Wapinzani wakumbusheni Watanzania madhara ya wabunge wa CCM yakiwemo kubariki (makato makubwa ya Bodi ya Mikopo, kuunganisha Mifuko, kikokotoo kipya)

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Wapinzani na wadau wengine kwa ujumla,wakati tunaelekea katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa Raisi wabunge na madiwani,ni vyema mkawakumbusha watanzania madhara ya kuwa na wabunge wengi wa CCM Bungeni hasa ikitokea CCM inaridu tena madarakani

Watanzania(baadhi yetu) tunakuwa wapesi sana wa kusahau na tunadhani kigezo cha kuchagua mtu ni umaarufu au nafasi aliyonayo katika jamii au elimu yake na hiki sasa ndio kinatakuwa mjadala katika mitandao na media tunasahau kabisa mwenendo wa wabunge wa CCM wawapo Bungeni

Hivyo,Wapinzani,waambieni na wakumbusheni watanzania angali mapema kuwa wabunge wa CCM wawapo Bungeni siku zote huwa ni kupitisha mambo yanayoletwa na serikali yao hata kama yanaumiza wananchi; hivyo, wasichague wabunge wa hiki chama kisa tu mgombea ni Doctor, Professor, mwanamuziki, tajiri, mchungaji, n.k.

Waambieni watanzania,ni wabunge hawa hawa wa CCM (baadhi yao wakiwa madokta, maprofesa, matajiri n.k), ndio walipitisha sheria mbaya inayomkata mlalahoi wa nchi hii asilimia 15 ya mshahara wake kulipia makato ya Bodi ya Mikopo.

Wakumbusheni watanzania kuwa, ni wabunge hawa hawa wa CCM waliopitisha sheria iliyounganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kubadili kanuni ya kukokotoa mafao ya wastaafu bila kujali athari zake kwa wastaafu na wastaafu watarajiwa.

Wakumbusheni watanzania kuwa,ni Bunge hili hili lililokuwa na wabunge wengi wa CCM lilituhumiwa na CAG aliepita kwa udhaifu wa kushindwa kutekeleza baadhi ya majukumu yake ya kuisimamia na kuishauri serikali.

Wakumbusheni watanzania kuwa ni Bunge hili lililokuwa na wabunge wengi wa CCM lilishindwa kuunda kamati teule kuchunguza matukio ya watu kutekwa na wengine kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Waelezeni watanzania ni Bunge hili la CCM lilishindwa kuunda kamati teule hata moja kuchunguza tuhuma zinazoikabili serikali kama ile ya matumizi yasioeleweka ya shilingi trilioni 1.5,mchakato wa Passport za kieletoniki na mambo mengineyo yaliyoibuka awamu hii.

Hatari ya kubadili katiba kuongeza muda wa Raisi kukaa madarakani
Wote ni mashahidi wa baadhi ya kauli za wabunge wa CCM kutaka kumuongezea Raisi muda wa kukaa madarakani; hivyo, muwaonye watanzania wakati wa kampeni kuwa wakirudisha wabunge wengi wa CCM, kuna hatari ya wao kwenda kukamilisha azima yao hiyo na hii itatugharimu wote bila kujali vyama na itikadi zetu.

Hivyo,Wapinzani,hata leo hii mkipata fursa ya kuongea na media za kimataifa na za humu ndani,tumieni fursa hizo kueleza madhara ya Bunge lililopita na mtumie mifano ya sheria kama za makato ya Bodi ya Mikopo kujenga hoja na kuwaeleza wananchi juu ya athari za kuchagua tena wabunge wa CCM hata kama ni wanamuziki maarufu,wasanii maarufu, wasomi, n.k.

Last but not least, kumbusheni na ile kauli ya mwenyekiti wao iliyolenga kuwaziba midomo kwa kutishia kupiga hata mashangazi zao ili wananchi wajue tu kuwa hata wakichagua mbunge mwenye status gani katika jamii, bado anaweza asiwe huru katika kazi yake kutokana na vitisho vya mwenyekiti wa chama chao ambae ameonyesha kuwashangaa wabunge wachache wa CCM wanaopinga mambo ya Serikali Bungeni.
 
Back
Top Bottom