Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwakilishi wa viti Maalumu CCM Asha Bakari Makame amependekeza kwa kamati ya kuratibu maoni ya katiba kwamba umri wa rais inafaa uongezwe ili kiongozi atumie busara katika kuongoza nchi.
Amesema mgombea urais kuwa chini ya miaka 40 inamaanisha atapatikana rais wa watoto. Aliyasema hayo juzi tume hiyo ilipokutana na Baraza la Wawakilishi.
Ni mapendekezo mazuri sana hasa ukizingatia nafasi yetu tulipo kama taifa yaani kisiasa, kiuchumi na kifikra. Taifa letu hatupaswi kabisa kufanya majaribio. Hekima ya hali ya juu sana inahitajika katika ofisi ya juu kama ikulu. Nikiangalia jinsi taifa la China lilivyo imara na serious katika masuala yote nyeti, jibu ni kwa sababu wameiheshimu sana ofisi kuu(ikulu) nchini mwao. Rais wa China huanzia umri wa miaka 70 na kuendelea. Kwetu kulingana na umri kushuka na watu kutaka kuwahi kujionyesha hata kabla ya kukomaa kiakili na kifikra napendekeza umri wa mtu atakaeruhusiwa kikatiba kuingia ikulu, angalau uanzie miaka 50 na ukomo wa mtu kuwepo ikulu uwe miaka 85 kwa maana kwamba atakaepata uraisi akiwa na miaka 80 ataongoza awamu moja tu.
.
Hatuandiki katika mpya kumfurahisha mtu mwenye tamaa zake, bali tunaandika katiba mpya kwa ajili ya miaka 50 ijayo, labda ungeuliza wakati Marekani inaweka kikomo cha Urais kuwa miaka 8 walikuwa wanamkomoa nani?Haya ni mapendekezo ya kumkomoa mtu. Mapendekezo kama haya hayafai kabisa hasa katika suala nyeti kama katiba. Niwaulize swali je umri mkubwa ndio kigezo cha mtu kuwa na busara na uwezo wa kuongoza?
Hili ni pendekezo zuri kwa kila kipimo. Lakini binafsi naamini ingeongezwa kwenye nafasi zote; udiwani na Ubunge isiwe chini ya miaka 30; Urais isiwe chini ya miaka 45 na nafasi zote ukomo uwe miaka 70! Na mtu akigombea akiwa na miaka sabini basi anaruhusiwa kipindi kimoja tu katika nafasi zote.