Wapinzani wafanye nini ili kuing'oa CCM?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
17,871
33,236
Imezuka hoja hapa JF kwamba CCM kuendelea kwake kuwa madarakani ni kwa sababu Tanzania tuna vyama vya upinzani dhaifu. inawezekana hoja hiyo ina ukweli fulani ndani yake lakini lazima wanaouona upinzani ni dhaifu watoe maoni yao ni nini kifanyike ili CCM ing'oke madarakani Tanzania ikibaki salama.

Wengine hatuuoni uimara wa CCM bali tunaona mabavu ya CCM kutumia dola dhidi ya vyama vingine vya siasa. Leo hoja kubwa kwamba upinzani ni dhaifu ni madai kwamba wameiacha hoja "yao" ya ufisadi.

Lakini ni kweli kuwa Upinzani wameacha hoja yao ya kupiga vita ufisadi? Hivi kuna tofauti gani ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya Lugumi kama ilivyokuwa kwa EPA ama Tegeta Escrow? Wakati ajenda ya wapinzani ilipokuwa kupiga vita ufisadi, CCM walifanya nini tofauti na sasa?

Lowassa aliitwa fisadi Pale Mwembe Yanga kwa kuvunja mkataba kati ya City waters na Dawasa, leo wapinzani wakizungumizia kuhusu Bombadier, ujenzi wa uwanja wa ndege Chato, matumizi nje ya bajeti,kukopa fedha kinyemela inaonekana hawazungumzii ufisadi, ni kwa nini?
 
Watanzania kwa ujumla wanahitaji maendeleo basi, hawajali yanaletwa na CDM,CCM,CUF etc, hii kukaa mnahubiri u Chadema na U CCM ndo unaowarudisha nyuma, kama Chadema itaendelea kuongelea udikteta na kukosoa hotuba za Raisi, wasahau kuongoza nchi hii labda 2080 kizazi kijacho, sio hiki cha kubadili gia angani. Halafu muache kukaribisha mafisadi mliotuaminisha mna ushahidi na ufisadi wao na kuwapa sifa na vyeo. Dhambi ya kumuweka Lowassa mgombea 2015 itawatafuna miaka 40 ijayo.
 
kwakweli.

#nakwenda_zimbabwe
 
Hayo umesema wanayotakiwa kuachana nayo, sema MAPYA YANAYOTAKIWA KUFANYWA.
 
Imezuka hoja hapa JF kwamba CCM kuendelea kwake kuwa madarakani ni kwa sababu Tanzania tuna vyama vya upinzani dhaifu. inawezekana hoja hiyo ina ukweli fulani ndani yake lakini lazima wanaouona upinzani ni dhaifu watoe maoni yao ni nini kifanyike ili CCM ing'oke madarakani Tanzania ikibaki salama.

Lowassa aliitwa fisadi Pale Mwembe Yanga kwa kuvunja mkataba kati ya City waters na Dawasa, leo wapinzani wakizungumizia kuhusu Bombadier, ujenzi wa uwanja wa ndege Chato, matumizi nje ya bajeti,kukopa fedha kinyemela inaonekana hawazungumzii ufisadi, ni kwa nini?

Hapa ndio wapinzani mliopokosea.Lowasa aliitwa Fisadi kwa kuwa na maslahi binafsi dhidi ya kampuni ya kufua Umeme ya Richmond. Baada ya kumsakama miaka yote then Mkampa nafasi agombee uraisi kupitia CHADEMA. Mkiendelea kumkumbatia huyo mtu Ikulu mtaiona kwenye TV tuu.
 
Ili kuweza kuing'oa CCM madarakani inabidi wapinzani mfanye yafuatayo 1.kuwa na viongozi ambao sio waroho wa madaraka ndani ya chama 2.kusiwe na viongozi ambao wapo kwa ajili ya masilahi binafsi ndani ya chama 3.inabidi muaandae katiba bora pamoja na kuwa na ilani ya kwenu 4.inabidi muwe na mfuko kwa ajili ya kutatua matatizo kwa watu ambao mnatamani siku moja kuwatumikia kabla hata ya kuwa madarakani 5.muwe na viongozi ambao kidogo wamesoma kwa Elimu ya maendeleo ndani ya chama na nje pia 6.msipokee viongozi wenye kashfa ya ufisadi au ulanguzi wa Mali za umma kabla ya kuingia ndani ya chama chenu...... But all is according to me sikuforce kunielewaaaaaa
 
majibu ya kukata tamaa hayo
Hatuwezi kufumbatia maji kama jiwe Mkuu, kuliko kuwepo watu wanapinga kila kitu no bora tubaki CCM wenyewe tu-focus kwenye ujenzi wa taifa, upinzani unatupotezea time, energy and money included.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom