Kwa sababu gani unatoa hoja yako hii?
Kifyatu si kwamba hoja yako haina mantiki, hapana. Ila mimi kutokana na uzowefu wangu wa zaidi ya miaka 29 kwenye siasa, kule "field" propaganda zinazotumiwa na CCM huwa kali sana na kwenye zama hizi za utandawazi basi ndiyo inakuwa shida sana!
Hapa Iringa kuna uchaguzi kuna uchaguzi kwenye kata ya Kitwilu. CCM wanazunguka hapa mjini na kuwaambia wapiga kura wa kata hiyo wamchague mgombea wao (Aliyekuwa diwani kupitia CHADEMA kabla ya kujiunga CCM) kwa kuwa wakimchagua atakuwa anawasiliana moja kwa moja na Rais Magufuli.
Sasa ndiyo mnaingia kwenye uchaguzi bila ya kuwa na mgombea Urais ndiyo inakuwa balaa. Ila ukisema mfumo wa kumpata mgombea urais ndani ya CHADEMA unatakiwa ubadilishwe, hilo nalikubali kwa asilimia mia moja (100%)