Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Mkuu;

Mafisadi wana kazi kwelikweli. Askofu msaidizi amesema waraka uo hauzungumziii dini yeyote.Jamani wabunge si mnao kwanini mhandikie mate angali wino upo. Vuta waraka huo bungeni chambua ambako kumendikwa kuchagua viongozi wakatoliki na sio dini nyingine waite na kuwafungulia mashitaka walioandika.

QUOTE]

Mheshimiwa Shibuda aliusifu sana huo waraka akiwa anachangia Bungeni juzi na huku yeye ni Muislam. Tiyari umeshaanza kuandikwa kwenye vyombo vya habari Raia mwema wiki iliyopita walidokeza... Nadhani huo waraka ungekuwa ni mbaya tiyari Waislam wangeshaanzisha zogo la nguvu!! Walipouona na wenyewe wakatamka kuwa wanaanzisha wakwao!! Sasa Mhe. Kingunge nadhani analake jambo "Siasa" anataka kuturudisha kuleee kwenye chama kimoja, unapiga kura ya mtu mmoja huku sehemu nyingine ikiwa haina hata jina
 
Acheni kudanganyana mwisho wa siku mambo yote yatakuwa hadharani,jiandaeni kwani najua wengi uwezo wa kushambulia hamna ila mna uwezo wa kukimbilia mabaya tuu,amini nawambia itafika siku baba atamtelekeza mtoto wake na mtoto hatomjali baba yake kwa uchungu wa siku hiyo,kesheni mkiomba mema kwani hamjuhi siku wala saa.Mungu ibariki taifa letu la Tanzania pia wabariki wana JF wenye mwelekeo mwema na nchi yao.
 
Viongozi wa Kanisa Katoliki ni wasomi wazuri sana. Kingunge naye ni msomi mzuri pamoja na Upagani wake. Naamini ameuelewa fika waraka huo wa Kanisa Katoliki, ila anachofanya ni kupotosha makusudi ionekane kwamba hawa wanaingiza udini kwenye suala la uchaguzi. Kinachowakera viongozi wa kanisa ni kuona wanasiasa wasio waadilifu wakihaha kuingia madarakani kwa njia ya rushwa. Hawa ni wanasiasa ambao wakishaingia madarakani huwa hawana agenda yoyote ya kuleta maendeleo kwa wananchi bali kujilimbikizia mali kwa njia za kifisadi na kutetea mfumo wa kifisadi ili waendelee kuwanyonya wananchi. Baada ya kufunuliwa, viongozi wa kanisa sasa wameona ni vema wasaidie kutoa elimu ya uraia kwa waumini wao kuwatahadharisha kuhusu fisi hawa. Kuna ubaya gani katika hili? Udini uko wapi hapo? Come on Mpagani Kingunge!
Hata wawe wasomi kiasi gani haijastify kutokuwa critisize. Sera nyingi tu huandaliwa na wasomi kama zile za loan board nk. Suala la msingi hawa wanaopinga ufisadi wao ni wasafi? Wanasemaje juu ya misamaha? Waandike basi kama inaandikika. Waache unafiki viongozi wa dini wajisafishe kwanza wao. Wamejaa majungu, fitna, choyo na ufisadi yale ambayo wanayekemea mara kwa mara. Waache kuiba kwenye misamaha, sadaka na kuwaalika hao mafisadi kwenye kufungua shughuli zao au hata kupokea michango yao
 
Mkuu MzeePunch, angalia bold hapo juu!!! Kingunge amesoma wapi vile??? Au ni kule Urusi walipelekwa kupata desa la propaganda!!! Jamani wenye CV ya Kingunge Ngombale Mwiru wanitupie hapa, na ionyeshe vyuo na kiwango cha elimu. Isiwe ni vile vyuo vinavyotoa vyeti vya utata au kwa kifupi vile ambavyo huwa ni rahisi kwa watu kuvitumia kwa kuwa these colleges/universities are not acredited!!!! Babu kubwa!!!
 
Amini amini nawaambia.... Hakuna fisadi atakayepona 2010 baada ya wana wa nchi hii kuamka. Tunawashukuru sana viongozi wa Kanisa Katoliki kwa mwongozo huu. Mungu awabariki na awalinde.
 
Wanasema waliupitia na wakaridhia uende kwa jamii. Note: Post zangu zoote nawataja viongozi wa dini na si maaskofu
Kwa kweli hata mimi ingawa sio mkatoliki kiasi hicho naukubali sana kwa mazingira na hali tuliomo kama NCHI. Viongozi wa dini katoliki wanaitwa MAAskofu na ndio waliotoa tamko kuunga mkono waraka huu.
 
Maane, ni vigumu kupata kumbukumbu za vyuo alivyosoma huyu Mpagani kule Urusi kwani vilibomolewa na vingine kuteketezwa kwa moto wakati wa mageuzi baada ya warusi kugundua kwamba vilitumika kupandikiza propaganda za ajabu kwenye vichwa vya watu ili waendelee kuwa masikini milele.
 
All in all si maaskofu hawa viongozi wa dini karibu wote nao imekuwa too MUCH inatosha sasa. Wao wanatufilisi kwa style yake pia. I am sure wakati wao unafika sasa si muda mrefu.
 
Hata wawe wasomi kiasi gani haijastify kutokuwa critisize. Sera nyingi tu huandaliwa na wasomi kama zile za loan board nk. Suala la msingi hawa wanaopinga ufisadi wao ni wasafi? Wanasemaje juu ya misamaha? Waandike basi kama inaandikika. Waache unafiki viongozi wa dini wajisafishe kwanza wao. Wamejaa majungu, fitna, choyo na ufisadi yale ambayo wanayekemea mara kwa mara. Waache kuiba kwenye misamaha, sadaka na kuwaalika hao mafisadi kwenye kufungua shughuli zao au hata kupokea michango yao

Hapa tunazungumzia WARAKA na sio mambo ya misamaha. Kama unataka masuala ya misamaha anzisha thread nyingine! Nina mashaka kama ume-take trouble ya kuusoma huo waraka.
 
Hapa tunazungumzia WARAKA na sio mambo ya misamaha. Kama unataka masuala ya misamaha anzisha thread nyingine! Nina mashaka kama ume-take trouble ya kuusoma huo waraka.
Mbona mmeweza kutaja ufisadi wa wa kina Kingunge hadi elimu yao. Lets be realistic mmegusa huko ngoja na siye tuseme upande unaofanana na huo. Kama unahoja ya kuwanasua kwenye hilo saidia kaka. Maana misamaha ni UFISADI, kama wanavyozinduliwa wananchi kwenye ufisadi wa kisiasa na hayo yaandikwe pia
 
Bado tuna kazi kubwa nchi hii! Kama hii ndiyo level ya uelewa wa watu wetu, sioni ni jinsi gani tutajikwamua kutoka kwenye makucha ya mafisadi.
 
Maane, ni vigumu kupata kumbukumbu za vyuo alivyosoma huyu Mpagani kule Urusi kwani vilibomolewa na vingine kuteketezwa kwa moto wakati wa mageuzi baada ya warusi kugundua kwamba vilitumika kupandikiza propaganda za ajabu kwenye vichwa vya watu ili waendelee kuwa masikini milele.

You said it all Mzee wangu. Yaani nashukuru hata kile cha pale Kigamboni wameona hakina maana ile iliyokusudiwa awali. Angalao hawakikichoma moto bali wamekibadilisha badilisha fulani hivi. Eti walikuwa wakitoka huko kwenye vyuo vya propaganda walikuwa wanapelekwa pale kusafishwa bongo, was it brain cleansing or what???? Tanzania bwana.

Ila jamaa letu Pagani Kingunge sijui aligutukaje kuona atakufa maskini atabaki kujengewa nyumba na jeshi akaamua kuwa katika jury ya kulisambaratisha Azimio la Arusha. At least kwa Azimio lile la 1967 kuna mambo mazuri yalikuwepo, siyo yote mabaya, na kama ni kulibadilisha basi wangefanya kwa awamu!!!! Wao walifanya full to allow full corruption, wahujumu uchumi, the fisadis, you name all, etc.
 
Tunawasakama wanasiasa bura nani kasema hawa viongozi wa dini si mafisadi? Harambee zote makanisani nani huzifanya? Taifa linapoteza asilimia 30% ya mapato yake kwenye misamaha, ni nani anaiba kama si hawa viongozi? Waache ufisadi kwanza ndio waweze kuwanyooshea vidole wengine. Wajitenge na siasa vingenevyo na wao wataumbuka kwa madudu wanayoyafanya

Mimi nafikiri hujui maana ya ufisadi kama ungeijua usingesema viongozi wa kanisa ni mafisadi.Hali tuliyonayo Tanzania kwa sasa inachangiwa kwa kiasi kikubwa na ufisadi uliosababishwa na wanasiasa walio madarakani.Hili hata mtoto wa darasa la saba hakawii kulitambua.

Vita yetu wana jamii ni dhidi ya ubadhilifu wa rasilimali zetu unaofanywa na viongozi tulio waweka madarakani.Wewe kama hulioni hilo sijui unataka usaidiwe kwa vipi.
 
Mianya ya ufisadi ni mingi ninakiri wazi hawa viongozi ni mafisadi. Na wale wanaoiba kwenye misamaha tuwape jina gani pia?
 
Mkuu, umefanya kazi takatifu. Ilikuwa kidogo na mimi niutume tena hapa JF.

Waraka huu unapaswa kutunzwa hala tuanze kuujadili na kuusambaza utakapokaribia uchaguzi! Tena hakuna haja ya kuomba copyright maana nasikia wakatoliki wamekubali uchapishwe na usambazwe na yeyote anayeweza kuusambaza. Ukizani nabisha piga simu kwa walioundaa yaani Chama Cha Wanataaluma Wakatoliki na namba yao hii hapa (022-2127675)

Mtumie MJJ kwenye cheche aanze kuutoa maramoja sio kusubiri
 
Jamani mwenye website ya bunge atupatie tucheck CV ya Kingunge si ipo pale jaribuni kuangalia kisha muianike hapa.
 
Hapa tunazungumzia WARAKA na sio mambo ya misamaha. Kama unataka masuala ya misamaha anzisha thread nyingine! Nina mashaka kama ume-take trouble ya kuusoma huo waraka.

Mwambie kabisa Mzee. Hapa ni waraka wa kuelekea 2010 na si misamaha ya kodi. Na kila mtu aelewe kuwa misamaha ya kodi ni kwa kila dhehebu, wakristo kwa makundi yao na Waislam kwa makundi yao. Na pengine tunaona wivu na misamaha ya kodi kwa Wakristo kwa kuwa wanaji-commit full kwa huduma za kijamii na ziko effective, tizama hospital zao, shule za Seminary na sasa za Secondary za kawaida, Vyuo vyao, etc. Yaani wana mipango mizuri sana. Na leo wakristo wakiamua hakuna huduma za jamii hiyo mikoa ya pembezoni wazalendo wetu watakufa, hebu ona machache kama Peramiho Hospital, Karatu Lutheran Hospital, Dareda Hospital, you name all. Je serikali huko nilikotaja na kwingineko kuna huduma za afya au ni zile dispensary ambazo hazina workforce na vitendea kazi??

Please, Wakristo wana haki ya kuilaani serikali hii kwa maana mchango wao ni wa dhati na unaonekana wazi. They have heart for the heart!!! Bisha.
 
Hili ndilo analohofia Kingunge na makuwadi wa ufisadi.Huu waraka ni tishio kwa mafisadi na wanasiasa type ya Chitalilo na Serukamba!
mbona Makanisa yote wanamtetea Mkapa!!! pia juzi walikuwa kwa Lowasa!!! tena wote kuanzia top sasa hapo kweli wako serious na Ufisadi kweli??? Wanatuyumbisha hawa "Nadhani Yesu yu karibu kuja"!!!!
 
Kingunge katoa maoni yake kama kiongozi mzoefu na raia wa Nchi hii. Tukimjadili yeye na mwanae na mke wake hatutakuwa tumelenga kwenye hoja yake ya UMOJA,AMANI na UTULIVU wa NCHI yetu. Anajua nafasi ya Viongozi wa DINI katika jamii yetu na ushawishi wao. Anajua pia hoja zilizomo kwenye waraka huu zimepotoshwa kwa makusudi na baadhi ya Waislamu na Wanasiasa uchwara na muflisi kama Manju Msambya, anaelewa pia kiwango cha uelewa wa watu wetu hasa wale ambao elimu ni ndogo, anaijua CCM yake na viongozi wao, waraka huu anauona kama mwiba unaoelekezwa kwenye kidonda.
Ningekuwa yeye kwa nafasi yake kama Mbunge wa IKULU ningemwomba Mh Rais na Mh Spika tuujadili BUNGENI na hata kwenye NEC ya CCM.
 
Kingunge, Where is th problem.

Me I think what have been issued by RC pastors is just for their followers and they have not anywhere be seen forcing others to either read of follow it.

T his document is just like CUF, CHADEMA or TLP manifestos? I have never heard CCM compalining about other party's manifesto. Or is it bad to tell your children to behave in a certain manner? Why only CCM is complaining and not CUF? Kingunge should help cleaning CCM house and not just come up with confusing agendas.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom