Wapendekeza umri urais uongezwe badala ya kupunguzwa - Maoni Katiba Mpya

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
ikulu_300_185.jpg



Mwakilishi wa viti Maalumu CCM Asha Bakari Makame amependekeza kwa kamati ya kuratibu maoni ya katiba kwamba umri wa rais inafaa uongezwe ili kiongozi atumie busara katika kuongoza nchi.

Amesema mgombea urais kuwa chini ya miaka 40 inamaanisha atapatikana rais wa watoto. Aliyasema hayo juzi tume hiyo ilipokutana na Baraza la Wawakilishi.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa pendekezo hilo la wananchi, uhuni kwenye siasa na vijitoto vinavyotafuta sehemu pa kuendelea kuimarika ki-umri kamwe hawatopata nafasi ya kwenda kufanyia majaribio maisha ya WaTanzania.
 
Hili nalo la msingi....ningependekeza iwe 55 angalau tumpate raisi aliyestaafu kuitumikia familia yake......ili awe na muda wa kuwatumikia wanannchi
 
[1]Napendekeza umri wa urais uongezwe hadi miaka 45.

[2] Lazima awe ameoa au kuolewa.

[3] Asiwe amewahi kupatwa na magonjwa ya kuanguka au kurukwa na akili.

[4] Apimwe afya kabla ya kugombea.
 
Umri wa Urais yapaswa uwe ni miaka 50 hapa ndipo tunapoweza kusema binadamu amekomaa, Urais wa Tanzania si Urais wa TFF au Miss Tanzania.
 
[1]Napendekeza umri wa urais uongezwe hadi miaka 45.

[2] Lazima awe ameoa au kuolewa.

[3] Asiwe amewahi kupatwa na magonjwa ya kuanguka au kurukwa na akili.

[4] Apimwe afya kabla ya kugombea.

hapo kwenye red umaanisha nini??
 
anaongea kwa sababu anajua umri H.mwinyi na Riz1,january, wanaandaliwa kwa miaka ijayo lakini wajue magogoni 2015 chadema
 
Hili ni pendekezo zuri kwa kila kipimo. Lakini binafsi naamini ingeongezwa kwenye nafasi zote; udiwani na Ubunge isiwe chini ya miaka 30; Urais isiwe chini ya miaka 45 na nafasi zote ukomo uwe miaka 70! Na mtu akigombea akiwa na miaka sabini basi anaruhusiwa kipindi kimoja tu katika nafasi zote.
 
Kuna watu wanataka kuweka kliniki pale magogono.
Dogo hajaoa akipewa urais ina maana kwa uzazi wa mpango kwa miaka kumi atakuwa mezaa watoto watano.
Kweli dogoalitaka kuuwa ndege 10 kwa jiwe moja.
 
Nyerere alikuwa na miaka 39 alikuwa raisi wa watoto? Mbona pamoja na uzee wa karume alikubaliana na nyerere.
 
Naunga mkono hoja, ubunge iwe miaka 30 na urais iwe 45 hawa watoto na vijana waendele kujengwa kwaza katika ngazi za udiwani na vyama ili baadae tupate viongozi bora na sio vigeugeu
 
Hili ninamuunga mkono. Lakini pia umri wagombea ubunge na udiwani vile vile.

Kwa urais hata mimi naona nii sawa; umri uongezwe lakini kwa ubunge na udiwani is not that much important. Kuna wabunge na madiwani vijana ambao ingawa kwa urais hata wao nadhani wanajua hawawezi lakini wamefanya vizuri sana katika ubunge na udiwani!
 
Hili ni pendekezo zuri kwa kila kipimo. Lakini binafsi naamini ingeongezwa kwenye nafasi zote; udiwani na Ubunge isiwe chini ya miaka 30; Urais isiwe chini ya miaka 45 na nafasi zote ukomo uwe miaka 70! Na mtu akigombea akiwa na miaka sabini basi anaruhusiwa kipindi kimoja tu katika nafasi zote.

Naunga mkono hoja!
Tukiangalia pia umri wa viongozi wanaotakiwa kwenye umoja wa vijana wa vyama ambao ni chini ya miaka 30, inamaana hao wanaoitwa vijana kwenye vyama watakuwa wamezuiliwa hata kuwa madiwani! Nadhani tungefanya udiwani uwe 25. Ni mtazamo wangu.
 
Haya ni mapendekezo ya kumkomoa mtu. Mapendekezo kama haya hayafai kabisa hasa katika suala nyeti kama katiba. Niwaulize swali je umri mkubwa ndio kigezo cha mtu kuwa na busara na uwezo wa kuongoza?
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom