Waraka huu unaweza kuligawa taifa. Bora upelekwe kanisani.
Wewe ni dhahiri hujausoma huo waraka au una chuki tu za kidini.
Waraka huu unaweza kuligawa taifa. Bora upelekwe kanisani.
Maana yake ni kwamba kabla hajauchana aliusoma, na hivyo ujumbe umemfikia. Atakuwa anaendelea kutafakari taratibu, halafu baadaye atakuja kuwa muhamasishaji na mgawaji mzuri wa waraka huo. Hii ni kama ilivyokuwa habari ya Paulo (Sauli).
kwanini wakatoliki jamani. kwani Tz ni ya wakatoliki?
Mkuu wangu, usidhani sikuelewi. Nina kuelewa sana tu. Nadhani nakuelewa kuliko ninavyotakiwa kukuelewa. Maelezo mengi hayawezi kunifanya nikuelewe zaidi.
Mkuu wangu labda ni summarize ninachomaanisha:
1. Waislam kama watu wengine wote nchini wanayo haki ya kutimiza sala zao kama inavyoagizwa katika maongozi ya dini. Ikiwa ni pamoja na kuwa na Mahakama ya Kadhi
2. Waraka unaoutumia kujibu hoja hapa si waraka uliotolewa kama ilani, bali ni ujumbe kwa wakatoliki (internal document). Kuna document 2 ambazo najua umeziona zote
3. Serikali haina haja, ulazima wala sababu ya kufuata ushauri kutoka kundi lolote la jamii endapo ikiona hakuna manufaa katika ajenda zake kufanya hivyo
4. Kila mtu anayo haki kikatiba kutoa maoni yake bila kuvunja sheria za nchi
5. Katiba ya nchi ni ya wote. Wenye dini na wasio na dini. Isibadilishwe kwa manufaa ya dini moja au kundi fulani la watu pekee
6. Ushiriki wa maendeleo ya jamii ni wajibu wa kila mtu ndani ya jamii. Mafundisho yoyote yanayoweza kuisaidia jamii si vibaya kutolewa na yeyote bila kujali dini yake, rangi yake, sura yake, jinsia yake, nafasi yake, itikadi yake wala umri wake n.k.
7. Makosa ya jinai yafuate mkondo wa sheria inayohusika
8. Dini zote zina lengo la kumkomboa binadamu na hasa muumini wake. Hakuna Dini bora duniani zaidi ya nyingine
Mkuu hiyo ndio imani yangu kutokana na suala hili.
Rufiji,
.. yale yale tukisema Pepo wewe unafikiria tunazungumzia shetani..
Ukiwa na maana sisi tumesimama upande wa pili tunapinga kanisa katoliki pasipo sababu.. jambo ambalo sii kweli kwa sababu nimekwisha sema wazi kuwa hata kama ningekuwa Mkatoliki, uwakilishi wa waraka huu nisingekubaliana nao...Ungewakilishwa na Msikiti au Sheikh nisingeukubali, hata kama waraka huu ungeandikwa na Pagan au Mkristu ningeukubali lakini ukawakilishwa na chombo cha dini ya Kiislaaam, nisingeupokea.. Ungeandikwa na dini zote mbili sawa lakini sii kwa kutumia aya na sura za dini hizo kama dira ya waraka na mwoingozo kwa society nzima nisingeukubali..Sura na aya hutumika kama kibwagizo cha kufikisha ujumbe lakini sii mwongozo wa ujenzi wa waraka au mkakati wa kile kinachojengwa.Watu wengi wanaopinga huu waraka wanapinga tuu kwa sababu umeletwa na wakatoliki , lakini awajawa specific katika kukosoa kilichomo katika huo waraka. Mimi napinga kabisa wale wanaojaribu kufananisha huu waraka na mahakama ya kadhi, huu waraka hauitaji kodi ya walipa kodi ili kuwa implemented ! Mahakama ya kadhi inataka hela za walipa kodi zitumike kitu ambacho sio sahihi....