Dalili kuwa unahishi na mchawi au upo katika himaya ya nguvu za kishirikina

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,181
5,315
Uchawi si jambo geni madamu upo afrika uhitaji mtu akuelezee maana yake ni nini hasa, bali wahitaji kujua nauepuka vipi au ntautambuaje kama huu ndiyo uchawi wenyewe.

Jibu lipo hapa leo ntataja sifa za uchawi uonekanao kwa macho ya kawaida na machale ya rohoni hivyo sipo hapa kuelezea matumizi ya uchawi kuugundua uchawi au kupambana nao bali na-share nanyi nachokijua kuhusu mtu msafi kiroho(asiyejiusisha na shirki)anavyo weza kujua au kugundua yanayomkabili halipo au anapoishi dhidi ya ushirikina.

Sifa ya kwanza ya mchawi ni ukarimu na upendo wakinafiki; usishangae kuna tofauti ndogo sana kati ya mchawi na mnafiki ukiwa uwezi mtofautisha mtu kama ni mnafiki au mkweli basi si rahisi kwako kumjua mchawi maana mchawi ni mnafiki professional, watu hawa uvunga wakarimu kupita kiasi,ufahamiana na kila mtu pale mtaani akupiti bila salamu, uigiza kwenda kanisani au msikitini na uheshimiwa sana na pia ukaa hata siti za mbele,

utembelewa na watu wasiofahamika mara kwa mara kama vikongwe au watu makamo na ukaa vikao mbalimbali uhani au chini ya miti au sebuleni bila kueleweka wanajadiligi nini,upenda kukudadisi sana na kujipendekeza kinafiki kama rafiki au kulazimisha kukusaidia hata kama huna shida na msaada wake.

Muda wote uionesha dunia kuwa wao ni watu wakucheka/wenye furaha/mtu wa watu au wasiokasirika hata pale wanapopaswa kuumia ila ukiwa makini kuwatizama machoni na kwenye paji lao la uso,

utagundua kuna sura ya machukizo na uasi nyuma ya lile tabasamu feki linalopumbaza wengi kuwatetea hata pindi ukisema ni wachawi utaambulia kutukanwa nakuambiwa wewe ndo mchawi hivyo kuwa makini sana maana mchawi anajua sana sanaa yakuaminisha jamii kwamba ni mtu mwema zaidi.

Migogoro isiyo na kichwa wala miguu; watu hawa upenda vyesi na kama ni mwenye nyumba na wewe ni mpangaji kila jambo uanzia serikali za mitaa na uwaweka karibu mno watu hawa kumtetea pindi likija kubumburuka, ni mtu mpenda shari na masharti mengi lakini kwa juu pia uvaa ngozi ya kondoo nakuvunga mnyenyekevu na asiye na makuu mbele ya watu wengi atakuacha ukiwa na doa.

Masharti; utakapokuwa umetembelea mji fulani au umeamia kama mpangaji zingatia kwanza suala la masharti je, masharti hayo unayopewa kwa mtizamo wa kawaida hayatii shaka kuwa kuna kitu akiko sawa, mfano utakiwi kukaa au kutoka nje usiku(licha ya usalama wakimazingira), usimwage maji uhani, kuna miti utakiwi kuketi chini yake au kuigusa,uruhusiwi kusikiliza mziki au kupiga kelele ya aina yeyote, usilete demu au marafiki au wageni bila ya ruhusa,n.k

Usafi usiyo wa kawaida; wachawi wengi utumia majini katika shughuli zao hivyo basi wengi wa majini haya upenda hali ya usafi na manukato,dalili ya kwanza ni msisitizo unaowekwa na masharti yakutosha kuhusu usafi wa mazingira na vyoo 24/7 hapa si ajabu kwenye kona za milango yakuingilia chooni au bafuni mara kwa mara ukakuta kuna kipisi cha udi uliochomwa au manukato au harufu nzuri za vyakula maliwatoni n.k

Kuhisi kelele za ngoma au sauti za vigelegele vya watu walioko kwenye sherehe fulani au vicheko na sauti za kilio cha watoto wachanga kupitia paka(japo si mara zote ni uchawi),milio ya fisi au bundi, kuhisi hali ya woga,msisimko wa ghafla mwilini, kuhisi kuna michanga inarushwa kupitia dirishani au juu ya bati,kusikia hatua za mtu akitembea juu ya bati katika paa lako, kuamka umechanjwa mwilini,kusikia sauti inakuagiza ufungue mlango nakukuita jina lako katika nyakati za usiku.

Uzinzi, dalili hii inaashiria mchawi sasa ameanza kuvuka mipaka nakuanza kukuchafua kiroho, hapa utakuwa usingizini lakini wahisi au kuota unaingiziwa kidole......au unaingiliwa kimwili au kinyume na maumbile kwa nguvu na unaishiwa nguvu ya kujinusuru(kwa jinsia zote),kuota mara kwa mara hata mchana ukiwa umelala kuwa wafanya mapenzi na watu usiwafahamu au unaowafahamu.

Mapambano kwenye ulimwengu wa ndoto; hapa utakuwa wewe ni mtu wa kuota vitu vya kutisha kama majoka,kung'atwa na wadudu,nyoka,mbwa n.k,kukimbizwa mara kwa mara,matukio ya vifo,kufunga ndoa,kuota ulaji wa nyama au

mizoga,unywaji maziwa,damu,au vyakula ndotoni,kuota wapigana au wapambana na nguvu mbaya kupitia maombi, kujikuta kwenye mazingira machafu machafu au kukanyaga vinyesi,maji machafu,mizoga au kuwa peku au kukabwa na kushindwa kupumua n.k

Uwepo wa mazingira ya siri kama vyumba visivyoeleweka matumizi yake, kutotakiwa kwenda upande fulani wa nyumba au ua, ujio wa waganga au imani za kipagani nakishirikina kufanywa kwa usiri hapo nyumbani,

matambiko na kuchimbia madawa au vitu ardhini, kugundua kuna makaburi mahali pasipo sahihi mfano pembeni mwa dirisha,mlangoni, chumbani,uwepo wa mimea ambayo uhusishwa na madawa yakishirikina n.k

Hofu isiyoweza elezeka toka kwa watu wa nje; utashangaa kuwa ukimwelekeza mtu kuja kukutembelea unapoishi muda mwingi wanakuwa wazito kuja au wanakuuliza mara mbili mbili hivi umesema unakaa wap vile?

Majirani kuonekana kama kuna wanachokijua ila hawawezi kusema labda ukiwa na ukaribu nao utadokezwa,watu kuogopa hata kukatiza kwenye mji huo pasipo hata kuambiwa wasifanye hivyo, japo hata kama ni nyumba nzuri kivipi muda wote unahisi hofu na upweke kana kwamba uko empty na maisha yako hayako sawa.

Mambo yako kukwama na kila jambo zuri kuchelewa au kukufikia mara tu unapokuwa umeshakata tamaa mfano ni kushangaa upati mwenza hata utumie nyenzo gani, kazini kutopendwa,marafiki kukugaya na wanandugu kukutenga kiaina, uchumi kuzidi kuwa mbaya, kuwa mtu wa ovyo nakutojali tena usafi,kujitunza, afya au mahusiano, badala yake kuwa mwenye urahibu wa ngono na watu wasiofaa,punyeto,kamari, pombe kupita kiasi n.k

vile vile kuwa na tatizo la akili au saikolojia mara kwa mara kuona visivyoonekana,kuongea mwenyewe,kushtuka mara kwa mara usingizini nakupiga makelele, kuwa na uso wenye hamaki,kutingisha kichwa au kuangalia pembeni mara kwa mara,kupikicha sana masikio au pua,kutokuwa na maamuzi sahihi au kuonekana kichaa n.k

kiufupi dalili ni nyingi mno inahitaji umakini kidogo wa kuyatafakari na kuchunguza mazingira yanayokuzunguka kwa umakini kujua upo mahali pasipo sahihi kwako na yakwamba shetani anakuandama.

Ni hatua gani uchukuwe unapojua kuwa sasa tiyari umeshaingia kwenye ngome ya wanga,

Cha kwanza, jiepushe kabisa na matendo yeyote ya kishirikiana kama afanyavyo mtesi wako, kama masharti yamewekwa usiangaike kuyavunja(when in Rome do as romans do) usijeingia kwenye migogoro mingi au kufatiliana isipokuwa usifanye yale yasiyovumilika au kuenenda kinyume na imani yako na wala moyoni usiyafate bali yapuuze au chukulia ni uprimitive au ukosefu wa ustaarabu. Usijiusishe nakuvisit waganga au kutumia mbinu mbalimbali zakuzuia nguvu za kichawi baki ulivyo.

Cha pili, Kama imani yako ilikuwa chini au ya vuguvugu jitahidi sasa umrudie Mwenyezi Mungu wako kwa dhati kabisa kiri moyoni mwako kuokoka na upokee wokovu wake na umwombe akuepushie majanga hayo, kwa mkristo ufunguo ni Yesu kristo, kifo chake msalabani na damu yake iliyoleta wokovu nakukufungua kutoka katika minyororo ya dhambi, kwa imani zingine amini na usali au uswali kadri ya unavyomwamini Mungu wako, endapo ukigundua kuwa imani yako ni haba tafuta njia mbadala ya msaada wa maombezi au dua kwa watu wanaokuzidi imani au viongozi wa dini.

Cha tatu; ama narudia tena hama yakikuzidia usijilazimishe kuendelea kuishi kwenye matatizo kisa umetoa kodi,au unamfurahisha mtu, ukihama hakikisha ujulikani ulipoenda na pia nenda mbali na mahali hapo pengine uko uendako unaweza kuta ni pasafi na hamna hayo mambo au uko upinzani si mkubwa kama pale pa mwanzo.

Cha nne;dawa ya moto ni moto pambana nao kichawi nawe nenda kwa vigagula waganguzi wakugange mpambane mpaka wakunyooshee mikono na heshima iwepo.
Ila ukiferi usijelahumu watu uwe tiyari kubeba msalaba wako mwenyewe.

Cha tano; potezea na dharau kuwa uchawi ni ujinga na haupo wala hauwezi kukudhuru wala nini zaidi ya mazingaombwe na utoto, niamini imani yako itakuwa imekuponya nakukuondolea stress nyingi na cha zaidi mchawi hana shida na mtu wa namna hii,kama unaweza tatua matatizo haya kwa njia hii pia ni sawa.

NB; Hapo nimezungumzia tu dalili za mazingira ya mchawi wa nje na siyo wa ndani yaani we wewe mwenyewe au wapendwa wako kama mke,au ndugu na namna yakugundua kama unajichawia mwenyewe au unafanyiziwa na mkeo au ndugu hiyo pia ni mada nyingine.
 
4 na 5 Apo nipuuze Kisha badae Ni revange mkuu ,ebu tuweke sawa .But thanks
Hizi zote ni njia za utatuzi wa tatizo katika njia yeyote hapo juu suala lako linaweza kutatulika nakufikia mwisho na ikitokea tatizo bado alijaisha unaendelea na kipengele kinachofata katika huo mtiririko 1, 2 mpaka 3

Japo kipengele namba 4 na 5 ni option utachagua njia ipi kati ya hizo ufate aidha umetumia moja mpaka tatu ikashindikana au ujataka kuzitumia hizo step za kwanza mpaka tatu waweza kuanza moja kwa moja na kipengele chochote kati ya 4 au 5,

kumbuka namba 4 ni hatari kubwa kuliko vipengele vyote hivyo ichukue ukijua lolote likikupata utakabiliana nalo mwenyewe

Namba 5 mara nyingi utumiwa na watu wasioamini uchawi,waliojikita kwenye mtizamo chanya, majasiri,wasiojali,walioathiriwa na usomi au sayansi,wenye tamaduni za kimagharibi zakuamini uchawi huu ni old fashion, n.k Kwahiyo utaona njia ipi inakufaa,kumbuka njia hizi pia zaweza tumika vice versa.
 
Nakubaliana na wewe kwa kila kitu hapo juu, mm pia huwa !asumbuliwa na mwili kusisimka ghafla. Ninini tiba ya jambo hili?
 
Uchawi si jambo geni madamu upo afrika uhitaji mtu akuelezee maana yake ni nini hasa, bali wahitaji kujua nauepuka vipi au ntautambuaje kama huu ndiyo uchawi wenyewe.

Jibu lipo hapa leo ntataja sifa za uchawi uonekanao kwa macho ya kawaida na machale ya rohoni hivyo sipo hapa kuelezea matumizi ya uchawi kuugundua uchawi au kupambana nao bali na-share nanyi nachokijua kuhusu mtu msafi kiroho(asiyejiusisha na shirki)anavyo weza kujua au kugundua yanayomkabili halipo au anapoishi dhidi ya ushirikina.

Sifa ya kwanza ya mchawi ni ukarimu na upendo wakinafiki; usishangae kuna tofauti ndogo sana kati ya mchawi na mnafiki ukiwa uwezi mtofautisha mtu kama ni mnafiki au mkweli basi si rahisi kwako kumjua mchawi maana mchawi ni mnafiki professional, watu hawa uvunga wakarimu kupita kiasi,ufahamiana na kila mtu pale mtaani akupiti bila salamu, uigiza kwenda kanisani au msikitini na uheshimiwa sana na pia ukaa hata siti za mbele,

utembelewa na watu wasiofahamika mara kwa mara kama vikongwe au watu makamo na ukaa vikao mbalimbali uhani au chini ya miti au sebuleni bila kueleweka wanajadiligi nini,upenda kukudadisi sana na kujipendekeza kinafiki kama rafiki au kulazimisha kukusaidia hata kama huna shida na msaada wake.

Muda wote uionesha dunia kuwa wao ni watu wakucheka/wenye furaha/mtu wa watu au wasiokasirika hata pale wanapopaswa kuumia ila ukiwa makini kuwatizama machoni na kwenye paji lao la uso,

utagundua kuna sura ya machukizo na uasi nyuma ya lile tabasamu feki linalopumbaza wengi kuwatetea hata pindi ukisema ni wachawi utaambulia kutukanwa nakuambiwa wewe ndo mchawi hivyo kuwa makini sana maana mchawi anajua sana sanaa yakuaminisha jamii kwamba ni mtu mwema zaidi.

Migogoro isiyo na kichwa wala miguu; watu hawa upenda vyesi na kama ni mwenye nyumba na wewe ni mpangaji kila jambo uanzia serikali za mitaa na uwaweka karibu mno watu hawa kumtetea pindi likija kubumburuka, ni mtu mpenda shari na masharti mengi lakini kwa juu pia uvaa ngozi ya kondoo nakuvunga mnyenyekevu na asiye na makuu mbele ya watu wengi atakuacha ukiwa na doa.

Masharti; utakapokuwa umetembelea mji fulani au umeamia kama mpangaji zingatia kwanza suala la masharti je, masharti hayo unayopewa kwa mtizamo wa kawaida hayatii shaka kuwa kuna kitu akiko sawa, mfano utakiwi kukaa au kutoka nje usiku(licha ya usalama wakimazingira), usimwage maji uhani, kuna miti utakiwi kuketi chini yake au kuigusa,uruhusiwi kusikiliza mziki au kupiga kelele ya aina yeyote, usilete demu au marafiki au wageni bila ya ruhusa,n.k

Usafi usiyo wa kawaida; wachawi wengi utumia majini katika shughuli zao hivyo basi wengi wa majini haya upenda hali ya usafi na manukato,dalili ya kwanza ni msisitizo unaowekwa na masharti yakutosha kuhusu usafi wa mazingira na vyoo 24/7 hapa si ajabu kwenye kona za milango yakuingilia chooni au bafuni mara kwa mara ukakuta kuna kipisi cha udi uliochomwa au manukato au harufu nzuri za vyakula maliwatoni n.k

Kuhisi kelele za ngoma au sauti za vigelegele vya watu walioko kwenye sherehe fulani au vicheko na sauti za kilio cha watoto wachanga kupitia paka(japo si mara zote ni uchawi),milio ya fisi au bundi, kuhisi hali ya woga,msisimko wa ghafla mwilini, kuhisi kuna michanga inarushwa kupitia dirishani au juu ya bati,kusikia hatua za mtu akitembea juu ya bati katika paa lako, kuamka umechanjwa mwilini,kusikia sauti inakuagiza ufungue mlango nakukuita jina lako katika nyakati za usiku.

Uzinzi, dalili hii inaashiria mchawi sasa ameanza kuvuka mipaka nakuanza kukuchafua kiroho, hapa utakuwa usingizini lakini wahisi au kuota unaingiziwa kidole......au unaingiliwa kimwili au kinyume na maumbile kwa nguvu na unaishiwa nguvu ya kujinusuru(kwa jinsia zote),kuota mara kwa mara hata mchana ukiwa umelala kuwa wafanya mapenzi na watu usiwafahamu au unaowafahamu.

Mapambano kwenye ulimwengu wa ndoto; hapa utakuwa wewe ni mtu wa kuota vitu vya kutisha kama majoka,kung'atwa na wadudu,nyoka,mbwa n.k,kukimbizwa mara kwa mara,matukio ya vifo,kufunga ndoa,kuota ulaji wa nyama au

mizoga,unywaji maziwa,damu,au vyakula ndotoni,kuota wapigana au wapambana na nguvu mbaya kupitia maombi, kujikuta kwenye mazingira machafu machafu au kukanyaga vinyesi,maji machafu,mizoga au kuwa peku au kukabwa na kushindwa kupumua n.k

Uwepo wa mazingira ya siri kama vyumba visivyoeleweka matumizi yake, kutotakiwa kwenda upande fulani wa nyumba au ua, ujio wa waganga au imani za kipagani nakishirikina kufanywa kwa usiri hapo nyumbani,

matambiko na kuchimbia madawa au vitu ardhini, kugundua kuna makaburi mahali pasipo sahihi mfano pembeni mwa dirisha,mlangoni, chumbani,uwepo wa mimea ambayo uhusishwa na madawa yakishirikina n.k

Hofu isiyoweza elezeka toka kwa watu wa nje; utashangaa kuwa ukimwelekeza mtu kuja kukutembelea unapoishi muda mwingi wanakuwa wazito kuja au wanakuuliza mara mbili mbili hivi umesema unakaa wap vile?

Majirani kuonekana kama kuna wanachokijua ila hawawezi kusema labda ukiwa na ukaribu nao utadokezwa,watu kuogopa hata kukatiza kwenye mji huo pasipo hata kuambiwa wasifanye hivyo, japo hata kama ni nyumba nzuri kivipi muda wote unahisi hofu na upweke kana kwamba uko empty na maisha yako hayako sawa.

Mambo yako kukwama na kila jambo zuri kuchelewa au kukufikia mara tu unapokuwa umeshakata tamaa mfano ni kushangaa upati mwenza hata utumie nyenzo gani, kazini kutopendwa,marafiki kukugaya na wanandugu kukutenga kiaina, uchumi kuzidi kuwa mbaya, kuwa mtu wa ovyo nakutojali tena usafi,kujitunza, afya au mahusiano, badala yake kuwa mwenye urahibu wa ngono na watu wasiofaa,punyeto,kamari, pombe kupita kiasi n.k

vile vile kuwa na tatizo la akili au saikolojia mara kwa mara kuona visivyoonekana,kuongea mwenyewe,kushtuka mara kwa mara usingizini nakupiga makelele, kuwa na uso wenye hamaki,kutingisha kichwa au kuangalia pembeni mara kwa mara,kupikicha sana masikio au pua,kutokuwa na maamuzi sahihi au kuonekana kichaa n.k

kiufupi dalili ni nyingi mno inahitaji umakini kidogo wa kuyatafakari na kuchunguza mazingira yanayokuzunguka kwa umakini kujua upo mahali pasipo sahihi kwako na yakwamba shetani anakuandama.

Ni hatua gani uchukuwe unapojua kuwa sasa tiyari umeshaingia kwenye ngome ya wanga,

Cha kwanza, jiepushe kabisa na matendo yeyote ya kishirikiana kama afanyavyo mtesi wako, kama masharti yamewekwa usiangaike kuyavunja(when in Rome do as romans do) usijeingia kwenye migogoro mingi au kufatiliana isipokuwa usifanye yale yasiyovumilika au kuenenda kinyume na imani yako na wala moyoni usiyafate bali yapuuze au chukulia ni uprimitive au ukosefu wa ustaarabu. Usijiusishe nakuvisit waganga au kutumia mbinu mbalimbali zakuzuia nguvu za kichawi baki ulivyo.

Cha pili, Kama imani yako ilikuwa chini au ya vuguvugu jitahidi sasa umrudie Mwenyezi Mungu wako kwa dhati kabisa kiri moyoni mwako kuokoka na upokee wokovu wake na umwombe akuepushie majanga hayo, kwa mkristo ufunguo ni Yesu kristo, kifo chake msalabani na damu yake iliyoleta wokovu nakukufungua kutoka katika minyororo ya dhambi, kwa imani zingine amini na usali au uswali kadri ya unavyomwamini Mungu wako, endapo ukigundua kuwa imani yako ni haba tafuta njia mbadala ya msaada wa maombezi au dua kwa watu wanaokuzidi imani au viongozi wa dini.

Cha tatu; ama narudia tena hama yakikuzidia usijilazimishe kuendelea kuishi kwenye matatizo kisa umetoa kodi,au unamfurahisha mtu, ukihama hakikisha ujulikani ulipoenda na pia nenda mbali na mahali hapo pengine uko uendako unaweza kuta ni pasafi na hamna hayo mambo au uko upinzani si mkubwa kama pale pa mwanzo.

Cha nne;dawa ya moto ni moto pambana nao kichawi nawe nenda kwa vigagula waganguzi wakugange mpambane mpaka wakunyooshee mikono na heshima iwepo.
Ila ukiferi usijelahumu watu uwe tiyari kubeba msalaba wako mwenyewe.

Cha tano; potezea na dharau kuwa uchawi ni ujinga na haupo wala hauwezi kukudhuru wala nini zaidi ya mazingaombwe na utoto, niamini imani yako itakuwa imekuponya nakukuondolea stress nyingi na cha zaidi mchawi hana shida na mtu wa namna hii,kama unaweza tatua matatizo haya kwa njia hii pia ni sawa.

NB; Hapo nimezungumzia tu dalili za mazingira ya mchawi wa nje na siyo wa ndani yaani we wewe mwenyewe au wapendwa wako kama mke,au ndugu na namna yakugundua kama unajichawia mwenyewe au unafanyiziwa na mkeo au ndugu hiyo pia ni mada nyingine.
hongera sana kwa newz yko ila ulionena yote ni km unamzungumzia bibi yangu.maana migogoro na chuki havimalizi kwake na mengne kibao
 
Back
Top Bottom