una hakika atalia? Mjomba angu alikuwa msumbufu sana kwenye ndoa. Mara kalala nje, mara kazaa na mtoto mdogo wa jirani, mara kaenda mkoani eti kutafuta maisha na hela yenyewe hata asitume nyumbani. Yaani ni ugomvi na uasherati. Mama wa watu kalia kachoka. Mjombangu alivyokaa mkoani karibu mwaka mkewe nae akajibanza kwa mbaba mwingine huko kijijini wakapeana na mimba. Mjomba sijui machale yalimcheza akarudi wakapeana unyumba, mara mke katumbo kakaanza kujitokeza. Hakushtukia chochote mpaka pale mke alipojifungua mtoto mkamilifu kabla ya miezi 9. Mjombangu eti akaanza ku-mind. Mamanagu mkubwa akamwambia tena unyamaze kimya umhudumie mwenzio. Mjombangu mkuki kwa nguruwe kwake ukawa mchungu. Siku ya siku kichanga kikiwa na miezi miwili mjombangu akapata mshtuko wa moyo akafa. Kwenye msiba mama zangu yaani dada wa marehemu na ndugu wengine walilia mpaka kuzimia. Chozi la mke halikudondoka ng'o. Siku 4 baada ya msiba kukaja kundi la watu 4 - wanaume wawili watu wazima, na wanawake wawili mmoja mtu mzima na mwingine msichana. Wazee wakajitambulisha wamekuja kutoa pole eti yule mjombangu alikuwa mchumba wa mtoto wao walikuwa wakiishi wote kule mkoani alikokuwa mjombangu. Wazee na binti wa watu hawakujua kama mjombangu ni mwanandoa wa miaka 12! Hapo wenyeji wanaangaliana na kufinyana. Mara akanyanyuka mke wa marehemu na kumrukia binti wa watu na kuanza kumchapa makofi eti yeye ndo alikuwa akimsababishia mateso yeye na wanae. Wageni wakatimka, yule mke akaenda kaburini akasema "yaani we mshenzi huko uliko natamani niongeze kuni uchomwe mpaka ushike adabu yako!". Hiki ni kisa cha kweli.