Wapemba Waanza Kukamatwa

ikiwa comoro ili kuleta usawa au kujaribu kufanya hivyo visiwa vitatu grand comoro, anjoun na kingine jina limenitoka kidogo wameweza klufanya hivyo je kinacho shindikana zanzibar ni nini? au kinacho chelewesha nini ? kama sio unafiki wa baadhi ya watu, hususani . vingapi wana vifanya bila kupiga kura ya maoni? au hiyo demokrasia ya kura ya maoni ni nzuri ikiwa hakuna maslahi yao binafsi?
 
Biafra haunting "bongo"?

we recognised biafra for the reasons of Ibo people being descriminated by the nigeria federal government.

what are we going to do with pemba people?
 
Sidhani kama kujitenga ni suluhisho la mwisho na kudumu la matatizo ya watanzania wa kisiwa cha Pemba.

Nakubaliana na wewe kujitenga si suluhisho na hii sisemei kwa Pemba na Unguja ambazo ni nchi moja asili na asili lakini hata na Muungano wetu - lakini la kujiuliza tutawasaidiaje Wapemba kwani madhila na kutengwa na serkali ya CCM hayana ubishi( atayebisha ni kwa utashi wake tu)kisa ni kutoiunga mkono na kama ni uvumilivu wameuonyesha narudia TUFANYEJE?
 
Watanzania Jamani kiama cha mwisho chaja; ndg zetu wa damu amabo nyerere aliwappigania leo wanatupwa mbele ya kaburi lake; wasitegemee muafaka tena watu walishaapa kiukweli si masihara; sio siri mimi nawahurumia sana CUF maana wamekuwa wavumilivu kuliko maelezo; sasa wamefika mwisho, nami nawaunga mkono kwa hilo; basi kama vipi PEMBA Yote wawekwe kifungoni maana wote wana mawazo sawa; ya democrasia ya kweli bila kujali ni rangi ya kijani; sio wabara waoga wakati wanakufa kwa njaa na maradhi huku vijisenti vyao vikitupwa; Tuwaunge mkono kwa moyo wa dhati; jamaa hawa utawala umewashinda; kumbe Tanzania kuna wauaji ambao walitakiwa kulinda usalama wa raia; kodi zetu kwa majeshi ni kwa ajili kuua au kukamata raia wema? kama lengo ni hilo kuna haja gani ya kuendelea kulipa kodi yangu?
 
Mimi kabla ya kuanza kuunga ama kupinga naomba kujua hawa watu wamekamatwa kwa sababu ipi ?Wamekamatwa je wamesha funguliwa mashitaka ?Ni kweli kosa lao litakuwa kupeleka barua UN ? Je UN wana habari ya huu mkasa ?
 
JK naye msanii tuu,anajidai kupeleka majeshi Commoro kutetea haki huku wananchi wake face the same fate kama ya Wacommoro,mpuuzi kweli huyu mtuu...tena asije kutuambia baadaye kama Mkapa alipoulizwa kitu gani unajuta katika utawala wake? bila aibu eti machafuzi ya Zanzibar na i wish ninge handle kwa namna tofauti,haya mkapa uko wapi sasa..do somethin au unaogopa ukienda public utaulizwa kiwira.
 
Mimi kabla ya kuanza kuunga ama kupinga naomba kujua hawa watu wamekamatwa kwa sababu ipi ?Wamekamatwa je wamesha funguliwa mashitaka ?Ni kweli kosa lao litakuwa kupeleka barua UN ? Je UN wana habari ya huu mkasa ?

Kwa wakati tulionao habari ni nyeti na ya uhakika walikamatwa usiku wa kuamkia leo Jumatatu ,May 12 2008 ,inavyoonyesha walitegemea kuwa siri lakini Pemba kama ijulikanavyo ni watu wenye ujasiri wa kubana kimya hadi wajue mwisho wake ,kwani polisi mmoja alieuwa kwenye maandamano ya january 2001 alitambulika kwa jina na alinadiwa mwizi na kuuliwa Unguja.Hivyo wanao mtandao unaowasaidia kwa kiasi fulani.Sababu watakayokuwa nayo Usalama wa taifa ni kuwaita wachochezi ,hiyo ndio sababu yao kubwa wanayoitumia huko Zanzibar kuwadhalilisha watu.Lakini kwa safari hii wasiachiwe kabisa haya mambo lazima yawe ya kufuatiliwa katika kiwango cha Kimataifa na kwa vile walishapeleka Barua UN hivyo Serikali ya Kikwete mpaka sasa tayari itakuwa na kesi ya kujibu.Vipi imewakamata watu usiku na kuwatorosha hadi Tanzania Bara ,Je Karume alikuwa na mpango wa kuwaua maana Karume Baba alikuwa na mpango wa kuwaua baadhi ya watu Mwalimu Nyerere akawavutia upande wake haraka.
 
kengeja_taxi.jpg
 
Ukiona serekali inashidwa kutatua mambo ya msingi na kumwiita Kizee cha siku nyingi Kingunge Ngombare Mwiru mwenye fikra za tangu ukoloni, ujamaa, ubepari na kwa sasa fikra za kifisadi kuongea na waandishi wa habari basi ujue kweli hawana sera. .. hapa sasa ndio wanataka kuigeuza pemba iwe kama iraq na kweli watu watajilipua.. Hapo ndipo unaona uwezo wa Muungwana ulivyo mdogo
 
"We are partners in democracy and believe that governments should respond to the people and are partners to fighting disease, extending opportunity and working for peace."

President Bush, you will recognise this as part of you speech when you were in Tanzania,you must be so embaressed by what JK and his government are doing now.
 
hebu subirini msiwe wa kuhukumu tu.

jee sheriA IMEVUNJWA? AU WAO HAWAWEZI KUHOJIWA NA WAKIHOJIWA HAKI ZA BINAADAMU ZIMEKIUKWA?
 
Kuhojiwa na kukamatwa ni vutu 2 tofauti..Kama watu wana dhana Njema hawawezi kuja usiku na Mtutu wa Bunduki...Kuhojiwa Gani hadi watu wapelekwe ZNZ kwa Ndege then warudishwe...

Tunachezea Aman ktk Pipa la Petrol...we will pay the price...

Wenzetu wa South Africa pamoja na Historia iliundwa Tume ya Desmond Tutu...Tume ya kurudisha Maelewano..
Kwanini isifanyike ZNZ kama inaonekana kuwa ktk historia kundi fulani lilidhulumiwa....!!!
 
CCM wanafanya makosa sana kwa kuwakamata wafuasi wa CUF nyakati za usiku kwa makosa ya kupeleka barua ya malalamiko kwenye Umoja wa Mataifa.

This is too much guys!
 
mmh... subirini J'tano; msikose makala yangu ya Jtano.. this is sad. Nilitaka kuandika kuhusu mafisadi naona tuzungumzie ya Pemba na kuyaweka kwenye maudhui yake.
 
NEWS ALERT: KWA WAPENDA AMANI NA ULINZI WA HAKI ZA BINADAMU.
Wananchi wa kisiwani pemba waliowasilisha waraka Umoja wa Mataifa (UN) wa kutaka shikirisho wameaza kujikuta ndani ya mikono ya polisi wa serikali kuazia jana usiku.katika waliokamatwa pamoja na ni Kiongozi wao bwana Ahmed Marshed Khamis.
Tafadhalini wanaJF huu ndio mwanzo wa mapambano na serikali za kidhalimu ,wahanga wa Demokrasia Tanzania wameanza kukamatwa tena nyakati za usiku.Wapemba ni watu ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuitetea haki ya Mtanzania kwa njia moja au nyengine wamewawezesha waTanzania wengine kuwepo mstari wa mbele katika kufichua maovu ya mafisadi ,huu ni wakati wa kuungana nao katika kuufichua udhalimu wa serikali ya Kikwete ..hawa ni waTanzania wenzetu tukinyamaza kwa hawa wachache basi watatumaliza mmoja mmoja.Peleka habari hizi kwenye vituo vyote vya habari vya U.N.
Mi nawaambia mafisadi wasipokamatwa kwanza then wao watatukamata sisi...

Mchawi ni to let them know kuwa you're aware of their uchawi..

Na mwizi anayejua kuwa wewe umeshamtambua then usipokamata yeye..Yeye takamata wewe na pengine kukuua!

Inanikumbushia ule usemi wa baba yake cube kwenye Friday ya kwanza...

Something about...." Its the dog gonna catching your ass and not you catch the dog!"

Hapo ni pale Ice Cube alipotaka kwenda kuanza kufanya kazi sambamba na baba yake ya kuwakamata MBWA!

I can see it clearly...If we dont catch the dog...Then the dog's gonna catch our asses!
 
Viongozi MAJAMBAZI WA CCM wanakuwaga haraka sana kuwakamata na kuwanyanyasa raia wasio na hatia ilihali kuna MIJAMBAZI mingi tu iko ndani ya Serikali yao inashindwa hata kuwahoji au wakufungulia mashitaka yeyote. Nadhani huu ni wakati kwa watanzania wote kuhakikisha haki inapatikana huko Pemba na manyanyaso dhidi ya raia wasio na hatia hayafanyiki. Watanzania wenzetu huko Pemba wameshanyanyaswa na kudhulumiwa vya kutosha, enough is enough.
 
mmh... subirini J'tano; msikose makala yangu ya Jtano.. this is sad. Nilitaka kuandika kuhusu mafisadi naona tuzungumzie ya Pemba na kuyaweka kwenye maudhui yake.

Samahani wakulu!
Sikujua kuwa hii thread haihusiani na ufisadi!
Hii ni kutokana na hii....
NEWS ALERT: KWA WAPENDA AMANI NA ULINZI WA HAKI ZA BINADAMU.
Wananchi wa kisiwani pemba waliowasilisha waraka Umoja wa Mataifa (UN) wa kutaka shikirisho wameaza kujikuta ndani ya mikono ya polisi wa serikali kuazia jana usiku.katika waliokamatwa pamoja na ni Kiongozi wao bwana Ahmed Marshed Khamis.
Tafadhalini wanaJF huu ndio mwanzo wa mapambano na serikali za kidhalimu ,wahanga wa Demokrasia Tanzania wameanza kukamatwa tena nyakati za usiku.Wapemba ni watu ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuitetea haki ya Mtanzania kwa njia moja au nyengine wamewawezesha waTanzania wengine kuwepo mstari wa mbele katika kufichua maovu ya mafisadi ,huu ni wakati wa kuungana nao katika kuufichua udhalimu wa serikali ya Kikwete ..hawa ni waTanzania wenzetu tukinyamaza kwa hawa wachache basi watatumaliza mmoja mmoja.Peleka habari hizi kwenye vituo vyote vya habari vya U.N.

Kwa mara nyingine naomba nijulishwe kama posting yangu iliyppita iko nje ya mada hii!

Ahsante
 
Haki ya kujitenga (right of secession) ni miongoni mwa haki za msingi za binadamu, mradi iwe imedaiwa kwa msingi wa amani na uamuzi kufikiwa kwa njia za kidemokrasia (mfano referrendum). Hawa wapemba mpaka hapo walipodai haki hiyo hawajakosea chochote, hakuna hata chembe ya uhaini. Ingekuwa uhaini kama wangechukua silaha na kujitangazia jamhuri yao kwa nguvu, au wangeeleza nia ya kutwaa serikali kwa nguvu. Lakini hawa wameandika tu barua na kupeleka katika mamlaka ambayo jambo kama hilo linaweza kujadiliwa, na ambako haki hiyo imetamkwa, ambako ni Umoja wa Mataifa. Kuwaita hawa wahaini na kuanza kuwatisha kwa kuwasomba kwenye madege ya kijeshi kwenda kuwahoji Unguja ni udikteta wa hali ya juu, ni kuwazuia kueleza mawazo yao, jambo ambalo ni kinyume kabisa cha haki za binadamu. Serikali ya CCM inapaswa kuacha kutenda udikteta wakati inahubiri demokrasia.
 
Back
Top Bottom