Nadhani wewe ndie una matatizo ya uelewa. Its this simple kama wanataka siasa fursa hiyo ipo waingie kwenye siasa.
Upo hapo?
KIINI CHA MIGOGORO NI KUCHANGANYA DINI NA SIASA - SENDORO
NA MARTIN MALERA
ASKOFU Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Elinaza Sendoro, amesema migogoro mingi ya kidini inatokana na kuingiza siasa katika dini hizo.
Askofu Sendoro alisema hayo jana, wakati akichangia mada ya mgogoro wa kikundi cha Wanamaombi na Kanisa Katoliki, mgogoro wa Dayosisi ya Pare na Mgogoro wa Dayosisi ya Meru katika kongamano la Dini na Demokrasia, linalofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Askofu Sendoro alisema katika mgogoro wa Dayosisi ya Pare, kuna Waumini wa Kanisa la KKKT, waliokuwa viongozi wa Serikali na baada ya kustaafu wakajiingiza katika uongozi wa dini na kuingiza siasa katika Kanisa hilo.
Alisema hata katika migogoro ya dini nyingine, chimbuko lake ni viongozi wa dini hizo kujiingiza katika masuala ya siasa.
Mbali na suala la siasa kuingizwa katika dini, Askofu Sendoro pia alisema migogoro mingi ya kidini ni ya siku nyingi na inapanuka kwa vile maamuzi yao hayako kisheria.
Alisema Kanisa au Msikiti unaweza kutoa uamuzi, lakini uamuzi huo haufuatwi kwa vile hauna mamlaka kisheria, inayotambulika na Mahakama.
Naye Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padre Pius Rutechura, alipendekeza iundwe Tume ya utatuzi wa migogoro ya kidini itakayojumuisha viongozi wa dini mbalimbali nchini. Pia alisema kuna haja ya kupanua wigo wa mazungumzo ya kidini kwa kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa kidini. Alisema migogoro ya kidini ni kitu cha kawaida kutokea, lakini utatuzi wake uanzie ndani ya dini zenyewe kabla ya kutoka nje.