Wanawake wenzangu mnawezaje kumsamehe a cheating husband?

Wanawake wenzangu mnawezaje kumsamehe a cheating husband?

Huyo aliye cheat hapo mwenyewe Hana amani Tena mke akimpuuza atakuwa anajishtukia shtukia tu hamwamini mkewe
Hawezi kumwamini lazima ajishitukie tu, naye aumie aone machungu, halafu hapo utakuta anatetewa na wazinzi wenzie
 
Nilivyokusoma ili upone inabidi upate side lover ulipize kiasi. Ukimaliza ndiyo muanze maisha upya na mumeo. Tofauto na hapo utaishia kupata depression na hiyo ndoa itakufa kifo kisichofufuka.
 
Hivi kuna tofauti gani kati ya mke wa kwanza na mke wanne ? Sasa kivipi uke wenza uwe ujinga tena bibie ?

Uzuri wanawake kama nyinyi mkiingia tu kundini mnakuwa marafiki sana, yaani mke wa nne anakuwa na ushoga na mke wa tatu,huwa raha sana.
Tofauti ipo Sana maana hzo ndoa za mitala ni za waswahili kutwa kugombana tu na uswahili ka wake wa mzee Yusuph, kina Queen darling.
Mimi staki ushoga na mtu yoyote Wala mazoea kabisa
 
Nilivyokusoma ili upone inabidi upate side lover ulipize kiasi. Ukimaliza ndiyo muanze maisha upya na mumeo. Tofauto na hapo utaishia kupata depression na hiyo ndoa itakufa kifo kisichofufuka.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tofauti ipo Sana maana hzo ndoa za mitala ni za waswahili kutwa kugombana tu na uswahili ka wake wa mzee Yusuph, kina Queen darling.
Mimi staki ushoga na mtu yoyote Wala mazoea kabisa
Siyo kweli, labda kama hujui historia, suala la sisi kuwa na wake wengi ni suala la tangu na tangu.

Suala la kugombana si uswahili ni tabia ya mtu, kwani wapo wanao gombana nje ya jambo letu hili. Wa ila zipo ndoa kibao za uke wenza kuna heshima na adabu, na hasa mwenye wake ukiwa imara.
 
Tofauti ipo Sana maana hzo ndoa za mitala ni za waswahili kutwa kugombana tu na uswahili ka wake wa mzee Yusuph, kina Queen darling.
Mimi staki ushoga na mtu yoyote Wala mazoea kabisa
Mapenzi hayagawanyiki hata siku moja
 
Muono wa kiPoyoyo, kimbulula, na kipuuzi mwingine huu! Hivi huu ujuha mnautoaga wapi? Aliyekuambia ndoa za wazungu zinadumu ni Nani!? Au ndio kusema unaangalia Sana sinema za kizungu na kuziamini! Toa upumbafu wa kipuuzi kiasi hicho! Ndoa haiangalii rangi ya ngozi Bali utayari wa dhati kutoka moyoni wenye upendo wa dhati! Ktk Hilo, upendo huvumilia yote, haukosi Kuwa na adabu,nk! Hayo matongotonga ya kishamba kuamunishwa wazungu sijui hivi...Mara hivyo uyanawe na yakitokea!
Kwa huyu dada, Kama anapenda kweli mumewe, Basi amsamehe, aongeze bidii ya kumlinda mumewe kwa kumuombea, kujitoa kwa mumewe zaidi! Kibri na dharau na hasira zitamharibu zaidi mumewe na ndoa kwa ujumla!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan mkewe amlinde mumewe kwa kipi? Ili iweje? Km mwenyewe mtu mzma hawez jilinda ndo mwingne ataweza? Kila mtu ashinde match zake.
 
Tofauti ipo Sana maana hzo ndoa za mitala ni za waswahili kutwa kugombana tu na uswahili ka wake wa mzee Yusuph, kina Queen darling.
Mimi staki ushoga na mtu yoyote Wala mazoea kabisa
Pili, suala la ushoga huwa linakuja tu "automatically" tu unastukia umekuwa rafiki kipenzi wa mke mwenzako.
 
Huyo aliye cheat hapo mwenyewe Hana amani Tena mke akimpuuza atakuwa anajishtukia shtukia tu hamwamini mkewe
Baada ya kusoma komenti zako nimegundua vitu viwili au vitatu. .....1;unawachukia sana wanaume kwa sababu you've been in failed relationship 2:upo single na jua limeshazama, 3;, profile pic sio yako.
 
kwanza elewa tuu sisi wanaume hatujaumbiwa mwanamke 1.kumbuka pia hata akicheat nje mapenz kwako hayataisha wala hatapunguza matumiz na watoto watasoma.ndio udhaifu tulio nao km nyie pia mna udhaifu wenu ingawa hamjielewi.unachofanya au kukosea ni kukosa apetite na huyo mmeo hilo ni kosa cha msingi wee mbadilishie style zile ambazo hamjawai kufanya yaani kiufupi ubadilike na usimtuhumu kwa chochote au kuonyesha hisia mbaya.mpende hivyo hivyo mpikie chakula kizuri umkaribishe kwa unyenyekevu badili mazingira yote ya mazoea!mfanye aone nyumbani ulipo wewe ni vantage point yake akute vitu ambavyo tofauti na anapochepukia na sio kumfanya ajione dhaifu kwa tuhuma unazompa.yaani mfanyie vitu ambavyo ataona siku zote alikuwa wapi kukufahamu.sisi wanaume akili yetu ndogo kututeka ni rahisi mno km kumpiga teke chura.soma hata majarida au tafuta watalam wakueleweshe jinsi ya kumkamata mume ili miaka yote aone hakuna mke km wee na sio kuonyesha chuki wazi waz au kuzira
Acha Uzinzi ni kujiendekeza na kutokuwa na kazi za kutosha unapata muda wote huo wa kuwa na wanawake zaidi ya mmoja.Wanaume wanaochiti wanakuwa maskini,wanakuwa na magonjwa yasiyoeleweka na kiroho hawaishi muda mrefu katika ulimwengu huu .Chunguza na wewe mwenyewe unayechti jichunguze na sio wanaume tu hata wanawake.Mnajiingizia maroho msiyoyajua kwenye miili yenu iliyo safi.Mungu alimwumba mwanamke na mwanaume basi.
 
Mwenzenu yamenikuta na kusema za ukweli nashindwa kabisa kuelewa namna ya kutoka hapa na kusonga mbele.

Ni mume nilompenda sana sana sana. Mungu katujaalia two beautifull kids na mengine ambayo am greatfull for. Tuliishi kwa upendo,furaha na amani hadi miezi 8 ilopita nilipogundua kuwa nilivyomdhania mume wangu sivyo alivyo.

Kwakuwa nampenda na kumfahamu sana mume wangu, kuna kitu nilikuwa tu nakihisi hakiko sawa kwa muda. Baadae nikagundua he was cheating. Yaani sitaki kuelezea mstuko niloupata na jinsi ninaumia jamani. Japo aliomba sana msamaha and all that ila moyo wangu umekufa ganzi wapendwa.

Mume nilompenda sana kwasasa namuona kama jirani yangu tu, hata hamu nae sina kabisa na hata tendo la ndoa ni kama ananibaka tu. Tushaongea sana, tushakwenda hadi vacation sie wawili tu ila sioni kinachobadilika. Akisafiri kikazi au mimi nikisafiri najisikia amani zaidi and i dont miss him kabisa.

Kuna wakati nilimuomba some alone time nifikirie kuhusu mustakabali wa hii ndoa, alinipa huo muda na kwa kipindi hicho cha wiki moja kichwani mwangu nilishangaa kunazunguka watoto wetu tu na sio mume wangu. Sijamueleza mtu yeyote kuhusu hili hata mama yangu wala mshenga wetu ila linanitafuna hatari.

Wenzangu mnawezaje kusamehe wanaume wanaowacheat na kurudi katika hali zenu za kawaida? Maana mie kwasasa mume wangu namuonaje sijui, nae naona hali hii inamtesa ila ndio hivyo tena[emoji134]
Sijisikii kumpenda wala kumheshimu tena, naona kama hadeserve kwa kutokuithamini na kuivuruga ndoa yetu.
Nilichokielewa hapo haumpendi. Sasa nenda kaombe talaka uwe huru vinginevyo utarevenge vibaya sana kwa chuki uliyo nayo kuwa huru na amani ya bwana ikuzunguke kafile talaka tu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan mkewe amlinde mumewe kwa kipi? Ili iweje? Km mwenyewe mtu mzma hawez jilinda ndo mwingne ataweza? Kila mtu ashinde match zake.
Walioanzisha ndoa ndio husema hivyo😂🤣😂🤣😂!
👇
Yeremia 31:22” hata lini utatanga tanga , Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani, mwanamke atamlinda mwanaume”.

Soma pia habari hii yote katika Isaya 32:9-17



Ule mstari wa tisa unasema “Inukeni enyi wanawake wenye raha, sikieni sauti yangu; enyi binti za watu wasiokuwa na uangalifu,tegeni masikio yenu msikie sauti yangu”.



Moja ya majukumu makubwa ambayo Mungu amemkabdihi mwanamke ni jukumu la ulinzi kwa mwamamumue yoyote na si mumewe tu kama wengi wanavodhani au kufikiri
. Kwa maana hili andiko linawahusu wanwake haijalishi wameolewa au la, ni binti au mjane linamhusu.



Si wanawake wengi wanaoifahamu siri hii juu yao. Imeandikwa ya kwamba Mungu ameumba jambo jipya, mwanamke atamlinda mwanaume. Hii ina maana ulinzi wa mwanaume uko kwa mwanamke. Hii inaashiria kumbe Mungu ameweka neno la ulinzi wa mwanaume kwa mwanamke.



Hebu tuangalie mifano kadhaa ndani ya Biblia;



" style="max-width: 100%; display: block !important;"> Kuzaliwa kwa Musa, Kutoka 2;1-10.

Tunaona wazi kabisa mama wa Musa alivyomlinda mwanae akijua ndani yake kuna kusudi limebebwa.

" style="max-width: 100%; display: block !important;"> Kuzaliwa, kukua na ndoa ya yakobo, Mwanzo 25:21-28, 27:1-4, 5, 6, 11-13, 17, 46.

Siri ya kusudi la Mungu hapa duniani kupitia Yakobo aliiweka kwa mamaye. Alimweleza maana ya vita iliyokuwa ikiendelea tumboni mwake alipokuwa mjamzito. Rebeka alihakikisha kusudi la Mungu juu ya watoto atakaowazaa linatimia, kwa sababu alijua Yakobo ndiye taifa kuu alihakikisha hilo linatimia na pia alihakikisha Yakobo haoi nje ya mpango wa Mungu kwa maana ya kuoa mataifa.

" style="max-width: 100%; display: block !important;"> Kuzaliwa na maisha ya Samson, waamuzi 13:2-5, 12-15.

Siri ya nini Mungu amekiweka kwa Samson na kwa nini anamleta duniani, pamoja na namna mtoto huyo anavyotakiwa kulelewa aliiweka kwa mamaye Samson na si baba yake, Mzee Manoa. Sasa ukisoma utaona jinsi huyu mama alivyosimama kwenye nafasi yake ki ulinzi mpaka Samson alipoanza wajibu wake uliomleta duniani.

" style="max-width: 100%; display: block !important;"> Zaidi unaweza ukajifunza pia kupitia kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Siri ya kitu gani kitazaliwa, Malaika aliileta kwa Mariam, akijua ni jukumu lake kulinda hiyo siri mpaka utimilifu wake. Soma Mathayo 1:18-25.



Hata leo wanawake wanatakiwa kusimama kwenye nafasi zao za ulinzi kwa ajili ya watoto wao, vijana wao, waume zao, ndugu zao waume nk. Kwa lugha nyepesi ni shauri la Bwana kwamba kila mwanamke amlinde mwanamume anayetoka katika tumbo lake, mumuwe kama ameolewa nk ili kuhakikisha kusudi la Mungu linatimia.



Kosa la hawa wanawake/mabinti katika siku za nabii Isaya ni kujisahau, kufurahia starehe na kutokuwa waangalifu katika kufuatilia maagizo ya Mungu kuhusu ulinzi wa watoto, vijana, na waume zao nk.



Kibiblia ni utaratibu wa Mungu kumpa kila mwanamke taarifa juu ya mtoto atayemzaa, juu ya mume ambaye atamuoa lengo ikiwa ni kumsaidia ajipange ki-ulinzi.



Mwanamke hakikisha unasimama vema kwenye nafasi yako ya ulinzi kwa mwanamume. Kama utasiamama vizuri kwenye nafasi yako ya ulinzi basi uwe na uhakika umeubariki moyo wa Mungu na kwa sababu hiyo umepelekea uponyaji kwenye familia yako, jamii yako, taifa lako na uchumi wako binafsi lakini na ule wa taifa pia.



Kazi kubwa ya Shetani ni kuwafanya wanawake waliokoka duniani wajisahau, wasiwe waangalifu na hivyo wasifuatilie maagizo ambayo Bwana Mungu ameweka ndani yao kuhusu waume zao, vijana, watoto na ndugu zao wa kiume ili kusudi la Mungu lisifanikiwe. Sasa wewe usikubali shetani akuzidi maarifa, weka neno hili kwenye matendo utaona wazo la Mungu linatimia kwa kuwa MWANAMKE AMESIMAMA KWENYE NAFASI YAKE YA ULINZI.



Bwana na akubariki
 
Nilichokielewa hapo haumpendi. Sasa nenda kaombe talaka uwe huru vinginevyo utarevenge vibaya sana kwa chuki uliyo nayo kuwa huru na amani ya bwana ikuzunguke kafile talaka tu.
Huoni wana watoto? Mbna huyo mwanaume hakuomba talaka kwan ndipo akachepuke vzuri na vidampa wake?
Revenge ts a soln in this situation.
 
Hawezi kumwamini lazima ajishitukie tu, naye aumie aone machungu, halafu hapo utakuta anatetewa na wazinzi wenzie
Na wazinzi humu wamemtetea mno loh, Hawa wanaume ni jipu wa kupuuzwa tu
 
Back
Top Bottom