Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Kwa nini usisome kwanza na kuelewa hoja niliyokuwa naijibu kuliko kunishambulia au ndivyo ulivyofundishwa kufanya? Kama kusoma ndiko huku, basi ipo kazi!

Huyu sheik ndivyo alivyo ukimpa hoja anarukia nyingine bila kujibu.
Na sishangai maana ndio kawaida yao. Huwa hamna hoja kabisa.
Kulalama tuuuuuuuuuuuuuuu 'tunaonewa, tunaonewa' hapo huwabandui.
Achana naye maana hata kumjibu ni kama kufanya kazi bure. Anahitaji elimu ya madrasa tu ndio size yake.
 
Thanks Brother, very useful message, now I know!
a) Vatican ina wakazi 750! shocked do we need to pay ambassor for this? what do we get in return? (economic gain?) kama una data zitanisaidia sana kubadili mtazamo wangu please!
b)Usilinganishe hata siku moja Iran, Saudia na Vatican (hiyo ni kulinganisha mbingu na Dunia wapi na wapi?
Prove of why waislamu has the point to argue!
i. Vatican ina mission ya "kueneza ukristo tuu" no economic gain as a "state" yaani Tanzania hatupati chochote ni mzigo unaobebwa na nchi kwa faida ya kueneza ukristo! unlike Saudia, Iran and the like ni uhusiano wa kiuchumi kwa faida ya jamii yote bila kujali dini (mafuta ni wote, technology ni wote tunafaidi)
ii. As long as vatican purpose is to "christinize the world population" ni state ambayo ni "kibaguzi" kwa ajili ya wakristo tuu.
iii. Kwakuwa nchi yetu imekubali kuwa na uhusiano na vatican (kama nchi siyo kama kanisa katoliki kama taasisi then logic and justice saves the kukubali kuwa na uhusiano na OIC kwa faida ya wenzao waislamu without any jealuos
iv. Otherwise Tanzania ifute uhusiano na Vatican kama nchi (ila iruhusu kanisa katoliki wajiunge kivyao vyao), otherwise this is precedent tosha kwa waislamu kujiunga na OIC kwa faida yao kama waislamu na kwa nchi kwa ujumla. sioni tatizo ila kuna "Wivu, chuki, na unafiki kwenye dealings among societies which is by no way healthier"
iv. Ni vizuri serikali ikashughulikia haya mambo bila kuonyesha kwamba "always christians make choices for country even for things which are benefiacial to muslims while when it comes to christians muslims never kuingilia"

Aisee, kama hiyo ndiyo shule ni bora ujiendeleze zaidi. Elimu haina mwisho. Kumbe nia yako ni kutaka vatican ifutwe ili Tanzania ijiunge na OIC? Kama mchangiaji mmoja alivyosema kwa nini OIC isilete balozi wake kama Vatican kama shida ni hiyo?
 
a) Toa ushahidi wa nchi ambayo waislamu wanauana? bila kuvamiwa na wakristo na kupeleka crusade zao (religion war) peleka biblia na bunduki
b) Kutojiamini ni kufanya mambo kwa siri (waraka wa kibaguzi) working behind the scenes, walifanya maaskofu huko rwanda walikufa watutsi wengi mbele ya maaskofu (can you deny this fact).
c)Wakristo ndio hawajiamini ina maana wakristo hawana elimu ya uraia mpaka wafundishwe na maaskofu aibu kubwa! (mpaka leo wakristo unamtegemea askofu akufundishe read yourself shame on! hiyo siri ndio kutojiamini kwenyewe
d) waraka uko tunao ila sina soft copy

Nauliza. Hivi wanaouana Somalia ni akina nani?
 
Thanks Brother, very useful message, now I know!
a) Vatican ina wakazi 750! shocked do we need to pay ambassor for this? what do we get in return? (economic gain?) kama una data zitanisaidia sana kubadili mtazamo wangu please!
b)Usilinganishe hata siku moja Iran, Saudia na Vatican (hiyo ni kulinganisha mbingu na Dunia wapi na wapi?
Prove of why waislamu has the point to argue!
i. Vatican ina mission ya "kueneza ukristo tuu" no economic gain as a "state" yaani Tanzania hatupati chochote ni mzigo unaobebwa na nchi kwa faida ya kueneza ukristo! unlike Saudia, Iran and the like ni uhusiano wa kiuchumi kwa faida ya jamii yote bila kujali dini (mafuta ni wote, technology ni wote tunafaidi)
ii. As long as vatican purpose is to "christinize the world population" ni state ambayo ni "kibaguzi" kwa ajili ya wakristo tuu.
iii. Kwakuwa nchi yetu imekubali kuwa na uhusiano na vatican (kama nchi siyo kama kanisa katoliki kama taasisi then logic and justice saves the kukubali kuwa na uhusiano na OIC kwa faida ya wenzao waislamu without any jealuos
iv. Otherwise Tanzania ifute uhusiano na Vatican kama nchi (ila iruhusu kanisa katoliki wajiunge kivyao vyao), otherwise this is precedent tosha kwa waislamu kujiunga na OIC kwa faida yao kama waislamu na kwa nchi kwa ujumla. sioni tatizo ila kuna "Wivu, chuki, na unafiki kwenye dealings among societies which is by no way healthier"
iv. Ni vizuri serikali ikashughulikia haya mambo bila kuonyesha kwamba "always christians make choices for country even for things which are benefiacial to muslims while when it comes to christians muslims never kuingilia"

Ni vichekesho tu. Suala la muundo wa Vatican linatuhusu nini watanzania? Suala la muundo wa nchi tunazohusiana linatuhusu nini? Ni nchi gani ambayo tuna-uhusiano nayo halafu tuanawaambia muundo wao uwe hivi au vile.

Huu ni wivu usio na msingi. Balozi wa Vatican halipwi na watanzania na yupo Tanzania kwa gharama za Vatican.

Vatican ni organization yenye State face. Tanzania ina uhusiano ni ile state face. Full stop. Uhusiano huo una sura zile zile za mahusiano na state nyinginezo na hakuna cha ziada. Tanzania is not a member in any Vatican related organization and cannot be.

Watanzania (wakatoliki) kupitia kanisa lao wana mahusiano na Vatican. Mahusiano ya Vatican na wakatoliki hayahusishi serikali. Yanahusisha kanisa lao na mahusiano hayo hayana uhusiano na haya ya kiserikali. Serikali inaweza kumfukuza balozi wa Vatican nchini kama inavyoweza kumfukuza balozi yeyote nchini ikiwa kuna kutoelewana kati ya nchi. Ikiwa atajihusisha na mambo yaliyo kinyume na shughuli za kibalozi serikali inaweza kumfukuza.

Lakini serikali haiwezi kuwazuia wakatoliki kuhusiana na Vatican. Wakatoliki wa Tanzania hawahusiani na Vatican kupitia Balozi wa Vatican wala kupitia serikalini. Awepo balozi au asiwepo wakatoliki wa Tanzania wataendelea kuhusiana na Vatican. Pengine hili ndo halieleweki.
 
Na ikiwa waislam watajiunga na OIC bila kuhusisha serikali, hakuna shida. Kwa mfano Bakwata au organization nyingine yoyote ya kiislam iende kujiunga OIC sina shida na hilo. OIC inaweza kuleta envoy wao hapa Tanzania na akafanya kazi na serikali bila mgogoro.

Shida ni pale tunapoitaka serikali ijiunge OIC kwa kuridhia katiba ya OIC ambayo imeshasomwa hapa. Kuridhia katiba ya OIC kutaifanya katiba hiyo iwe binding kwa watanzania wote kama zilivyo binding sheria nyingine zote za kimataifa ambazo Tanzania imeridhia.

Sasa kama mtu haoni shida hapo, nadhani inabidi ajifunze zaidi.
 
Nziku,

Ahali yangu sio vizuri kutoa lugha mbaya kwa wengine kwani kila mtu ana haki sawa katika kutoa maoni na wewe kama una hoja basi jaribu kutafuta hoja na kujibu hoja kuliko kutumia lugha ya kukera au dhihaki kwa wengine.

Nafikiri msingi mkuu ni huu kama ulivyobainisha wee mwenyewe ' 'no research no right to speak'.

Sasa usikurupuke kutoa hoja bila kufana tafiti. Sasa soma gazeti la leo la RAIA MWEMA utakiona kijitabu hicho picha yake ni kisha kitafute kwenye bookshop ( mimi nimemwagiza mtu aninunulie huko Dar kipo Cathedral bookshop pale opp forodhani sec ,posta.

Elewa kuwa ndio maana Hata spika hakuhitaji kuthibitisha kani kitabu bila shaka kitakua kimeeleza mengi.

Sasa labda nije na suala dogo tu kwako. Hivi kwanini waislamu haana miradi mingi ya kijamii kama shule, hospitali, na vyuo vikuu? Kwanini wawe wakristu kwa kila kitu? hebu fanya utafiti kidogo.

Labda kwa kukusaidia kwanini SM Tanzania haitaki kuwaruhusu waislamu waingie katika OIC?

Ukiangalia na kutafiti kidogo utaona Roman Cath ndio wenye miradi mikubwa a kijamii na ndio wanaopata ruzuku na misamaha mikubwa ya kodi.
Je unajuwa kwanini balozi wa Vatican yupo TZ, anamwakilisha nani? na yupo kwa maslahi ya nani?

naomba ufikirie hayo kisha uje na hoja na wala sio kejeli.

Dr Hamza



'
Katika maandishi mekundu ndugu ni kwamba kuwa na miradi mikubwa au midogo ni juu ya mhusika kuamua. Mashirika yote ya dini yanapat misamaha ya kodi iwe ni waislamu, wahindu, wakristu etc suala hapo ni kuwa madhehebu yanajihusisha na taasisi za kutoa huduma kwa kiasi gani?. Hakuna aliyezuiliwa kufungua mashule, mahospitali,Youthh & training centres etc milango iko wazi. nadhani ni wakati muafaka sasa wale wote aidha christians au waislamu au wahindu Nk kufungua taasisi hizi kwa wingi ili kufaidika na ruzuku hizo na katika kufanya hivyo jamii itanufaika zaidi kuliko kukaa tunatoleana maneno makali ambayo hayajengi bali kuondoa umoja wetu.
Katika maandishi ya bluu. nawe hujawahi kujiuliza kuwa ni kwa nini balozi wa Irani yupo hapa nchini na anamwakilisha nani na kwa maslahi ya nani? Irani ni nchi ya kiislamu kama ilivyo Vatican ni nchi ya kikristo. Vatican ni nchi kamili yenye utawala na mawaziri wake kama nchi nyingine yoyote.
 
Nguvu ya kweli ya kutawala mazingira inaletwa na sala yenye unyenyekevu kwa mungu na elimu yenye kutupa uwezo wa kupambanua mambo. Kama hatutaki kusoma, kuheshimu watu wengine, kuchukia udhalimu hii mbinu ya kutokea kwenye mgongo wa udini liyoitumia mbunge haitampeleka popote. Tanzania imejaa watu wa dini zote na tusidanganyane kuwa kuna dini ina nguvu kuliko nyingine kwa kupeka hoja zake kwa jazba. Jamani, sisi ni ndugu. Tuachane na wanasiasa wanaoleta mambo ambayo hawana utafiti nayo. Mjadala ungekuwa na hoja kama ile document ya kanisa ingeonyesha kuwa wakristu wawapigie kura wakristu tu.Ni juavyo mimi, maaskofu sio wajinga kiasi hicho cha kuandaa waraka ambao utawachoma mikono mbeleni kwa kuleta dhana za kibaguzi. Trust me they are smart!!
Kupigna nao na kushinda kwa jazba hatutaweza.Tulete hoja. Kanisa lipo kila sehemu mpaka sehem ambazo watu hawana njia za kupita ila ni kwa baiskeli tu na wanaconnection na askofu wao. Don't underestimate this power, which comes of learning kwa hoja za jazba. Lengo walilolikusidia linaenda kisomi na litafanikiwa. Dawa ya watu wengine ni kujibu kisomi pia ili kuwapa changamoto ya kweli kanisa.Tuachane na huyu mbunge mufilisi
 
Na ikiwa waislam watajiunga na OIC bila kuhusisha serikali, hakuna shida. Kwa mfano Bakwata au organization nyingine yoyote ya kiislam iende kujiunga OIC sina shida na hilo. OIC inaweza kuleta envoy wao hapa Tanzania na akafanya kazi na serikali bila mgogoro.

Shida ni pale tunapoitaka serikali ijiunge OIC kwa kuridhia katiba ya OIC ambayo imeshasomwa hapa. Kuridhia katiba ya OIC kutaifanya katiba hiyo iwe binding kwa watanzania wote kama zilivyo binding sheria nyingine zote za kimataifa ambazo Tanzania imeridhia.

Sasa kama mtu haoni shida hapo, nadhani inabidi ajifunze zaidi.


BInafsi hilo ndo lina nishangaza!

Kama wenzetu waislam wanapenda kujiunga na OIC, kwani shida iko wapi? wao si wajiunge tu kupitia jumuia zao? sidhani kama kuna mtu atawazuia.

Mahakama ya Kadhi, ni nzuri sana kulingana na imani yao, kwanini wasijipange wakaianzisha wao wenyewe kwa faida yao?, sidhani kama serikali itawakatalia kufanya hivo.

Ninapo shangaa, kwanini mambo haya wanatamani yaingie katika katiba ambayo ina husu watu wote hata wasio wa imani hiyo?

Bibafsi nawatakia heri kabisa wafanikiwe katika hayo mahitaji yao lakini si kuyaingiza katika katiba, kwani katiba ni ya watu wote hata wasio husika na imani hiyo.

 
Je unafahamu Vatican ina status ya nchi kama ilivyo Iran au Saudi Arabia? Na hao wenye jamuhuri za kiislamu balozi zao ni za nini TZ?
Jamani tusipoteze malengo kwenye suala hili. Kwa mfano, mi nimekutana na waislamu wengi ambao kwa matendo yao ninawaheshimu kama waungwana na marafiki zangu.
Tuwe wakweli. Maendeleo ya nchi yetu hayana mjomba wa kuyasaidia. Kanisa na misikiti ina uhuru sawa wa kuanzisha huduma za kijamii. Tutafanya makosa makubwa kuamua kuziba macho tusione mambo yaliyo wazi na kuleta hoja kama hii ya kuwa na balozi wa Vatican Tanzania iwe kama nalo ni kosa. Unless unihabarishe wewe unajua balozi wa Vatican anafanya kazi gani TZ tofauti na ile iliyokusudiwa ntakuelewa.

Ndugu Ndahani,huyo ndugu kumjuza itakuwa ngumu sana,sikutegemea kama hajui kuwa Vatican ina status ya nchi kama zilivyo nchi nyingine!!
Dokta vipi bwana unatuangusha na status yako ya U-'dokta'.Bora kwanza ungecheza na google,mana majibu yote ungepata kuhusu Vatican,lol...
Jamani tusiwe wavivu kucheza na google kuliko kukurupuka na kuandika.Bora kama ungekuwa huna uhakika ungeuliza humuhumu JF watu wangekuelimisha free of charge dokta!
Vatican ina status ya nchi ndo mana ina balozi hapa Tz.
 
Wabunge wetu wengi sio wasomaji wazuri. Msambya shida yake kubwa ni kwa nini waraka huu utolewe na MAASKOFU. Hana na wala hakuonyesha nia kuyashambulia yaliyoandikwa mle. Waraka ule ungeandikwa na TAMWA, REDET au NGO yoyote mbali na MAASKOFU, Msambya asingehangaika nao.
Hilo moja, la pili tusisahau wanasiasa wanapokuwa wamefilisika kisiasa na mambo yanaelekea kuwaendea kombo ( hasa hawa wa kuchaguliwa) watatafuna njia yoyote ile kujihalalisha upya kwa wapiga kura wao ikiwemo DINI, KABILA, JINSIA, PESA,...
 
Siri nzito ilani ya Kanisa Katoliki

Na Mwandishi wa Raia Mwema​
Julai 1, 2009

bul2.gif
Yahoji mamlaka ya Rais kuteua mawaziri
bul2.gif
Yapendekeza wagombea binafsi isipokuwa urais

WAKATI Ilani ya Uchaguzi ya Kanisa Katoliki ikitoa vipaumbele na mwongozo wa mtu binafsi kuchagua chama na mgombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa 2010, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), nalo linaandaa tamko la kuwaandaa waumini kuwawajibisha watawala, imefahamika.

Kiongozi mmoja mwandamizi wa KKKT, amelithibitishia Raia Mwema wiki hii kwamba tayari vyombo vya juu, Baraza la Maaskofu na Halmashauri Kuu ya Kanisa hilo, kwa pamoja vimeridhia uandaaji wa tamko hilo zito litakalolenga chaguzi za viongozi wa dola katika ngazi ya Serikali za Mitaa 2009 na Serikali kuu 2010.

“KKKT nao wako katika mkakati wa kuandaa tamko lenye sura ya kuwaelekeza waumini wake kuamka na kuwawajibisha watawala katika kila ngazi, tangu vitongoji hadi Taifa. Wanasema kwamba wanazuoni maarufu wa vyuo vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi, wanadiplomasia na wanaharakati wanashiriki katika kukusanya takwimu,” kinaeleza chanzo chetu cha habari kilicho karibu na maandalizi ya tamko hilo.

Hayo yakijiri, Waislamu nao wameelezwa kujipanga ili kuhakikisha kuwa Rais, wabunge na madiwani hawachaguliwi kwa misingi ya kidini, uamuzi ambao umeelezwa kwamba umekuja baada ya mipango ya makanisa kuandikwa katika magazeti hivi karibuni.

Wanazuoni wa Kiislamu pamoja na mashekhe 15 wameunda jopo ambalo pamoja na mambo mengine, litaratibu na kusimamia mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu ujao kwa maslahi ya Waislamu.

Jopo hilo lililozinduliwa katika hoteli ya Starlight, hivi karibuni, linaongozwa na Sheikh Mohamed Idd, ambaye alinukuriwa akikemea ubaguzi wa kidini katika masuala yote ya uchaguzi.

Tayari uongozi wa juu wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, umeelezea masikitiko yake kwa jinsi viongozi wa dini zote wanavyouangalia kwa mtazamo hasi utawala wa sasa, ikiwa ni pamoja na viongozi na waumini wa Kikiristo kuhisi kwamba uongozi wa sasa unapendelea Waislamu huku kwa upande wao Waislamu wakiona kiongozi wa kutoka dini yao haonyeshi kuwasaidia. Kauli hiyo imetolewa hadharani mwishoni mwa wiki.

Katika vijitabu vya “Ilani, Mapendekezo ya Vipaumbele vya Kitaifa” ya Kanisa Katoliki pamoja na “Mada za Kuongoza Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2010”, maandiko ambayo yameandaliwa kitaalamu na ‘Wanataaluma Wakristo Tanzania (CPT), kwa baraka zote za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), waumini wamepewa miongozo ya kufahamu vipaumbele vyao kabla ya kushiriki chaguzi zilizo mbele yao.

Sehemu kubwa ya nyaraka hizo za Kanisa Katoliki, mmoja utakaochapishwa katika toleo lijalo la Raia Mwema, zinakosoa maeneo karibu yote ya Serikali ikitoa vipaumbele vikiwa na mapendekezo ya jinsi ya kuboresha maisha ya Watanzania katika sekta zote muhimu ikiwa ni pamoja na sheria na haki za binadamu; uchumi; elimu; afya na ajira.

“Kwa sababu chaguzi za mwaka 2010 haziko mbali tunaona ni muhimu kupendekeza vipaumbele vyetu kama jamii tukiwaambia viongozi wetu wajao yale ambayo tungependa yafanyike kwa ajili ya jamii yetu. Katika uchaguzi hatupigi kura tu, tunapaswa kueleza makusudio yetu kwa yale tunayofikiri kuwa muhimu kwa Taifa,” inaeleza sehemu ya utangulizi wa Ilani ya Kanisa Katoliki, ulioandikwa na Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani, Askofu Mkuu wa Tabora, Paul Ruzoka.

Kwa umakini mkubwa, Ilani hiyo ya Katoliki imekuwa ikisisitiza kuwaelekeza Watanzania wote na si waumini wao pekee ambao wametajwa kama walengwa wakuu wa waraka huo kutokana na wote kuguswa na mambo yatakayofanywa na viongozi.

“Tunatoa mwaliko kwa wote na kuwasihi Watanzania wote kufikiri kwa makini changamoto kuu zinazokabili nchi yetu na wananchi wake wengi ambao ni masikini wa mali, waliotengwa na wasio na uwezo. Kuzishughulikia changamoto hizi kunahitaji kuweka vipaumbele sahihi na njia sahihi za ufumbuzi ambazo zinashughulikia kikamilifu matatizo ya umasikini, utenganisho wa kijamii na hali ya kukosa uwezo kwa Watanzania wengi,” inaeleza sehemu ya maelezo ya ‘madhumuni/lengo la Ilani na kuendelea.
Katika kuonyesha kwamba lengo si kuelekeza chama ama mtu maalumu, madhumuni ya Ilani hiyo yanaeleza kwamba itakuwa “mwongozo kwa mtu binafsi kuchagua chama na mgombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2009 na Uchaguzi Mkuu wa 2010.”

Pamoja na kuzungumzia haja ya kuifanyia marekebisho Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ilani hiyo imeweka suala la ‘hadhi ya utu wa binadamu’ kama kipaumbele cha kwanza, ikisisitiza kuwapo kanuni za kimaadili na weledi (meritocracy) katika vigezo au sifa za kuwapa watu kazi na kupandishwa vyeo. Kigezo hicho kinaashiria kuwapo malalamiko ya upendeleo katika ajira na utoaji nafasi za ajira na uongozi.

“Pana haja ya kuunda Baraza la Mapitio ya Katiba. Katika mifumo mbalimbali ya kisiasa, kuna njia kadhaa za kuwezesha suala kutekelezwa; Mahakama ya Kikatiba, chamba ya pili katika Bunge na Mkutano wa Katiba.
Tunapendekeza paundwe Baraza la Wazee wanaoteuliwa na sekta ya kijamii, ama wanaochaguliwa na taasisi mbalimbali za kijamii, kidini na wanazuoni. Chombo hiki kingechaguliwa na kuhakikishiwa uhuru watendaji wake kulingana na katiba yenyewe. Kisibanwe na Serikali,” inaeleza.

Kutokana na matukio ya matumizi makubwa ya fedha katika chaguzi, Ilani hiyo imependekeza kuwapo kwa kanuni za marekebisho na udhibiti na kuwezesha uwazi wa kisheria kuhusiana na upatikanaji wa fedha za chama ama wagombea pamoja na kupendekeza kuwapo kwa kanuni za udhibiti na marekebisho katika kuchagua wagombea kutoka ndani ya vyama kwa lengo la kusaidia mchakato mzima wa kidemokrasia.

Pendekezo lingine la kikatiba lililoguswa na Ilani hiyo ya Katoliki ni pamoja na pendekezo la kutaka kuwapo kwa wagombea binafsi katika ngazi zote isipokuwa ile ya urais na kuikumbusha Serikali, “kuheshimu kanuni ya kuwa Serikali haina dini na kutoruhusu taasisi za kidini kuwa sehemu ya mfumo wa nchi ikitoa mfano wa suala la la Mahakama ya Kadhi na uanachama wa OIC.

Kutokana na kukithiri kwa matukio ya kifisadi, Kanisa Katoliki katika Ilani hiyo limependekeza kuwapo uwazi katika uteuzi na kufanyika kwa mapitio ya “mamlaka ya Rais katika kuwateua mawaziri, idadi ya wizara, na pia uwezo na uhuru zaidi wa bodi za usimamizi wa mashirika ya huduma za umma,” na kuwapo kanuni na taratibu za uongozi za kuondoa wale wanaothibitika kutumia vibaya nafasi zao.

Maeneo mengine yaliyoguswa kwa kina, sehemu kubwa ikiwa ni kukosoa mfumo wa sasa ni pamoja na mfumo wa kisheria; viwanda, biashara na fedha; uchumi; elimu; afya; ajira na hifadhi ya jamii, huku ikitoa mapendekezo mbadala yenye lengo la kuhakikisha wananchi wengi zaidi wananufaika na nchi kupiga hatua kubwa zaidi kimaendeleo.

Habari zinasema vijitabu hivyo vya Kanisa Katoliki vimesambazwa nchi nzima na kuuzwa kwa bei nafuu na hata kugawanywa bure kwa watu wote wakiwamo waumini wa dini nyingine, lakini vimeibua mjadala mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwamo waumini wa madhehebu mengine, huku baadhi ya watu wakitafsiri kwamba Kanisa Katoliki linalenga kusaidia watu maalumu kuingia madarakani.

Hata hivyo, uongozi wa Kanisa hilo ukiongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ulitoa ufafanuzi kwamba kanisa hilo linatimiza wajibu wake wa kitume wa kuwaelimisha waumini wake na Watanzania wengine kuhusu haki zao na si kutaka kumsimika mtu ama kumwangusha kiongozi yeyote.

Kauli ya Kardinali Pengo na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini kuhusiana na suala hilo ilitafsiriwa kwa namna tofauti na baadhi ya vyombo vya habari, chombo kimoja kikieleza kwamba sasa kanisa hilo linajipanga kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, katika kampeni za uchaguzi mkuu ujao wa 2010, tafsiri ambayo nayo imepingwa na viongozi wengi wa kanisa hilo wakisema hawataelekeza mtu bali wanachofanya ni kutoa elimu ili uamuzi uwe ni wa wananchi wenyewe.

Jana Jumanne tukienda mtamboni suala hilo liliingia bungeni kupitia kwa Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM) Manju Salum Msambya, aliyerejea waraka huo akitaka Serikali kutoa tamko akisema unalenga kuwaelekeza waumini wao kuchagua viongozi maalumu ambao unaweza kuwafanya waumini hao kuchagua viongozi kutoka dini yao pekee.

“Tusiifikishe nchi pabaya. Ukitoa waraka wa kichungaji unatoa sababu ya waumini kujielekeza kuchagua muumini mwenzao. Ni hao hao waliowahi kusema kwamba tusichanganye dini na siasa, leo hii wao ndio wanaofanya siasa. Kuna waziri mmoja wa serikali hii hii ya CCM ambaye aliunga mkono waraka huo. Nchi hii ni yetu sote, hakuna mwenye hati miliki hata Rais wa nchi,” alisema Msambya akichangia bajeti ya Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba.



Source:
Gazeti la Raia Mwema
 
Wenye soft copy ya kitabu tunawaomba watuwekee

5161d1246544359-siri-nzito-ilani-ya-kanisa-katoliki-ilani_kanisa.jpg
 

Attachments

  • ILANI_KANISA.jpg
    ILANI_KANISA.jpg
    14.7 KB · Views: 648
Haya yote yanaweza kuchangiwa na Serikali yenyewe ikiongozwa na Mzee wetu wa Kaya, sasa itakuwa ni vurugu sana
 
Na wewe Halisi acha udini, hiyo "siri nzito" ipo wapi? wakati content ya habari inaonyesha waraka umesambazwa, unauzwa na kugawiwa bure!

Umeileta habari kishabiki shabiki na ki udini udini shame on you!
 
Hii mikakati ya kanisa sasa inajitokeza ,ninavyowasoma wakatoliki wanakasumba mbaya sana ,kuwa hapa duniani ni wao tu na wanao uhuru wa kumuua yeyote yule ambae si mkatoliki,ukisoma kitamu cha mauaji ya Mwembe Chai utaona mwandishi ni jinsi gani ameweza kuonyesha msimamo wa wakatoliki na makanisa mingine ,inaonyesha wakifanikiwa kuwaweka pembeni Waislamu watawageukia wenzao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom