Wapemba Waanza Kukamatwa

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,743
NEWS ALERT: KWA WAPENDA AMANI NA ULINZI WA HAKI ZA BINADAMU.
Wananchi wa kisiwani pemba waliowasilisha waraka Umoja wa Mataifa (UN) wa kutaka shikirisho wameaza kujikuta ndani ya mikono ya polisi wa serikali kuazia jana usiku.katika waliokamatwa pamoja na ni Kiongozi wao bwana Ahmed Marshed Khamis.
Tafadhalini wanaJF huu ndio mwanzo wa mapambano na serikali za kidhalimu ,wahanga wa Demokrasia Tanzania wameanza kukamatwa tena nyakati za usiku.Wapemba ni watu ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuitetea haki ya Mtanzania kwa njia moja au nyengine wamewawezesha waTanzania wengine kuwepo mstari wa mbele katika kufichua maovu ya mafisadi ,huu ni wakati wa kuungana nao katika kuufichua udhalimu wa serikali ya Kikwete ..hawa ni waTanzania wenzetu tukinyamaza kwa hawa wachache basi watatumaliza mmoja mmoja.Peleka habari hizi kwenye vituo vyote vya habari vya U.N.
 
NEWS ALERT: KWA WAPENDA AMANI NA ULINZI WA HAKI ZA BINADAMU.
Wananchi wa kisiwani pemba waliowasilisha waraka Umoja wa Mataifa (UN) wa kutaka shikirisho wameaza kujikuta ndani ya mikono ya polisi wa serikali kuazia jana usiku.katika waliokamatwa pamoja na ni Kiongozi wao bwana Ahmed Marshed Khamis.
Tafadhalini wanaJF huu ndio mwanzo wa mapambano na serikali za kidhalimu ,wahanga wa Demokrasia Tanzania wameanza kukamatwa tena nyakati za usiku.Wapemba ni watu ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuitetea haki ya Mtanzania kwa njia moja au nyengine wamewawezesha waTanzania wengine kuwepo mstari wa mbele katika kufichua maovu ya mafisadi ,huu ni wakati wa kuungana nao katika kuufichua udhalimu wa serikali ya Kikwete ..hawa ni waTanzania wenzetu tukinyamaza kwa hawa wachache basi watatumaliza mmoja mmoja.Peleka habari hizi kwenye vituo vyote vya habari vya U.N.

People should not be afraid of their governments. Governments should be afraid of their people.
 
Kosa kubwa zaidi dhidi ya Jamhuri yetu ni uhaini siyo kutoa maoni ya kupinga au kutaka kujitenga. Mtwara wamewahi kusema hivi, Kidoma wamewahi kusema hivyo na kuna watu wa kanda za ziwa wamewahi kutoa matamshi kama hayo ya kuonesha kuchoshwa na kusahauliwa.

Kwanini wanatumia mkono wa nguvu namna hii dhidi ya Wapemba?
 
Jamani Muungwana, Chonde chonde hii mijamaa inaweza kuanza kujilipua!!!!!

Jadiliana nao tu wataelewa!
 
mmmh, pemba si kama sehemu nyengine za Tanzania kwa sababu kule ni upinzani tu uliochaguliwa. hivyo basi, seriali ya ccm haiwachukulii kama ni raia wake.
huyo Ahmeid Marshed Khamis ni mtu anakaribia miaka 70. atampindua nani?
 
Waliokamatwa wengi ni wazee wakiongozwa na mzee Ahmed Marshed Khamis, ambaye anatajwa kuwa alikua Kiongozi wa watu waliokwenda katika Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) Jijini Dar es Salaam kuwasilisha waraka wa barua wakidai serikali shirikishi Kisiwani Pemba.

Wengine ni: Dk. Gharib Omar Gharib, Jirani Ali Hamad, Bi. Mariam Hamad Bakar, Bi. Hidaya Khamis Ally, Mzee Salim M. Abeid, na mzee Mohamed Mussa, na wote wamechukuliwa na kupelekwa Zanzibar kwa ndege ya jeshi na hatimaye Dar es Salaam. Polisi wamekanusha kufahamu lolote, na kazi hiyo inafanywa na maofisa Usalama na Maofisa wa JWTZ kutoka Bara wakishirikiana na wenzao wa Unguja
 
Hii sasa ni danger taa nyekundu imewaka CCM wamezidiwa sasa.Wakubali tu sasa hii
 
tanzania ni nchi ya majaabu, na hii inatokana na utawala mbovu wa ccm.
ingekuwa pemba, walishughulikiwa kidogo tu kama sehemu ya zanzibar basi haya yasingetokea.
na kama ccm bara inashindwa kuithibiti ccm zanzibar, whats the point ya kuwa ndani ya chama kimoja?
kikwete hili lipo mikononi mwako, na wewe mwaga damu kama ilivyomwagwa enzi za mkapa. its your turn. we will get to know how much of a mchamungu you are. au ndo kharam nguruwe tu na pombe?
 


Ndugu zangu wanaforum mimi napenda kwanza kuunga mkono hoja za wapemba za kutaka kujitenga . kwa nini naunga mkono?
 1. Kwanza serikali ya Mapinduzi haiwatambui Rasma kama ni raia sawa wa Zanzibar wenye haki sawa kama wenzao wa Unguja
 2. Pili serikali ya Zanzibar yenyewe mara zote imesema na hakuna amekanusha ya kwamba haiwezekani kwa MPEMBA kuongoza serikali ya Zanzibar
 3. Haya yamekua yakitamkwa ndani ya Baraza la wakilishi , mikutano ya hadhara na hakuna asojua mpaka juzi ndani ya mkutano wao wa Butiama wamesema wazi
 4. Nafasi zote za serikali ya Zanzibar zimeshikiliwa na watu wa unguja japo wapemba wapo wengi wenye uwezo
 5. Hakuna Mpemba katika baraza la mapinduzi
 6. Nafasi zote za masomo ya juu zinakwenda kwa watu wa Unguja na CCM
 7. Kuna hujuma za makusudi zimefanywa dhidi ya wapemba kuwadhuru kama kisa cha kutiliwa sumu kule pemba
 8. Ingawa serikali ya Muungano huwa inawavumilia Wapemba kwa kuwapa nafasi muhimu kama DR. Shein na Salim Ahmed na Dr, Omar wote walikua ni wakuonyeshWa mfano katika uongozi wa nchii hii hawa HAWANA hata chembe ya UFISADI lakini subutu huyu Shein aseme tu nataka mimi kugombea Urais wa ZANZIBAR HATA FORM HATOPEWA NA CCM UNGUJA
 9. Haya ya ubaguzi na ufashisti maaana huuu ni ufashisti kubagua raia wako kuwa ni watu wa daraja la pili
 10. Haya yakifanyika Huko za Zanzibar Dhambi kubwa ni kwa Serikali ya Muungano kutojali na kuvumilia hali hii ya CCM wenzao Unguja la ajabu wao Bara hawana Tabu na WAPEMBA
 11. KUNA SABABU NYINGI ZA JAMAA ZETU KUJITENGA
 12. UNAPOMWAMBIA MTU NDANI YA NCHI YAKE KWAMBA WEWE MPEMBA HUWEZI KUTAWALA NCHII HII BASI MAANA YAKE HUWATAKI BORA WAWE MBALI NA WEWE YAANI TAYARI UMEWAPA RUHSA KAMA WANATAKA KUJITENGA BASI RUHSA
 13. WATU WANASEMA KWA NINI WAPEMBA HAWAJENGI KWAO WAKATI WANAUWEZO? LAKINI JAMANI NI SERIKALI NDIO INTAKIWA IPELEKE MAJI . UMEME BARABARA , BANDARI , AIRPORTS NA MASHULE KAMA WAFANYAVO UNGUJA
 14. KUNA VISA VINGI VYA KIBAGUZI KUNA JAMAA ALITAKA KUFUNGUA HOSPITAL KUBWA PALE WETE MSAADA WA KUTOKA NJE AKANYIMWA KIBALI ATI ASAIDIE ZILIZOPO
 15. KUNA WATU WALITAKA KUJENGA BARABRA YA GANDO KWENDA WETE SERIKALI IKAKATAA MPAKA LEO GARI HAZIPITI WATU WATEMBEA KWA MIGUU
 16. HATA USAFIRI WA BAHARINI UNAPIGWA VITA KWENDA KATI YA PEMBA , MOMBASA NA TANGA ILI WAPEMBA WASIFAIDI KUJIENDELEZA
 17. KUNA WAKATI BEI YA PETROL PEMBA ILIKUA CHINI KULIKO UNGUJA , HII NI KUTOKANA NA SOKO HURIA BAI IKAAMULIWA IPANDISHWE IWE SAWA NA UNGUJA HUU NI UBAGUZI WA HALI YA JUU
 18. PEMBA MARA NYINGI KUNA TOKEA UKAME NA HALI YA NJAA IKITOKEA HAKUNA WA KUWASAIDIA SERIKALI YA UNGUJA HAIJALI BALI HUTOA KEJELI HATA SERIKALI YA MUUNGANO NAYO HUKAA KIMYA IKITOKEA NJAAA SEHEMU NYENGINE BASI HARAKA MISAADA INA PELEKWA
 19. MIAKA YA NYUMA WAPEMBA WALIKUA WANASAFIRI KUTOKA TANGA KWENADA PEMBA HALI YA HEWA ILICHAFUKA BASI WAKAPIGA SOS YA KUOMBA MSAADA NA WALIPIGA RADIO CALL IKAPOKELEWA LAKINI HAWAKU PATA MSAADA NA ROHO ZAO 25 ZIKAPOTEA KISA ATI BOTI ZA KMKM HAZIKUA NA MAFUTA
 20. WAKATI PEMBA KUKIWA NA NEEMA YA CHAKULA WATU WA PEMBA HUUZA KWA WINGI CHAKULA CHAO KWA NGUGU ZAO WA UNGUJA LAKINI PEMBA KUKIWA NA NJAA BASI WAPEMBA HAWARUHUSIWI KUPELEKA CHAKULA KUTOKA UNGUJA HII NII AIBU
HIVYO WANAZO SABABU NA NIA YA KUJITENGA WAO NI BINAADAMU NA WAMESOMA VYA KUTOSHA KUENDESHA NCHI YAO KAMA WAPEMBA .CCM TAYARI IMESHAWAFUKUZA KWA HIYO WAO WANATAMKA TU KWAMBA JAMANI WENZETU TAYARI WAMETUTOA KATIKA SERIKALI HIVYO TUNAKAA KWETU NA SERIKALI YETU MAANA KATIKA HIO HATUNA NAFASI SASA HUUUU SII UHAINI
 
Mie naunga mkono kwa wapemba kujitenga, kama hali ya huko ni mbaya namna hiyo. yaani kama hakuna basic needs na wanakataliwa na wenzao wa Pemba na kuona kama ni wakuja, basi wajitenge. Kuna maana gani, yaani inakuwa kama wa Pemba ni kama vibarua tu na wakulima. Waachieni basi hata karafuu yao wauze wenyewe. Wamechoka ndio maana wakaamini kuwa CUF kama chama kinaweza kuwaletea uhuru wa kiuchumi na unafuu vilevile. Kwani kama CCM wangepeleka basic needs unafikiri hawajamaa wangetamka kujitenga? Mbona wakazi wa Dar hawajatamka kujitenga, ni wakazi wa Kigoma,Mtwara na huenda hata Songea na Rukwa watakuja tamka hayo maneno. Wapeni haki halafu mtaona kama watatamka hayo maneno ya ``uhaini``
 
MIMI NAPENDA TUWAULIZE MAKAMBA , KIKWETE , KARUME NA KINGUNGE TUCHUKULIE CUF WAMEKUBALI HIO KURA YA MAONI KUHUSU MUSTAKBALI AU AINA YA SERIKALI WANAYOTAKA WATU WA ZANZIBAR . SASA TUSEME SWALI LA KURA YA MAONI LITAKUW " JEE UNAKUBALI KUUNDWA SERIKALI SHIRIKISHI ITAYOPATIKANA BAADA YA UCHAGUZI WA ZANZIBAR ILI KUWEKA UWIANO WA KIUTAWALA"
JEE SERIKALI YA CCM , MAKAMBA .KINGUNGE KARUME WATAKUA UPANDE GANI WA KURA YA MAONI ??????? WATAWAMBIA WANA CCM ZANZIBAR WAKUBALI SERIKALI SHIRIKISHI AU WATAWAMBIA WAKATAE?????????? NAOMBA MAONI YAO . NAOMBA KIKWETE , MAKAMBA NA KINGUNGE ATUJIBU. MAAANA IPO WAZI CUF WAO WATASEMA TUNAKUBALI JEE CCM UPI UTAKUWA MSIMAMO WAO KWENYE KURA YA MAONO ?????////
 
Nafikiri hili suala litamaliza kabisa heshima ya muungwana Jk katika medani ya kimataifa. Sasa atasolve je maswala ya Zimbabwe?
 
mh! kwa jinsi ninavyofahamu, kuwakamata hawa wazee kutazidi kuwasha moto, kwa kjuwa the rest of wapemba na watanzania kwa ujumla wataona hawa kama makomredi na hii ndiyo mwanzo wa safari ya wapemba kusaka taifa lao, mkoloni wao sijui atakuwa ni unguja au kikwete
 
watu wanaowaambia wapemba waache kujenga kariakoo majumba ya mamilioni wakajenge pemba nafikiri wanashindwa kuelewa hali halisi ya pemba.
1) mtu akajenge pemba mtaji wake ikisha kuwe hakuna umeme wala maji?
2) biashara yake ataifanya vipi wakati hakuna airport ya maana pemba?
3) barabara pia mbovu, mtu kweli anaweza kuendesha biashara pemba ?

si kama wananchi wa pemba hawajitolei kwa kile wanachoweza, kuna volunteer organizations nyingi tu ambazo zinachangiwa pesa na hao hao wafanya biashara na raia wa zanzibar walioko nje ya nchi.....mfano mmoja ni wa utibabu.
kuna camps za utibabu zimeanzishwa ambapo madaktari huenda pemba kwa kujitolea na kuhudumia wananchi wa kule bure.

kuna miradi ya maji ya vijijini ambayo ilichangiwa na wananchi wa pemba na jamaa zao amabyo imepunguza ingawa kidogo adhabu ya maji kwa baadhi ya vijiji vya pemba

kuna miradi ya kujitolea ya kupeleka walimu katika mashule ya pemba, ambayo pesa inatoka mifukoni mwa watu wa kawaida.

mtu hujiendeleza kwa anapoweza yeye, lakini maendeleo hasa ya pahala hupelekwa na serikali.

maji, umeme, miundombinu, matibabu, walimu ni mifano tu ya mambo ambayo ni wajibu wa serikali.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom