Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
- Juzi walienda kufungua kitabu cha mke wa Lowassa, leo wanaanda waumini na uchaguzi! Huyu Lowassa tuna safari ndefu sana naye na hili taifa.

Mungu Aibariki Tanzania.

FMEs!
 
nilvyoona askofu nilizania pengo nikataka kushangaa tangu lini yeye akapinga ufisadi...


Mazee halijatajwa neno askofu hapo na sijui wapi ulipolipata, hivyo unaweza uka-reserve your idle comment mpaka fursa itakapopatikana..bila hivyo tutachukulia kuwa una matatizo ya ku-imagine vitu visivyokuwepo mazee.
 
Mbona haya yalifanyika pia chaguzi zilizopita. Waliwafundisha waumini wao jinsi ya kupiga kula na nani wa kumpigia kula.

Matoke yalipotoka wakatuambia kuwa ni chaguo la Mungu...!


Wamekosa walicho ahidiwa waamua kutamka hadharani.

Naona unaunga unga vipande visivyohusiana ili kukidhi conclusion yako uliyokwisha ijenga tayari kichwani mwako. Inasikitisha mtu anapoweza kupoteza muda kukusanya vipande vipande vya habari nusu ili kubomoa badala ya kuutafuta ukweli utakaomuweka huru.

Wahenga wanasema chuki na husda huziba milango ya fahamu na umedhihirisha hili ndani ya post yako kuhusu hoja yako 'Chaguo la Mungu', mwenyewe umeiweka hii..lol

“Ni vema nikaeleweka kuwa maandiko ya Mungu yanasema uongozi na mamlaka yote hutoka kwa Mungu, hivyo basi rais aliyechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi wenyewe ndilo chaguo la Mungu na sisi tutaendelea kuwa na msimamo huo,” alisema Askofu Kilaini

Ila tuendelee kujadili mpaka tudhihirishe kuwa chuki na upeo finyu wa baadhi ya wachangiaji ndio hasa tatizo na wala sio lengo-mama lililotangazwa na kanisa kama lilivyonukuliwa ktk post ya kwanza.
 
eti chaguo la mungu.. why wud Mungu give a toss about who gets elected?lol This is just stupidity. Watu wamejaa makamasi kwenye akili let them continue to be controlled by these so called elects-of-god. They are just imposters, their history tells it all.

Ok, talking of impostors, how about we start discussing it rightaway..and let me toss the first topic..eerrhh..the prophet of islam..Shall we?
 
Halisi,

Kuwa muangalifu na hao "ndugu" zako watakuita mdini ilhali wewe huna mambo hayo na umekuwa ukifanya nao kazi bega kwa bega na always kwako Tanzania kwanza halafu ndio mambo mengine.

Ndugu inaonekana una matatizo ya msingi. Kwanza ni wapi ndg Halisi amesema yeye ndiye aliyeandika hiyo article?

Hayo hayo ya "elimu kwa wapiga kura" yangesemwa msikitini au kwenye kongamano la waislam ungeona michango ya "ndugu" zako hapa na hoja za 'kusilimisha" nchi zingemwagwa hapa.

Sasa hii inahusiana vp na subject matter? Lack of objectivity huwa inatuleteaga matatizo sana sisi ngozi nyeusi. Badala ya kujadili hoja muhimu ambayo ni elimu kwa wapiga kura, tunaangalia kuanzisha mitafaruku mipyamipya badala ya kuangalia adui yetu ni nani.

Lakini kwa kuwa wamesema wao wenye haki ya kusema chochote bila kuonekana wadini hakuna taabu hapo.

Haki ya kusema nani? Hizi ndizo kauli za chuki zinazosababisha tuendelee kuwepo hapahapa ..badala ya kukabili matatizo yaliyopo ..tunatengeza dhana na matatizo mapya.

Tahadhari yangu kwako ni kuwa wewe hawa huwajui, nasisitiza huwajui lakini muombe mola wako uhai mrefu utakuja kukumbuka haya ninayo kuambia. Kwa ufupii tu kwa sura ya nje utawaona "wenzio" lakini wakiwa wao kwa wao wewe sio mwenzao lakini kwa sasa kwa kuwa unacheza ngoma yao watajitahidi kwa kadiri ya uwezo wao wote usilione hilo.

Sasa hata ngoma imeingia ndani na umegeuka nabii na shehe Yahya at the same time. Mazee you need to think beyond this kama una matumaini yeyote ya kuikomboa nchi yetu.

Hii vita ya ufisadi imeficha mambo mengi ndani yake unahitaji miwani mikali kuliona hilo.

Na ndio maaana hakuna atakae kemea hilo la "kuandaa waumini uchaguzi 2010" kwa sasa ni la kwao na tazama choice ya maneno hapo wameitwa "waumini" sio wakristo sasa sijui Kanisa Katoliki litawapata wapi waumini wasio wakristo kuwapa hiyo elimu je hao waumini "wanaoandaliwa" ni waumini wa aina gani hapo? huhitaji kuwa rocket scientist kujua hilo. Na katika hilo zile rhetoric za tusichanganye dini na siasa, nyumba za dini kwa ajiri ya dini tu nk. haina nafasi kwa sasa.

Huu ni wangu wasia nasisitiza ila endelea "kukaa vizuri" na ndugu zako hao ukijua utamu wa mua ukiisha ganda hutupwa!

Masalaam

Nadhani lengo la kuelimisha limelenga kwa waumini wao kwanza, due to obvious reasons..mojawapo ni logistics na pili ni chuki kama mlizomwaga hapo juu. You don't need to be a nuclear scientist to see this too..

Just imagine ..wana funds kiasi gani kuweza kuwafikia waumini wao kutengeza materials za kufundishia..badala ya kuwapongeza na kuwapa moyo mmeanza kwa kuleta mawazo hasi na shutuma kabla hata ya kuelewa msingi wa wanachofanya. Sasa ktk mazingira kama haya mlitaka wawafuate majumbani kwenu wakati tayari mna chiki na chuki ya hali ya juu?
 
Binadamu yoyote ni chaguo la Mungu ,na ndiyo maana akawepo hapa duniani.Ndiyo JK ni chaguo la Mungu ndiyo maana yupo Duniani kutimiza hapa duniani portion yake aliyotumwa.Asingekuwa chaguo lake na asingepata kuwepo duniani.

Watu wanafikiri Chaguo la Mungu ni mpaka awajaze mapesa mfukoni.Wakati mwingine ni CHAGUO ili kitu fulani kipate kutimia ama wanawaadamu wapate kufikishiwa ujumbe fulani ama kwayo wapate kuuamka na kuchukuwa mwelekeo sawia.
 
Mosi, Unaposema wao, hiyo wao inamui-include nani na kumuacha nani mazee? Pili, Lete ushahidi wa uyasemayo ili tusikupuuze mazee.

NB: Kutokujibu hoja itachukuliwa ni utaahira.

ebwana vipi wewe mbona unataka kulazimisha hoja hapa?tangu lini umekuwa kiranja wa kuamrisha watu waandike unavyotaka wewe?
tusikupuuze=wewe na nani?
sasa mimi sijibu unavyotaka wewe,haya amua unaloweza
 
A significant question that has been posed here is whether leaders like JK are indeed “chaguo la Mungu”. Yes, ni “chaguo la Mungu”, but one has to know what that means.

God gives us what we deserve. Ni “chaguo la Mungu” in the sense that He allowed it. Hata Pontius Pilate alikuwa ni chaguo la Mungu.

Of fundamental importance is the question about why God would allow evil men to rise to power. But that is just a part of the larger question about why God allows evil in the world. There is only one correct answer, and that is: He allows evil on order to bring a grater good out of it. The greatest evil that ever happened in the world was the crucifixion of the Son of God, and yet that evil resulted in the greatest good ever, which is our salvation.

We are currently ravaged by corruption and mismanagement. Out of this evil, there will emerge a better informed citizenry, true democracy and rule of law. We needed and deserved the people we elected.

I would say Fr. Mapunda spoke prophetically. He dares to ruffle feathers when the need arises. He is absolutely correct when he says that the National Electoral Commission is not democratically constituted. How can one of the teams singly select the referee?
 
Augustine Moshi,
Mkuu imani yako si lazima iwe imani ya kila mtu..Na pengine mimi napingana na hata baadhi ya waislaam wenzangu ktk hili.
Mimi nachosema ni kwamba viongozi tuliokuwa nao ni uchaguzi wetu sii wa Mungu. Mungu chaguo lake ni mitume - Prophets na sii viongozi kama hawa maanake utakuja sema hata Hitler alikuwa chaguo la Mungu.
Binafsi sina matatizo na Ujumbe wa kanisa kwa sababu wanachokusudia kufanya ni kuwafundisha wananchi kile ambacho serikali yetu imeshindwa..
Na siku zote dini husimamia maslahi ya watu wote bila kujali dini zao pamoja na kwamba kuna imani inayotakliwa kufuatwa. Ktk mfano huu nachukulia dini kama vyama vya siasa..Siwezi kupingana na CCM au Chadema hata pale wanapotaka kueneza ujumbe mzuri kwa wananchi au hata waumini wake ati kwa sababu tu sina imani na viongozi wake..
Uchaguzi nchini ni kitu muhimu sana na hata siku moja tusitake kumwingiza MUngu kwa sababu hizi ni fikra za Kitumwa na zililetwa na wakoloni ktk kutupumbaza..Viongozi wote wa dini au serikali ni chaguo letu sisi wananchi kulingana na CV tunayoihitaji unless unataka kunambia hata hiyo CV kaileta Mungu nasi tunafuata maagizo ya Mungu..
Kanisa katoliki endeleeni na dhamira kama hii na ningependa sana viongozi wa dini na madhehebu mengine wafuate mfano kama huu...
 
Maana ya kusema ni chaguo la Mungu ni kama vile ukimpa mtoto ruhusa ya kuchagua mke, hata akichagua mbaya tunasema huyo mke ni chaguo lako.

Mungu katupa UHURU wa kuchagua viongozi. Wale tuliochagua ni "chaguo lake", kwa maana hiyo. Haina maana kwamba ni wazuri.
 
Well Mungu hajatuambia tuchague viongozi wetu ambao ni wake pia kama huyo mzazi..
Tofauti za dini, madhehebu na siasa ni utaratibu wa chaguzi zetu sisi binadamu..
 
Kumbe makeke yote haya ni kumuandaa Lowassa kuwa Rais wa Tanzania?

ebwana vipi wewe mbona unataka kulazimisha hoja hapa?tangu lini umekuwa kiranja wa kuamrisha watu waandike unavyotaka wewe?
tusikupuuze=wewe na nani?
sasa mimi sijibu unavyotaka wewe,haya amua unaloweza

Kwa sababu umeshindwa kuleta majibu mujarabu, sina budi kukupuuza..maana naona watu humu wanatumia mwamvuli wa u-Great Thinker kuleta mashudu yao..lakini tupo hapa kuhakikisha hoja zenye maana zinaprevail..
 
Binadamu yoyote ni chaguo la Mungu ,na ndiyo maana akawepo hapa duniani.Ndiyo JK ni chaguo la Mungu ndiyo maana yupo Duniani kutimiza hapa duniani portion yake aliyotumwa.Asingekuwa chaguo lake na asingepata kuwepo duniani.

Watu wanafikiri Chaguo la Mungu ni mpaka awajaze mapesa mfukoni.Wakati mwingine ni CHAGUO ili kitu fulani kipate kutimia ama wanawaadamu wapate kufikishiwa ujumbe fulani ama kwayo wapate kuuamka na kuchukuwa mwelekeo sawia.

Napenda ulivyoliweka hili bayana.

Anyway, hoja hasa ya msingi ilikuwa ni umuhimu wa elimu inayotolewa na kanisa katoliki kuhusu haki za raia kupiga kura na kuchagua viongozi bora. Bahati mbaya au nzuri hii hoja ilikwishawekwa hapa jamvini kama mara mbili ktk miezi michache iliyopita hapa JF kupinga upotoshaji wa makusudi wa baadhi ya vyombo vya habari na wengine wanaotaka kulifanya zoezi lionekane ni kuwaweka madarakani viongozi kwa matakwa ya kanisa..Ikaletwa mpaka attachment hapa watu wasome ili wajue kiendeleacho lakini watu naona wanatanguliza chuki kwanza na maarifa baadae.

Wanaoleta hoja dhaifu kama hizi za kushutumu mambo wasiyoyaelewa vyema, si tu ni wahuni wenye kumbukumbu finyu, bali hata nashawishika wana lao jambo ambapo inabidi sasa tu-raise our eyebrows na kuwatazama kwa macho matatu kwani si bure kuna mtafaruku wanataka kuuanzisha.

Si mara ya kwanza kwa kanisa na kuwaelekeza waumini wake na kusisitiza umuhimu wa kuitumia haki yao ya kikatiba. Chaguzi za nyuma waumini walisisitizwa kujiandikisha na kuambiwa kuacha kupiga kura ni kuacha wajibu ( Sio haki). Wenye kuhamasika walihamasika wakajiandikisha na kupiga kura. Sasa sijaelewa kwa kuelekea 2010 kwanini ionekane ni special case na kila mwenye kinywa anataka kulazimisha kuelezea hata yale yasiyokuwepo na wasiyoyaelewa vizuri. Kama kanisa lilngekuwa na nia mbaya sidhani kama lingeweka wazi hizi harakati zake, its very logical watu hapa wanasukumwa na chuki na jazba badala ya reason.
 
Kanisa lina wajibu wa kuwaelimisha waumini kuhusu uchaguzi. Kanisa linahudumia mtu mzima (roho na mwili), na sio roho peke yake.

Ni wajibu wa Kanisa kuwahimiza waumini wachague viongozi bora. Hao ndio watawaendeleza waumini kiuchumi, kielimu na kiafya. Kanisa ambalo linahusika katika utoaji wa Elimu na Afya ni lazima lihusike kuhimiza uchaguzi wa viongozi wanaoweza kuboresha huduma hizo.

Si Tanzania tu ambako Mabaraza ya Maaskofu huhimiza umuhimu wa kuchagua viongozi bora. Uchaguzi wa mara ya kwanza wa Tonny Blair ulisaidiwa sana na jarida la "The Common Good" ambalo lilitolewa na maaskofu katoliki wa huko.

Wanaoogopa waumini kuelimishwa kuhusu kuchagua viongozi bora ni CCM?
 
Nadhani wachangiaji wengi wame miss lengo la Kanisa Katoliki. Lengo lao sio kuwaelimisha wananchi kuhusu haki na namna ya kupiga kura. Lengo lao ni kuwaelimisha WAUMINI haki na namna ya kupiga kura. Waroma wanaamini kuwa Roman Catholic Church is the only true church. Kwa hiyo waumini hasa ni wafuasi wa kanisa katoliki. Ili kuhakikisha kuwa nchi inaendeshwa kwa mwelekeo wa kiumini kwa mujibu wa kanisa lao, basi ni lazima waumini wao wachague viongozi wa nchi kutokana na wao.

Huu ni mkakati wa muda mrefu wa Kanisa Katoliki tangu enzi za Nyerere na ndio maana mpaka sasa hajapatikana Rais mkristo ambaye si Mkatoliki.

Hii habari ya kanisa kufanya juhudi hizo kupinga ufisadi ni upuuzi mtupu kwani kanisa katoliki halina history ya kupinga ufisadi kwani limekuwa na matokeo mengi ya kifisadi na ufuska hasa kwa vijana wadogo wa kiume. Hata hapa hapa kwetu Tanzania mafisadi wamekuwa wachangiaji wakubwa wa kanisa.

Tatizo la sasa lililo sukuma kanisa katoliki kuamsha juhudi hizi ni baada ya kuona kuwa Rais Kikwete anajaribu ku balance uteuzi wa viongozi wa serikali kwa kuteuwa wakristo wa madhehebu zote na waislamu kwa uwiano badala ya kupendelea waroma kama ilivyokuwa huko nyuma. Sasa Kanisa Katoliki linaona limeanza ku loose grip ya utawala ukulinganisha na huko nyuma. Kwa hiyo solution kwa muono wao ni kuwahamasisha WAUMI wao kuchagua WAUMINI wenzao.

Kwa hiyo madhehebu nyingine ya dini nayo yafanye hivyo kama yanaona hiyo ndio solution ya kuendeleza imani zao through kuakamata dola.
 
You tell lies Tk. The Roman Catholic Church does not hold that it is the only true Church. It teaches that it has the fullness of the truth, but it recognizes the existence of varying amounts of truth in other Churches as well. In fact, it teaches that the Orthodox Church is a true Church.

If you have a bone to pick with the Catholic Church, then you should at least inform yourself about its essence first. It is devious of you to simply throw mud at it and hope that some of it will stick.

The Church has remained unscathed by hordes of strong persecutors throughout the centuries. She carries within her a promise, from her founder, that He will be with Her always; unto the consummation of the world!
 
hili ni hatua nzuri sana ambayo kanisa imefanyaa kwani kwa hakika ikitumika vema ni kampeni mwafaka kuelekea taifa endelevu kiuongoziii...

Kanisa lina wajibu mkubwa wa kuelimisha waumini wake kiroho na kimwili ili kufikia maisha bora. na kikwazo kikubwa cha ukosefu wa maisha bora kwa watanzania ni UONGOZI BORA.

Huu ni wakati mwafaka wa kuachana na BORA UONGOZI na KUWA NA UONGOZI BORA.
Ni matumaini yangu kwamba waumini wataitumia vema nafasi hii adimu ya manufaa makubwa katika mustakabali wa maisha yao na taifa letu. Kupitia jumuiya ndogondogo kanisa linatarajia kufikia waumini wake wote nchini kwani miundo mbinu hii imelisaidia kanisa kuimarika siku hadi siku.

nawapongeza maaskofu wa kanisa katoloki kwa maono hayo yenye busara na uzalendo kwa taifa lao.

nawataka wananchi wote wakristu na wasio wakristu kuunga mkonoo juhudiii hizi za ukombozi wa taifa letu kiuongozi..

CHANGE IS COMING TO TANZANIA....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom