Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,305
- 33,924
Imezuka hoja hapa JF kwamba CCM kuendelea kwake kuwa madarakani ni kwa sababu Tanzania tuna vyama vya upinzani dhaifu. inawezekana hoja hiyo ina ukweli fulani ndani yake lakini lazima wanaouona upinzani ni dhaifu watoe maoni yao ni nini kifanyike ili CCM ing'oke madarakani Tanzania ikibaki salama.
Wengine hatuuoni uimara wa CCM bali tunaona mabavu ya CCM kutumia dola dhidi ya vyama vingine vya siasa. Leo hoja kubwa kwamba upinzani ni dhaifu ni madai kwamba wameiacha hoja "yao" ya ufisadi.
Lakini ni kweli kuwa Upinzani wameacha hoja yao ya kupiga vita ufisadi? Hivi kuna tofauti gani ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya Lugumi kama ilivyokuwa kwa EPA ama Tegeta Escrow? Wakati ajenda ya wapinzani ilipokuwa kupiga vita ufisadi, CCM walifanya nini tofauti na sasa?
Lowassa aliitwa fisadi Pale Mwembe Yanga kwa kuvunja mkataba kati ya City waters na Dawasa, leo wapinzani wakizungumizia kuhusu Bombadier, ujenzi wa uwanja wa ndege Chato, matumizi nje ya bajeti,kukopa fedha kinyemela inaonekana hawazungumzii ufisadi, ni kwa nini?