Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza rasmi kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 utafanyika tarehe 29 Oktoba. Tangazo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele, tarehe 26 Julai 2025, alipokuwa akitoa ratiba ya uchaguzi.
Uchaguzi huo utahusisha kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Bunge la Taifa, pamoja na Madiwani kwa upande wa Tanzania Bara. Ni sehemu muhimu ya mchakato wa kidemokrasia unaofanyika kila baada ya miaka mitano.
Kwa mujibu wa Jaji Mwambegele, jumla ya wapiga kura waliojiandikisha ni milioni 37,655,559. Aidha, vituo vya kupigia kura vitakavyotumika katika uchaguzi huo ni 99,911, vilivyosambaa nchi nzima.
INEC imesisitiza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na imewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi
Soma pia: GE2025 - Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania kutangaza ratiba ya Uchaguzi Mkuu