Waberoya nashukuru kwa kutoa ushauri mzuri sana. Badala ya kurusha vijembe ni kheri kutoa mawazo hata kama tutatofautiana na mawazo hayo.
Nianze na la Lowassa. Mimi kwa mtazamo wangu kila siku ni kwamba Lowassa si tatizo bali tatizo ni CHADEMA. Kuna hoja aliitoa Dr. Slaa kwamba kabla ya kujiunga na CHADEMA ni lazima kwanza Lowassa atangaze hadharani kwamba yeye si mhusika na kashifa ya Richmond. CHADEMA wakapuuzia.
Haiwezekani mtu ambaye kila siku mlikuwa mnamwita majina mabaya ya kila aina ghafla tu bila ya maelezo mnapokea na kumfanya mgombea wenu bila hata ya kutoa maelezo ni nini kimewafanya kubadilika kwa kiasi hicho.
Ndiyo maana "marafiki" wa Dr. Slaa kina
Mzee Mwanakijiji na
idawa wanawananga kila siku CHADEMA kwa upuuzi huo walioufanya. Hawajajibu hoja kama walipokuwa wanasema wana "ushahidi" walikuwa wanamaanisha nini ama walikuwa wanatumia uongo kujipatia ufuasi tu?
Leo mtu anajiuliza ni kwa nini Msigwa, Lema, Mnyika na hata Mbowe ambao walikuwa wanawaaminisha watanzania kuwa Lowassa ni mtu "Mbaya sana", wanatakaje watanzania wamchague mtu mbaya kuwa Rais wao?
Sasa mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba Lowassa alihusika na ufisadi wowote ule kwenye Richmond, lakini itakuwa ngumu sana kuwaamini viongozi wa CHADEMA wanaposema kwamba Lowassa anafaa kuwa Rais. Viongozi wa CHADEMA hawana nguvu ya kimaadili (Moral Authority) kumnadi Lowassa bila ya kwanza kuwaeleza watanzania ni kwa nini walikuwa wanamsema ni mtu mbaya kiasi kile?
Kuhusu Sera na ujenzi wa chama nadhani kuna matatizo mawili makubwa. Kwanza ni wana CHADEMA kutaka kumlinganisha Vincent Mashinji na Slaa. Mungu kampa kila mtu kipawa chake kwa ivo haiwezekani tukafanana. Mashinji anapata wakati mgumu sana kuiunganisha hii CHADEMA "mpya".
Jambo la pili ni CHADEMA kushughulika na Lowassa wakiwa wamemakinika. Lowassa alijitengeneza kama taasisi na alipokwenda CHADEMA alikwenda kama taasisi. CHADEMA wanatakiwa kumlazimisha Lowassa asiwe taasisi ndani ya taasisi.
Kuingia kwa Lowassa kulileta taharuki na fadhaa kwa baadhi watendaji ndani ya CHADEMA ambao walikuwa wanaamini waliipigania chama kwa muda mrefu wakati huo Lowassa "anakula raha" CCM. Kuna watu CHADEMA wamepotezwa kabisa kwa ujio wa Lowassa.
Jambo moja la kufurahisha ni kwamba hata CCM wanaposema vyama vya upinzani humaanisha CHADEMA. je CHADEMA wenyewe wanaijua na kuikuza thamani yao?