Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,672
- 2,697
Kama ilivyo ada, kila wakati katika kila nchi kuna ajenda ama sakata linalolindima, linaweza kuwa la kisiasa, kijamii ama kiuchumi. Ikiwa sehemu ya nchi zenye Siasa za mlengo wa Kidemokrasia, Tanzania imeingia katika mjadala mkali kati ya Serikali, wadau wa uwekezaji, vyama vya upinzani, asasi na taasisi mbali mbali.
Mjadala huu unahusisha uwekezaji bandarini, Uwekezaji unaotarajiwa kufanywa na kampuni ya kimataifa ya DP-World kutoka nchini Saudia. Kuzuka kwa mjadala mkali kati ya Serikali, taaisisi na Wadau kumetokana na baadhi ya vipengele ambavyo vinaonekana kutoleta tija au maslahi kwa Taifa.
Lakini, hivi karibuni, kumeibuka na hisia mbali mbali baada ya Sakata hili kujadiliwa na Taasisi za kidini, hasa, baada ya Waraka wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), Waraka ulioonyesha msimamo wa Baraza hilo ambao unakinzana na ule wa Serikali, wa kuruhusu uwekezaji wa kampuni ya DP-World kama ulivyoainishwa katika vipengele vya Mkataba huo (IGA)
Kati ya maswali yaliyogonga vichwa vya watu, ni wapi basi, Kanisa hili kongwe linapata Mamlaka ya kutangaza misimamo yake hadharani juu ya masuala ya Kisiasa licha ya kuwa Taasisi ya kidini.
HIZI NI SABABU KUU TATU ZINAZOIPA TAASISI HII USHAWISHI KWA SERIKALI YA TANZANIA.
Kwa kumalizia, ndugu zangu mnaodhani Kanisa hili linatawala nchi eleweni halitawali kwa Mamlaka yake kikanisa, bali kwa ushawishi wake kama Taasisi kongwe, anayetawala nchi hii ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Raia.
Ahsanteni.
Mwl. Diwani.
Rejea makala hii kutoka Vatican News - Mchango wa Kanisa Katoliki Nchini Tanzania! Elimu, Afya na Ustawi wa Jamii

- Mtaji watu: Historia inaonyesha, tangu kabla ya uhuru, Kanisa Katoliki nchini Tanzania, limekuwa na idadi kubwa ya waumini, ambao kimsingi ndio mtaji mkubwa wa ushawishi na nguvu ya kanisa hili kufikia 32% ya waumini mpaka 2022. Kama ujuavyo, Siasa inagusa maisha ya watu, lakini, mamlaka juu ya maisha ya watu hayaishii kwa Wanasiasa pekee. Zipo taasisi nyingine zenye nguvu juu ya maisha ya watu, nazo ni Taasisi za kidini, asasi za kiraia pamoja na mashirika. Yote haya yanagawana nguvu na Wanasiasa, lakini kwa upande wa Kanisa Katoliki, ushawishi wake ni mkubwa. Hivyo basi, si Kanisa linalohitaji Serikali ili liwe na nguvu, bali, ni Serikali kupitia Wanasiasa wake linahitaji Kanisa ili kuongeza na Kudumisha ushawishi na nguvu kwa watu linao waongoza.
- Mchango wa Kanisa Kanisa Katoliki katika maendeleo tangu uhuru: Kazi mojawapo kuu ya Serikali ni kutoa huduma za Kijamii, kama Elimu kupitia ujenzi wa Shule, Miundombinu na Afya kupitia ujezi wa Hospitali. Kihistoria, elimu tuliyoanza kuipata hata punde baada ya Uhuru ilikuwa ni elimu yenye chembe za Kikoloni. Lakini, mpaka inafika wakati wa Utekelezaji wa Sera za Kijamaa miaka 1967-80 Shule zilizokuwa zikimilikiwa na Kanisa Katoliki zilikuwa ni Mara tatu ya zile zilizojengwa na Serikali. Kwa kutoa fursa sawa, bila kuzingatia misingi au tamaduni za Kidini, Serikali iliamua kuzitaifisha zote, hivyo, Kanisa likapoteza Shule nyingi na Hospitali ili kutengeneza usawa. Wingi wa shule hizi, ulitokana na Uambatanishaji wa huduma za Kijamii kama Afya na Elimu uliokuwa unafanywa na Wamisionari, wa Katoliki. Jambo ambalo lilivutia watu wengi hususan wa eneo la bara kuishi karibu na maeneo hayo. Mbali na hilo, hata leo 2023 Kanisa hilo Limeendelea kuwa na umiliki wa Taasisi kama Shule, Vyuo na Hospitali nyingi zaidi nchini.
- Kanisa Katoliki, limelea na kukuza viongozi wengi wa Kisiasa, Kijeshi na Kijamii: Kuanzia awamu ya Kwanza mpaka awamu ya tano, Maraisi wote katika mfululizo wa maisha yao hawakuwahi kuepuka kabisa malezi ya Kanisa hili. Si tu Marais, bali hata viongozi wa ngazi za juu za Jeshi, wamelelewa na wengineo kama aliyekuwa Mkuu wa Majeshi aliyemaliza muda wake, Gen. Venance Salavatory Mabeyo. Kuna Wanasiasa wengi leo hii ambao wamelelewa na kanisa hili na kukuzwa katika malezi ya kirho, nidhamu na hata kufunzwa uongozi kupitia kanisa hili.