Basi la Abood lagongana na IST wakati dereva 'aki-overtake', Watu wanne wafariki Dunia

Basi la Abood lagongana na IST wakati dereva 'aki-overtake', Watu wanne wafariki Dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,316
Reaction score
15,806
TAARIFA,AJALI JIJINI DAR ES SALAAM.webp
TAARIFA,AJALI JIJINI DAR ES SALAAM (1).webp

TAARIFA KWA UMMA
AJALI YA BASI KUGONGANA NA GARI NDOGO NA KUSABIBISHA VIFO VYA WATU 04 NA UHARIBIFU WA MAGARI
​
Tarehe 07 Septemba, 2026 saa 07:40 usiku katika barabara ya Bagamoyo eneo la Bunju Sokoni Kinondoni Dar es Salaam basi lenye namba T 235 EMJ aina ya Yutong mali ya Kampuni ya Abood iliyokuwa ikiendeshwa na Christivian Steven Shemuhilu Miaka 38, mkazi wa Kange Tanga likitokea Tegeta kuelekea Bunju kwa safari ya kwenda Mkoani Tanga iligongana na gari namba T 274 ERU aina ya Toyota IST iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Hamad Mohamed Juma Majid miaka 37, Mkazi wa Mtoni Mtongani Dar es Salaam.

Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi kuyapita magari mengine "Overtake" bila ya kuchukua tahadhari ya watumiaji wengine wa barabara na kusababisha vifo vya, Hamad Mohamed Juma Majid miaka 37, Mkazi wa Mtoni Mtongani Dar es Salaam, Edward Kimanyara, mstaafu, mkazi wa Yombo Dovya Temeke Dar es Salaam, Magdalena Manyenga, miaka 45, mkazi wa Temeke Dar es Salaam na Melina Emmanuel Kayoka miaka 42, mkazi wa Yombo Kisiwani Temeke Dar es Salaam. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala Kinondoni Dar es Salaam.

Dereva wa basi namba T 235 EMJ aina ya Yutong anashikiliwa kwa hatua nyingine za kisheria.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watumiaji wote wa barabara wakiwepo waendesha vyombo vya moto kuendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuzuia na kuepusha ajali.

Imetolewa na;-
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi,
Dar es Salaam.

​
Pia soma:
~ Abood mnatukosea sana Abiria wenu
~ Abood wametukomesha, safari ya Dar – Mbeya imechukua Saa 24, wana huduma mbovu kwa wateja
~ Basi la Abood lakamatwa na kilo 101.2 za mirungi, eneo la Tegeta Kibo
 
Watu wanne wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili katika barabara ya Bagamoyo, eneo la Bunju Sokoni, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo imetokea saa 7:40 usiku, baada ya dereva wa basi la Abood lenye namba T 235 EMJ aina ya Yutong kuligonga gari lenye namba T 274 ERU aina ya Toyota IST lililokuwa likielekea mkoani Tanga.

Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi ambaye alikuwa akilipita gari lingine bila kuchukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.

Waliofariki katika ajali hiyo ni Hamad Mohamed Juma, Edward Kimanyara, Magdalena Manyenga na Melina Emmanuel Kayoka, huku miili yao ikihifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

Dereva wa basi hilo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria, huku Jeshi hilo likiwataka madereva kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kupunguza ajali.
SaveClip.App_799250344_18561660175074085_3898569625844075909_n.jpg
SaveClip.App_799634296_18561660184074085_8999669637747848812_n.jpg
 
Madereva wengi wa mabus
Ni vichaa ujuaji mwingi
Sasa njia ya bunju,njia 2
Nayo ya ku overtake na mspeed

Ova
Nimesema jana ajali zetu Bus linaua 20km kutoka kituo cha bus aisee ni kama wamerogwa sio bure wao wanakuletea gari ili wewe utoe usipojiongeza ndio mtihani huo na anagonga huku anaona gari ya mbele inakuja kasi hawezi hata kusimama ili kupunguza ukubwa wa ajali au wote wawili wasimame..
 
Kampuni ya usafirishaji abiria ambapo iko miaka mingi na ikijikita Ubungo mpaka Morogoro , yenye rangi damu ya mzee.

Kampuni hi inamilikiwa na mwanasiasa na madereva wake wana kiburi sana, huwa wanaendesha nakuingiza mitaroni sanan wenye malori na gari ndogo. natanua, akiona uso-kwa- uso anachomekea na hapo kama upo speed ukikwepa unaingia mtaroni yeye anatembea. Kama alikuwa slow utapona.

Pale Bunju, Hii kampuni yenye rangi damu ya mzee alitanua kupita magari 10, akakutana na IST, kaua abira wote wa IST, alafu anaenda mahakamani kulipa faini ya Elfu 50 tu.

Ifike pahala, wananchi wagomee kampuni zinazowatoa kafara!
 
Back
Top Bottom