Kuhusu kuvuruga ndoa ya Amina na Medi, mtu wa kumpa lawama zaidi nadhani ni yule Naibu Waziri aliyemwita Medi na kumshawishi amwache mke wake. Tumekua tukifundishwa kuwa ugomvi wa mme na mke usiuingilie, lakini bwana huyu aliingilia mambo ya unyumba wa wengine. Kama angekuwa na nia njema, angemwonya Amina kabla ya kufikisha taarifa hizo kwa mumewe.
Mkandara.
Mkandara unajua future ya Amina ameharibu huyu mpuuzi? wewe kama Amina angekuwa dada yako ungejisikiaje?
Masatu, sijui kuhusu wewe, lakini hilo la kumwingiza mama wa watu halina udhuru. Kama mswahili anataka kumtukana Mwanakijiji amtukane, kama anataka kumtukana Zitto amtukane, kama anataka kunitukana mimi na anitukane. Kwa sababu mimi nami ni mwanachama hapa JF. Kama huyo mama angempa sababu ya kumtukana au kufanya kitu ambacho kingemlazimisha atukanwe hapa hilo tungelijadili, viongozi wa dini ni fair game (matatizo mengi hapa duniani yametokana na imani hizo!), viongozi wa kisiasa (ni fair game), mabalozi ni fair game.. hata hivyo mama zao au watu wa familia zao ambao hawana hatia kwanini wawe sehemu ya mjadala? Mama Mkapa anajadilika kwani kuna issue, Mama Salma anajadilika kwani kuna issue...Regina wote wanazungumzika.
Hadi hivi sasa sijaona ni kwa nini mama Zitto amekuwa somo kisa cha makosa ya mwanae?
Masatu,
Nitukane mimi, sawa. Mtukane kiongozi, sawa. I draw the line inapofikia kwa mama yangu. Hapo nitakuvulia shati na kukunja misuli.
Masatu,
Nitukane mimi, sawa. Mtukane kiongozi, sawa. I draw the line inapofikia kwa mama yangu. Hapo nitakuvulia shati na kukunja misuli.
kwa hiyo wewe unafikiri vipi kuhusu kitendo cha Mswahili kumuingiza mama Zitto kwenye suala lisilohusika na kujaribu kumzulia mambo yasiyo ya kweli, ati jina la Zitto ni kutoka kwa mamake na ya kuwa mama yule hakanyagi Dar?!
Haya ndio maajabu ya Jamboforums, wametukanwa marais wote wa Tanzania Nyerere, Mwinyi, Mkapa JK, mawaziri wakuu, mawaziri. Dini zimetukanwa mitume wameitwa malaya Mabalozi wameambiwa wamebaka na kila ya aina ya kashfa zimo humo. Hakukuwa na wito wa karipio, adhabu au kufungiwa.
Kwa bahati mbaya limemkuta kiongozi wa chama "M-badala" sitoshangaa mapendekezo yakafanyiwa kazi, why not after-all yametoka kwa kada Kitila.
Naomba nieleweke sitetei watu kutukanwa, kudhalilishwa nk bali consistency and equal treatment kwa watu wote bila kujali background za vyama vyao, makabila, dini, jimbo nk.
As we have broke the principles now the principles have found a way of breaking us....