The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,503
- 2,046
Wanabodi naomba mnisaidie kuelewa shida iko wapi, maana tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini, tumeshuhudia vyama tofautitofauti vya upinzani vikiibuka na kujipatia wafuasi wengi na hivyo na hivyo kuwa tishio kwa chama tawala.
Kwa kumbukumbu zangu ni kwamba ilianza nccr mageuzi ilipata umaarufu mkubwa sana siku za mrema na kutoa ushindani mkali sana kwa ccm hasa kwenye uchaguzi wa 1995.
Baada ya hapo ulizuka mgogoro mkubwa sana ndani ya chama hicho ambapo viongozi wakuu waliishia kuvurugana na kufukuzana na kukiumiza sana chama na kukiondoa kwenye ramani ya siasa za ushindani.
Ndipo ikafuata zamu ya cuf chini ya prof Lipumba na Maalim Seif, kama ilivyokua kwa nccr ingawa kwa huku bara cuf haikufikia ile nguvu ya nccr ya Mrema lakini taratibu ilianza mizozo ya ndani ambayo nayo haikuiacha CUF salama.
Kilele cha CUF kuvurugana tulikishuhudia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo mambo yaliyotokea yameifanya cuf isiaminike tena. Maana viongozi wakuu walivurugana na kufukuzana.
Kwa upande wa chadema ingawa walikuwa na nguvu za waziwazi tangia 2010, lakini pia wao hawakuwa na kinga dhidi ya hii changamoto ya kuvurugana maana tulishuhudia baada ya kumpokea lowasa chamani katibu mkuu alisusa na baada ya hapo tumeshuhudia matukio mengi ya fukuzafukuza ndani ya chama.
Ila kinachonishangaza ni kwamba ccm ina wanachama wengi sana, na mara kadhaa wamekua wakitifautiana kauli na mitazamo hata hivyo wao huitana kuombana msamaha na makaripio na maisha kuendelea.
Ni kwa nini wapinzani ni ngumu kumaliza tofauti zao kwa kusameheana na kuruhusu maisha yaendelee!?