Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Lazima tufike mahali kwa kuwaunga mkono Kanisa Katoliki maana hakuna haja ya kuongopa maana kuna ulazima kuwa na makanisa yote na kutoa elimu yao na pia kama makanisa yakikubaliana na kutunga Ilani moja na pande zote
 
Na najua ana wasi wasi sababu waraka huu utamgusa. Tusubiri ripoti ya CAG muone itakavyomuumbua. Mtu ukiwa safi waraka kama huu haukusumbui
 
Nakushukuru Shangazi kwa mchango wako Mzee Kingunge hana ubavu wa kuisafisha CCM,yeye mwenyewe alishachafuka siku nyingi na anakalia uchafu atapata wapi guts za kusafisha wenzake.

Radical changes zinahitajika ili kuleta mageuzi ya kisiasa na kiuchumi sasa hivi Tanzania na kwa kuanzia waraka huu utawaelimisha wengi kwa kanisa husika kutumia vigango vyake kutoa elimu.Wanao pinga lao ni moja wamefaidika na ufisadi kwa namna moja au nyingine.
 
Jaman Watanzania sasa tumesoma wote tunaweza kuelewa kizuri na kibaya.
Mzee kingunge keshaona jinsi mambo yatakavyokuwa kwa CCM mwakani,kama inaonekana Wakatoliki wamekosea SHERIA si zipoo wazifuate.
Mimi ninaona anachotaka kufanya nijisi ya kuonekana kuwa na yeye amechangia hoja tu kwanini asiseme kwenye hayo magazeti yanayoandika uongo? mengi ya hayo magazeti yakiwa ya SERIKALI?
Sisi watanzania tupo tiari kuchambua baya na zuri kwa manufaa yetu sote si kwa manufaa ya Chama au Mtu Binafsi
 
Shangazi ningekuwa karibu ningekushika mkono utaona mtu mzima akiumbuka.
 
Mwambie kabisa Mzee. Hapa ni waraka wa kuelekea 2010 na si misamaha ya kodi. Na kila mtu aelewe kuwa misamaha ya kodi ni kwa kila dhehebu, wakristo kwa makundi yao na Waislam kwa makundi yao. Na pengine tunaona wivu na misamaha ya kodi kwa Wakristo kwa kuwa wanaji-commit full kwa huduma za kijamii na ziko effective, tizama hospital zao, shule za Seminary na sasa za Secondary za kawaida, Vyuo vyao, etc. Yaani wana mipango mizuri sana. Na leo wakristo wakiamua hakuna huduma za jamii hiyo mikoa ya pembezoni wazalendo wetu watakufa, hebu ona machache kama Peramiho Hospital, Karatu Lutheran Hospital, Dareda Hospital, you name all. Je serikali huko nilikotaja na kwingineko kuna huduma za afya au ni zile dispensary ambazo hazina workforce na vitendea kazi??

Please, Wakristo wana haki ya kuilaani serikali hii kwa maana mchango wao ni wa dhati na unaonekana wazi. They have heart for the heart!!! Bisha.
Kingunge kasema ukweli kwa sababu hana cha kupoteza kwenye hizi dini. Nadhani tumezikumbatia mno. Tumegeuzwa mabubusa hatuna tena uwezo wa kuhoji. Tunaogopa. No way. Siangalii waje waislam na mambo yao au wakristo provided wanakuwa bias then lazima nitasema tu. Hayo maendeleo katika hospitali na shule ni sehem ndogo a misamaha nyingi watu wanaingia nazo mitini. Haiwezekani lazima tujue tunaenda wapi. UFISADI si kwa wanasiasa kila mtu anayetumia njia ya aina yoyote kukwamishwa maendeleo ya nchi tutapambana naye. Unaambiwa kuna kituo kinahudumia watoto 50 kina magari 13. Nini hii kama si upuuzi???? Haiwezekani ni lazima tuhakikishe mafisadi wa aina yoyote wanadhibitiwa. Kubwa misamaha ihusu maendeleo ya jamii na si matumbo ya wachache
 
Pia kinachomtisha xaidi ni kwamba waislam nao wanataka kupitisha kampeni against CCM. Sasa waislamu no, wakatoliki ambao ni zaidi ya nusu ya wakristo wote nchini wakasema no, hatujui kundi gani tena litajitokeza, CHADEMA nao wanakuja juu, CCM nao hawaelewani. Wana JF HAMUONI ccm lazima wachanganyikiwe?
 
Ukweli ni kuwaaa CCM sasa bila mabavu hawawezi Sisi tumeshuhudia wenyewe eti kura 862 zimewaangusha CHADEMA hili la wap? ni uongo mtupu
Watakoma 2010 shangazi
 
Mnao taka mabadiliko wangapi mmejiandikisha kupiga kura?
 
Pia kinachomtisha xaidi ni kwamba waislam nao wanataka kupitisha kampeni against CCM. Sasa waislamu no, wakatoliki ambao ni zaidi ya nusu ya wakristo wote nchini wakasema no, hatujui kundi gani tena litajitokeza, CHADEMA nao wanakuja juu, CCM nao hawaelewani. Wana JF HAMUONI ccm lazima wachanganyikiwe?
Lakini jamani hawa viongozi si ndio walituchagulia kiongozi toka kwa Mungu? Mbona leo wanamgeuka Mungu wao? Mie naona viongozi wa dini wanatapatapa tu huku nao (baadhi) wakisubiri wapewe bahasha zao. Si ndio hawa waliopokea na bado wanachukua michango ya mafisadi? Si ndiyo hao mara wanawakingia vifua mafisadi leo WARAKA? No way siwaamini. Naamini njia ya mageuzi iundwe na wananchi wenyewe hakuna watu wakuwaletea njia mbadala. hawa ndio waliowalea na kuwakuza wengi katika mafisadi. Leo wanatuhadaa. Haiwezekani ni moto kwao wote. wakati fulani najiuliza hivi nyumba za ibada tuingiazo hzina tofali za EPA. If yes tunamuomba Mungu kwa mlango pi?
 
Kingunge kasema ukweli kwa sababu hana cha kupoteza kwenye hizi dini. Nadhani tumezikumbatia mno. Tumegeuzwa mabubusa hatuna tena uwezo wa kuhoji. Tunaogopa. No way. Siangalii waje waislam na mambo yao au wakristo provided wanakuwa bias then lazima nitasema tu. Hayo maendeleo katika hospitali na shule ni sehem ndogo a misamaha nyingi watu wanaingia nazo mitini. Haiwezekani lazima tujue tunaenda wapi. UFISADI si kwa wanasiasa kila mtu anayetumia njia ya aina yoyote kukwamishwa maendeleo ya nchi tutapambana naye. Unaambiwa kuna kituo kinahudumia watoto 50 kina magari 13. Nini hii kama si upuuzi???? Haiwezekani ni lazima tuhakikishe mafisadi wa aina yoyote wanadhibitiwa. Kubwa misamaha ihusu maendeleo ya jamii na si matumbo ya wachache


Ndugu yangu tusiuchukulie ule msemo kuwa samaki mmoja akioza na wengine wote wameoza. La hasha ondoa yule aliyeoza na chukua hatua ya kumteketeza, ndivyo hivyo kama kuna waliodanyanganya kodi basi wachukulie hatua za kisheria. Any way, tusiende tofauti na mada hii. Tujikite kwa waraka wa kuelekea 2010, Kingunge in this kwa kuwa amelisemea na hatima ya Tanzania. Asante.
 
Kingunge nyamaza, hakuna mantiki kwa kila unachosema. Kwanza niwaunge mkono wote mnaoukubali waraka huu makini wa kanisa katoliki, kama serikali haitaki kuelimisha watu namna nzuri ya kupata viongozi safi kwanini kanisa lisitoe elimu hiyo adimu na ya lazima kwa wananchi wote. Halafu hajui kuwa katika inatoa uhuru wa watu kupata habari!

Kingunge alikuwa kimya wakati CCM inaingiza udini kwenye ilani ya chama na yeye akiwa mmoja ya watu waliyo tunga ilani ya CCM ambayo iliahidi kuwapa waislamu mahakama ya kadhi huku akijua ni ukiukwaji wa katiba! Sasa leo anashutumu kanisa katoliki linalotaka kuelimisha wauumini wake wasichague mafisadi! Aache kelele asubiri hukumu yake na mafisadi wenzake!

Mimi ni si muumini wa katoliki lakini naaunga mkono waraka huu, na nimeshapata mialiko kadhaa ya kwenye makanisa ya katoliki vijiji kuufundisha huu waraka na nitaenda! Mafisadi wajiandae kuanguka kwa kishindo!
 
Kingunge nyamaza, hakuna mantiki kwa kila unachosema. Kwanza niwaunge mkono wote mnaoukubali waraka huu makini wa kanisa katoliki, kama serikali haitaki kuelimisha watu namna nzuri ya kupata viongozi safi kwanini kanisa lisitoe elimu hiyo adimu na ya lazima kwa wananchi wote. Halafu hajui kuwa katika inatoa uhuru wa watu kupata habari!

Kingunge alikuwa kimya wakati CCM inaingiza udini kwenye ilani ya chama na yeye akiwa mmoja ya watu waliyo tunga ilani ya CCM ambayo iliahidi kuwapa waislamu mahakama ya kadhi huku akijua ni ukiukwaji wa katiba! Sasa leo anashutumu kanisa katoliki linalotaka kuelimisha wauumini wake wasichague mafisadi! Aache kelele asubiri hukumu yake na mafisadi wenzake!

Mimi ni si muumini wa katoliki lakini naaunga mkono waraka huu, na nimeshapata mialiko kadhaa ya kwenye makanisa ya katoliki vijiji kuufundisha huu waraka na nitaenda! Mafisadi wajiandae kuanguka kwa kishindo!
NAkutakia kila la kheri ningependa kushiriki pia lakini mpaka na wao watoe ufafanuzi juu ya tuhuma za kufisadi rasilimali za nchi. Na tunawasubiri kwa hamu njooni kutufundisha na tutawauliza. Andaeni majibu ya kueleweka
 
Mwaka 2007 alipinga vikali List ya Shame ya CHADEMA. akaja na kupinga kuwa CCM haina Mafisadi leo wote wamefikishwa mahakamani na hakuna jipya hivyo hakuna haja, then yeye hana Dini kinamuuma nini Sasa
 
Mnao taka mabadiliko wangapi mmejiandikisha kupiga kura?


Kingunge anasema Nyerere alileta umoja na udugu kwani siku hizi hawa voingozi wa sasa wameulinda huo umoja na udugu?


Sasa hivi kuna kundi la walionacho na wasio nacho. Wanajiona kuwa wao ndi wamiliki wa tz na wana haki ya kuongoz nchi hii siku zote hadi mauti kama yeye na ambao wakitaka kuingiz katika siasa lazima waulizwa to which group you belong kama wewe ni mpinzani au ccm na kama ni ccm ni wa kambi ipi!
haya yote yameletwa na weak, greedy iresponsible readers kama watawala wangekuwa makini yote haya yasingejitokeza.

wito ni kuwa tunaye OBAMA supporting democracy and hating thief leaders and supporting the clean yaoung but not serambas, hivyo watu jitokezeni muwatonwe nyoka huko kwenye madaraka. Wakati ni huu those who are conscious wakati ni huu, otherwise the country will be drugged 20 years back in the period 2010-2015 I tell you watmess up sana!
 
Oh yes,tuko njia panda.Kwani wanacho ogopa hawa wana siasa hasa ni nini.Binafsi sioni kama Kanisa limefanya jambo baya.Infact kama serikali ingekuwa na nia njema na wanachi wake,Kanisa lingepaswa kusaidiwa katika kutekeleza jukumu hili la msingi sana katika jamii.Kinyume chake sasa linakuwa ridiculed.Ajabu sana.Hivi Kingunge anadhani madhehebu mengine yana vigezo tofauti vya kiongozi bora,loo amechelewa sana.

Nadhani hawa jamaa wanacho ogopa ni hii civic education ambayo hili kanisa linatoa.Wanaogopa kwamba kama wananchi wataamka wataingizwa mkenge.Lakini lolote liwalo, siku inakuja ambapo wananchi wataamka kisawasawa,na CCM itatemwa.


MBUNGE wa kuteuliwa na mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru ameushambulia waraka wa kichungaji uliotolewa na Kanisa Katoliki nchini, unaoelekeza namna ya kupata kiongozi anayefaa kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu ujao adai kuwa utaligawa Taifa.

Kingunge alitoa kauli hiyo alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, ambayo iliwasilishwa na George Mkuchika bungeni mjini Dodoma jana.

Hata hivyo, Kanisa Katoliki kupitia Baraza lake la Maaskofu (TEC), limekuwa na utamaduni wa kutoa mwongozo kama huo wakati Taifa linapoelekea Uchaguzi Mkuu, huku kumbukumbu zikionyesha kuwa pia lilifanya hivyo mwaka 2005.

Katika kikao hicho cha jana kilichokuwa chini ya Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama aliyekuwa mwenyekiti, Kingunge alizungumza kwa msistizo huku akiwataka wabunge wamsikilize kwa makini na kutahadharisha kwamba asinukuliwe vibaya.

``Na sasa nimalize, nina jambo moja kubwa, naomba mnisikilize kwa makini, lakini msininukuu vibaya. Kanisa Katoliki, viongozi wake rafiki zangu, wale wa juu nawafahamu sana, Kanisa hilo limetoa mwongozo kuelekeza anayefaa kuchaguliwa katika uchaguzi ujao.

“Mimi nikautafuta na kuusoma. Sasa hili Kanisa Katoliki linatoa mwongozo wa kuchagua kiongozi wa kisiasa, kwa maana hiyo huu ni mwongozo wa Wakatoliki. Si utakuwa mwongozo wa Wakatoliki pekee?” alisema Kingunge akihoji.

Aliendelea kusema: “Kwa hiyo KKKT (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania) nao watoe mwongozo kwa sababu wao hawaongozwi na Kanisa Katoliki, ni Wakristo ndiyo, lakini mantiki tu. KKKT wakitoa, Pentekoste watatoa wakwao na Anglikana bado, nao watatoa wakwao, Waislamu bado na wao watoe wa kwao.”

Kingunge ambaye ni mmoja wa wabunge wa muda mrefu ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu enzi za Mwalimu Nyerere Rais wa Kwanza wa Tanzania aliongeza kuwa anazungumza hayo kwa kuzingatia mantiki ya mwongozo huo.

“Ni mantiki tu, nasema kwa heshima zote nawaomba viongozi wa Kanisa Katoliki, nawapenda sana, nawaomba warudishe ule mwongozo wao, sisi tunataka nchi moja na tuishi pamoja kwa kushikamana, hatutaki kugawanyika kama Lebanon,” alisema Kingunge bila kufafanua zaidi kuwa waurudishe wapi na kwa vipi.

Kauli hiyo ya Kingunge imetolewa wakati waraka huo wa Kanisa Katoliki umezua mjadala miongoni mwa watu wa kada mbalimbali, huku baadhi wakilishutumu kanisa hilo wakidai kuwa linaingilia masuala ya kisiasa.

Hata hivyo, juma lililopita Askofu Msaidizi wa Kanisa hilo Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini alisema mafisadi wanauhofia mwongozo huo.

Kwa mujibu wa Kilaini mwongozo huo unaweka vipaumbele vya nchi katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, ndiyo maana wanaupinga.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya misa ya upadrisho iliyofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jimboni humo, Kilaini alisema mwongozo huo ulianza kutumika tangu uchaguzi wa mwaka 1995 na kusisitiza kuwa kwa mwaka huu watu wengi wameshtuka kutokana na kugusa masuala ya ufisadi.

Kanisa hilo lilitoa vitabu viwili vya mwongozi na vipaumbele vya nchi kabla ya kuuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2010, mwongozo ambao umekumbana na vipingamizi kutoka kwa baadhi ya wanasiasa kwa madai kuwa dini inaingilia mambo ya siasa.

“Kwanza napenda watu waelewe kuwa mwongozo hauna lolote kuhusu dini kama watu wanavyodhani, kwa sasa jamii imeshituka kuhusu vitendo vya rushwa na ndiyo sababu baadhi ya wanasiasa wanapinga muongozo huo kwa kuwa unalenga kuwafungua watu macho na kukemea vitendo vya ufisadi,” alisema Kilaini na kuongeza.

“Ninachowataka wanasiasa wote washiriki kupiga vita ufisadi. Asiyetaka kupigana na ufisadi tusimchague na ndivyo mwongozo huo unavyosema,” alisema.

Alifafanua kuwa mwongozo huo unazungumzia juu ya serikali na msimamo wake na wala si kumchangua mtu fulani wala chama fulani kwa ajili ya kumpa uongozi.

“Watu wausome mwongozo huo kwa moyo mweupe na ninaamini wataufurahia, utakuza ufahamu juu ya masuala ya kidemokrasia,” alisema Kilaini.

Awali Mbunge wa Kigoma Kusini, Manju Msambya alishutumu mwongozo huo aliouita kuwa ni "Waraka wa Kiaskofu" wakati akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya Wizara ya Sheria na Katiba, akisema unawafundisha waumini wake kuhusu namna ya kuchagua viongozi kwa imani zao na kuonya kuwa nchi inaweza kuingia kwenye vurugu.

Msambya ambaye hakutaja moja kwa moja dhehebu la dini lililotoa waraka huo, alisema unapingana na kanuni inayosema watu wasichanganye dini na siasa.

Lakini Askofu Kilaini alisema mwongozo huo haukutungwa na maaskofu wala mapadri wa Kanisa hilo na kufafanua kuwa umetungwa na Chama cha Wataalam wa Kanisa Katoliki (CPT) na kwamba wao waliupa baraka zote baada ya kuusoma na kuona unafaa.


Source: Mwananchi
 
Mwaka 2007 alipinga vikali List ya Shame ya CHADEMA. akaja na kupinga kuwa CCM haina Mafisadi leo wote wamefikishwa mahakamani na hakuna jipya hivyo hakuna haja, then yeye hana Dini kinamuuma nini Sasa
 
Wiki jana niliandika barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Kikwete na kuiweka kwenye JamiiForum siku ya Ijumaa. Barua hiyo ilikuwa katika lugha ya Kiingereza. Pamoja na mambo mengine nilimwomba Rais na serikali yake wasichukulie waraka wa kanisa katoliki kama mzaa. Mimi ni mkatoliki na kiongozi wa ngazi fulani hivyo najua kinachoendelea. Wakatoliki wana mtido wa kufanya mambo yao kimya kimya na kupitia katika waraka huo kuna ujumbe mahususi na mzito. Jambo nililomwomba Rais wetu kupitia vyombo vyake achunguze kiini cha waraka huo. Kwa nini sasa na si wakati mwingine? Hizo semina zinaelekeza tu yale yaliyomo kwenye waraka au kuna mengine zaidi ambayo hayakuandikwa kwenye waraka? Rais akipata jibu atajua jinsi ya kutatua tatizo hili. Ili nataka kusema kwamba Mzee Kinguge asipoteze muda wake kushauri kanisa katoliki kwa lolote maana kanisa haliendi hivyo. Angetaka angewasiliana na viongozi wa kanisa faragha na sio kupitia Bungeni. Ushauiri wake umepitia sikio la kushoto na kutokea sikio la kulia!
 
Mimi naungana na Mh Kingunge kupinga WARAKA huo wa wawakatoliki. Tunafahamu wazi kuwa waraka huo una baraka zote za Pengo, baraza la maaskofu, balozi wa Vatican na hatimaye Papa.

sasa kama hilo baraza lina hamu ya kufanya hao basi wavue majoho yao na kuingia kugombea uongozi wa kisiasa kama alivyofanya Dr Slaa.

HONGERA SANA KINGUNGE

Barubaru,

Hivi ni kweli umeusoma huo waraka au unakurupuka tu kutoa comments? Hebu tueleze kwa kifupi tu ni kipi ambacho hukukipenda kwenye huo waraka! Wapi unafikiri wataalamu wakatoliki wamepotoka kwenye huo waraka wao!!!!

Tusaidie tafadhali ambao labda hatukuusoma na kuuelewa vizuri huo waraka.

Tiba
 
Kamwe siwaungi mkono viongozi wa dini mpaka na wenyewe watoke na wajisafishe kwenye tuhuma za kutumia vibaya misaha. Hivi hiyo 30% ni kiasi. Mpaka kieleweke wanasiasa na hawa viongozi wa dini kila mtu awajibike. wakati tunatuma msg za kuwasakama wanasiasa tusisahau meseji za keuelezea misamaha inavyofujwa. Lazima tuseme wananchi watambue kila mtu ni mwizi tu hapo

Mafisadi payroll at work!!!!!!!

Tiba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom