Habari za masiku tele ndugu zangu.
Nimeona ni muhimu niingie katika mjadala huu ili niweze kuweka wazi baadhi ya facts zisaidie mjadala wetu.
Mshahara wa Mbunge kwa mwezi Tshs. 1,200,000. Kodi inakatwa asilimia 30 ambayo ni sawa na Tshs. 360,000. Kwa wale ambao wamechukua mkopo wa magari kila mwezi analipa Tshs. 500,000. hivyo pato la mbuge baada ya makato ni Tshs 340,000.
Posho ya ubunge
Hii tunapewa shs 1,000,000 kila mwezi. pesa hii ni kwa ajili ya huduma za ubunge kama mawasiliano, kulipa wasaidizi, kuganya utafiti kwa ajili ya miswada na pia mafuta. Mafuta tunalipwa kwa sasa lita 500 kwa mwezi kwa wastani wa shs 1000 kwa lita.
Posho ya kujikimu na vikao
katika hili tunalipwa shs 55,000 tunapokuwa dodoma kwa ajili ya malazi na chakula. kuna habari kuwa tunapewa nyumba dodoma, sio kweli bali kila mbunge anatafuta makazi yake.
mbunge akihudhuria kikao cha bunge analipwa shs 70,000 kwa kikao. hivyo kwa wale wanaohudhuria kwa siku ni 125,000.
maombi ya wabunge:
wabunge walitaka kulipwa zaidi pesa ya mafuta ili iendane na bei ya mafuta na pia kulingana na ukweli kuwa baadhi ya wabunge majimbo ni makubwa sana na hivyo lita 500 kwa mwezi ni kidogo. mfano, mimi kutoka dodoma mpaka kigoma kwenda na kurudi ni km 1100 hivi.
pili, wabunge walitaka kuongezewa uwezo wa kuajiri wasaidizi wenye elimu kubwa zaidi. mfano mimi msadizi wangu ambae ana shahada ya sheria ninamlipa shs 500,000 kwa mwezi. kwa malipo ya sasa ninatakiwa kulipa shs 70,000 kwa mwezi.
mimi sijajua kwa malipo ya sasa yaliongozeka ni kiasi gani kitakwenda kwa mishahara na maeneo mengine. hivyo siwezi kucomment na kusema nini.
ukweli ni kwamba mjadala wa malipo kwa wabunge vs matunda ya kazi zao ni mjadala muhimu sana. lengo liwe ni kuzuia malipo makubwa bila tija na pia kuepuka kuwa na wabunge wasioweza kufanya kazi sawasawa ya kuisimamia serikali