. Kila siku tuma kipengele kimoja cha waraka kwa jamaa zako kumi. Na yeye mueleze atume kwa watu kumi. Baada ya mwezi kila mmoja atakuwa ameshsoma kitabu kizima. Ndipo hapo joto ya jiwe itawashukia wanafiki kabla ya uchaguzi. Maana kwa njia hiyo hata aliye kijijini atausoma maadam ana simu.
 
Hilo ndilo tunalolitaka mkuu, mafisadi watengwe kabisa mbali na jamii ili mbegu ya ufisadi isizidi kuenea miongoni mwa wanajamii.
Hili ndilo analohofia Kingunge na makuwadi wa ufisadi.Huu waraka ni tishio kwa mafisadi na wanasiasa type ya Chitalilo na Serukamba!
 
Si ndo Kingunge huyu huyu anayehusishwa na kuingiza mahakama ya kadhi na OIC kwenye election manifesto ya CCM? Kuna watu wameshasema kuwa Kingunge na Mangula ndo waliingiza mambo haya kwenye manifesto ya CCM.

Ikiwa hayo ni kweli basi hatupaswi kushangaa yeye kupinga wakatoliki kwani huo msimamo ambao yeye anao, wakatoliki wanaupinga. Lakini inapaswa ajue kuwa kwa kuingiza kadhi na OIC ndani ya manifesto ya CCM aliingiza mambo ya dini ndani ya CCM.

Hapaswi kushangaa vile vile ikiwa dini zinaanza kuamka. Ameshakula nyama ya mtu!!
Ni huyuhuyu aliingiza vitu hivyo na asilaumu kwa kutumia propoganda zake za Urusi.Mtu huyu mkumbuke ndiye alikuwa anamfitinisha Mwl Nyerere na akina Malecela,Kolimba na wengineo.Alijaribu kumfitinisha Prof.Mwandosya na Kikwete,matokeo yake ulaghai wake uling'amuliwa na Mh.Rais na kuishia kutemwa.
 
Mimi pia nimeona kwenye muhtasari wake kwenye magazeti, mbona huo waraka hauna neno???...unasisitiza usawa kwa watanzania wote na kutokuchagua viongozi wabovu kama hawa tulionao.

Kingunge lazima aumie kwa sababu alishiriki kutu chagulia kiongozi mkuu mbovu, na pia yeye ni mbovu mwenye ufisadi tele ukiwamo wa mradi wa ubungo bus stand na kumuendekeza mwanae (Kinjekitile) hadi kufikia hatua ya kuua watu ovyo akijua baba yake anamlinda. (Rejea kesi yake ya kuua mtu kwa kumgonga na gari makusudi, then akashinda kesi kimizengwe.)

To quote his own words "LIKE FATHER LIKE SON "
AND WORSE STILL IS HIS USE OF MWALIMU NAME IN HIS SENILE OBSERVATIONS. A REALLY DANGEROUS ATHEIST/POLITICIAN WHO HAS OUTLIVED HIS USEFULNESS TO SOCIETY.
 
Waraka huu wa CPT unataka kuwa kama BIBLIA/QURAN. unawachanganya na utaendelea kuwachanganya wengi hata ambao nilidhani unawasemea wao pia.
 
Waraka huu wa CPT unataka kuwa kama BIBLIA/QURAN. unawachanganya na utaendelea kuwachanganya wengi hata ambao nilidhani unawasemea wao pia.
Kamwe siwaungi mkono viongozi wa dini mpaka na wenyewe watoke na wajisafishe kwenye tuhuma za kutumia vibaya misaha. Hivi hiyo 30% ni kiasi. Mpaka kieleweke wanasiasa na hawa viongozi wa dini kila mtu awajibike. wakati tunatuma msg za kuwasakama wanasiasa tusisahau meseji za keuelezea misamaha inavyofujwa. Lazima tuseme wananchi watambue kila mtu ni mwizi tu hapo
 
Wakuu msisahau kwamba huyu mzee ni Mbunge wa kuteuliwa tuu. Hana lolote zaidi ya ufisadi wake. Hawezi kubadilisha lolote maana yeye is time barred. Hata angepiga debe kiasi gani haliwezi kumsafisha ufisadi anaotufanyia Watz. RIP
 
Wakuu msisahau kwamba huyu mzee ni Mbunge wa kuteuliwa tuu. Hana lolote zaidi ya ufisadi wake. Hawezi kubadilisha lolote maana yeye is time barred. Hata angepiga debe kiasi gani haliwezi kumsafisha ufisadi anaotufanyia Watz. Hana usahuri maana akili imeshachoka mbaya. Akalale
 
Wakuu msisahau kwamba huyu mzee ni Mbunge wa kuteuliwa tuu. Hana lolote zaidi ya ufisadi wake. Hawezi kubadilisha lolote maana yeye is time barred. Hata angepiga debe kiasi gani haliwezi kumsafisha ufisadi anaotufanyia Watz. Hana usahuri maana akili imeshachoka mbaya. Akalale
No way tujenge hoja hakuna haja ya kumshambulia huyu mzee. Mara fisadi oh whasever. alichokisema kina mantiki? Nini mustakbali wamchezo huu maana kameibuka kamtindo kaviongozi wa dini kuvutana na serikali bila sababu.
Hawa viongozi nao wasafi? Wanasemaje juu ya misamaha? Ule si ufisadi? Wameainisha hayo katika waraka kwa wananchi? Wameandika lolote juu ya kujinasua kwenye aibu ya misahama? Wametoka hadharani na kutoa ufafanuzi kwa umma au wamelalamika wakaja na vitisho? Nani anawawajibisha wao kwa ufisadi wao? Tunataka na tungependa kuona 30% wanayotuibia inakoma
 
No way tujenge hoja hakuna haja ya kumshambulia huyu mzee. Mara fisadi oh whasever. alichokisema kina mantiki? Nini mustakbali wamchezo huu maana kameibuka kamtindo kaviongozi wa dini kuvutana na serikali bila sababu.
Hawa viongozi nao wasafi? Wanasemaje juu ya misamaha? Ule si ufisadi? Wameainisha hayo katika waraka kwa wananchi? Wameandika lolote juu ya kujinasua kwenye aibu ya misahama? Wametoka hadharani na kutoa ufafanuzi kwa umma au wamelalamika wakaja na vitisho? Nani anawawajibisha wao kwa ufisadi wao? Tunataka na tungependa kuona 30% wanayotuibia inakoma
Na wewe usingewashambulia MAASKOFU. Ungeshambulia kilichoandikwa mle. Na wala sio Maaskofu waliouandaa waraka ule. Ni CPT na wadau wao.
 
Na wewe usingewashambulia MAASKOFU. Ungeshambulia kilichoandikwa mle. Na wala sio Maaskofu waliouandaa waraka ule. Ni CPT na wadau wao.
Wanasema waliupitia na wakaridhia uende kwa jamii. Note: Post zangu zoote nawataja viongozi wa dini na si maaskofu
 
Viongozi wa Kanisa Katoliki ni wasomi wazuri sana. Kingunge naye ni msomi mzuri pamoja na Upagani wake. Naamini ameuelewa fika waraka huo wa Kanisa Katoliki, ila anachofanya ni kupotosha makusudi ionekane kwamba hawa wanaingiza udini kwenye suala la uchaguzi. Kinachowakera viongozi wa kanisa ni kuona wanasiasa wasio waadilifu wakihaha kuingia madarakani kwa njia ya rushwa. Hawa ni wanasiasa ambao wakishaingia madarakani huwa hawana agenda yoyote ya kuleta maendeleo kwa wananchi bali kujilimbikizia mali kwa njia za kifisadi na kutetea mfumo wa kifisadi ili waendelee kuwanyonya wananchi. Baada ya kufunuliwa, viongozi wa kanisa sasa wameona ni vema wasaidie kutoa elimu ya uraia kwa waumini wao kuwatahadharisha kuhusu fisi hawa. Kuna ubaya gani katika hili? Udini uko wapi hapo? Come on Mpagani Kingunge!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom