Wapenda makuu ni matatizo katika jamii.

Wapenda makuu ni matatizo katika jamii.

jf user

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
777
Reaction score
625
Haina haja ya kuumiza kichwa sana kwani mwisho wa watu wanaopenda vitu vilivyoko nje ya uwezo wao huishia pabaya.
Watu wanaopenda umaarufu wasiouweza, utajiri/mali, nafasi za kazi n.k ndio huishia kwenye uuaji, ushirikina/uchawi/ushetani, madawa ya kulevya, wizi, ushoga, umalaya mwishowe ni kifo kwa sababu MUNGU hatakuacha ufanye uharibifu wote huu mbele ya wapendwa/wateule wake.

Maisha ni kujikubali/kuridhika vile ulivyo kupapatikia usiyoyaweza utaishia pabaya.
Ukitaka uishi maisha ya furaha ridhika na hali yako vinginevyo utataabika na utakua unahaha kama mbwa anaeachama juani akitembea barabarani.
Mwisho wa makuu ni dhambi, magonjwa hasa ukimwi, laana na mikosi maishani mwako mwishowe ni kifo.
Jamii ya hawa viumbe ni mkosi/matatizo popote pale duniani.
Uzuri mifano tunayo kwenye jamii kwa hiyo yujifunze tusirudie makosa.
 
Ukitaka uishi maisha ya furaha ridhika na hali yako vinginevyo utataabika na utakua unahaha kama mbwa anaeachama juani akitembea barabarani.

Sawa, ni vizuri kuridhika na hali uliyonayo. Ila hii sio excuse/kisingizio cha kuzembea na kuacha kutafuta maisha kihalali. Vinginevyo utabaki maskini kuchukia wenye mafanikio zaidi yako na hutaendelea kamwe.
 
Nimekuelewa vyema mkuu... Unajua kuna wezo wa mwisho wa mtu wa kutafuta? hapo ndipo naposema ridhika na hali yako... yes huo ndio uwezo wako kwahiyo ridhika nao.
Huwezi tafuta Zaidi ya hapo mzee kwa hiyo jikubali/kubaliana na hali yako halisi.
 
Uwezo wa mtu kutafuta kihalali hauna kikomo. Ukomo huanza uhalali unapokosekana eg. Wanaotumia nguvu za giza kutafuta hawana kipato cha halali mbele za Mungu wa Mbinguni.
 
Hakuna kikomo katika kutafuta bali unatumia mbinu gani kutafuta.
Nimekuelewa vyema mkuu... Unajua kuna wezo wa mwisho wa mtu wa kutafuta? hapo ndipo naposema ridhika na hali yako... yes huo ndio uwezo wako kwahiyo ridhika nao.
Huwezi tafuta Zaidi ya hapo mzee kwa hiyo jikubali/kubaliana na hali yako halisi.
 
Ukomo wa kutafuta ni pale unapodhani unafika ukomo
Wanaodhani wamefika ukomo ni pale wanapotumia njia nyingine kutafuta. Kama kubeba madawa,ujambazi, ushirikina. Ukiona mambo hayaendi na ukapambana kwa njiaa halali bado hujafika ukomo.
 
Wanaodhani wamefika ukomo ni pale wanapotumia njia nyingine kutafuta. Kama kubeba madawa,ujambazi, ushirikina. Ukiona mambo hayaendi na ukapambana kwa njiaa halali bado hujafika ukomo.
Na ukomo huja pale mtu anaporidhika ama anapokata tamaa
 
Uwezo wa mtu kutafuta kihalali hauna kikomo. Ukomo huanza uhalali unapokosekana eg. Wanaotumia nguvu za giza kutafuta hawana kipato cha halali mbele za Mungu wa Mbinguni.
Utafanyaje sasa kama huwezi zalisha au ingiza Zaidi ya ulicho nacho?
Hapo ni kujikubali mkuu na kuendelea na hicho/hivo ulivyo navyo.
Kikomo kipo pale ambapo huwezi lazisha Zaidi ya uwezo wako.
Tusidanganyane mkuu! We unasema tusidishe jitihada pale tunapohisi ni kikomo kumbe ni mwanzo wa kutumia njia haramu za kishetwaini kujipatia mali.
Cc Mzigua90 Mc cane
 
utakufa maskini!
Nope watu wasioridhika na walivyo navyo ndio huingia kwenye hizo njia haramu.
Mimi naamini maiahs ni kujikubali basi unabaki na Amani.
Hayo mengine unayosema kwangu mimi haina tofauti na wanawake wanaotumia mchina kuongeza chura matokeo yake kuishia pabaya.
So kujikubali for me is everything.
Huwezi fanya Zaidi ya uwezo wako hata darasani wapo watu wanaopata A, B, C, D na wengine failure kabisa so ni uwezo ndugu yangu.
Do not cheat yourself.
Cc Prisoner of hope
 
Mtoa mada umeandika mambo mazuri na yenye maana sna ila wengi hawajakuelewa...Big up
 
jiandae kwa hilo hakika " . halafu hakuna sababu ya kuogopa sana kifo .. kwa sababu kufikwa na umauti ni lazima
Lakini umauti unakufika kabla ya siku zako!
 
Uwezo wa mtu kutafuta kihalali hauna kikomo. Ukomo huanza uhalali unapokosekana eg. Wanaotumia nguvu za giza kutafuta hawana kipato cha halali mbele za Mungu wa Mbinguni.
ukomo wa kutafuta haupo na hakuna kabisa chief "... acha kujipa hayo mawazo hasi
 
Kwa mawazo ya wengi humu naona mnaiwazaga leo tuu hamuiwazi kesho yenu na familia, ndugu jamaa na marafiki.
 
Back
Top Bottom