Wanawake wengine hawajui kusamehe

Wanawake wengine hawajui kusamehe

RIP Rob,hii imenikumbusha kaka mmoja alikuwa IT engneer pale Mwadui,sasa palitokea ugomvi na mke wake,kaka wa watu akapandwa hasira,kwenda Maganzo kautwika huko ile anarudi Mwadui maeneo ya Geti kuu kaka wa watu akapata ajali,alikufa hapo hapo,ilikuwa siku ya christmass,UGOMVI wa kwenye ndoa sio mzuri kwa kweli.
 
Haya haya ya wanadamu hakuna kosa lisilosameheka hata liwe kubwa kama mlima Kilimanjaro nasema hakuna, ni kuutune moyo wako na akili yako tu kwa lile ulilotendewa,kuna Baraka kubwa sana katika kusamehe na ni mateso makubwa sana kuwa na moyo usiosamehe,Siku zote anayeteseka ni yule asiyesamehe kuliko yule anayehitaji kusamehewa,ukishi katika kanuni ya kutangaza msamaha hata kabla hujaombwa msamaha ni nzuri sana Siku zote utakuwa mtu mwenye furaha na amani na utaishi mwenye heri siku zote za maisha yako.

Katika kesi hii Labda kiwatengu tuambie bidada hakusamehe kabisa au alisamehe akakataa kurudiana naye?

Unaelewa maana ya Mungu kusema kama mbingu ilivyo mbali na ardhi ndivyo mawazo yangu (akili/utashi) yalivyojuu ya wanadamu.
Uwezo wa Mungu katika mambo yote ikiwemo kupenda na kusamehe si sawa na tunavoweza binadamu ndo maana nimetofautisha kosa kati ya wanadamu maana kosa langu kwa mwanadamu mwingine sio necessarily likawa ni dhambi. Hivyo mwanadamu anahitaji kuomba neema ya Mungu aweze kusamehe na kusahau kosa kubwa alilotendewa. Tukiongelea kijamii ukiacha ya kiimani, huwezi kumlazimisha mtu asamehe na kumlaumu asipokupa nafasi nyingine maana hujui amejeruhiwaje.
 
Last edited by a moderator:
Apumzike kwa amani tu .. japo duh ..uyo dada atakuja kuzikaje na atalia kwa style ipi uku watu wanafaamu aliombwa msamaha akakataa ...... usimuesabia mtu makosa ata alie sema samehe saba sabini alifaamu kuna ambayo kwa akili za kibinadamu ayasameeki bt ndo tushaambiwa ivyo.
 
Wewe mkeo akiwa analala na kila anayemuona ukajua akakuomba msamaha ukamsamehe halafu ndani ya mwaka ukamfumania hali ukijua kuna ukimwi utamsamehe na kumrudia na kuwa nae kinyumba? Inawezekana ndo mazingira yaliyomkuta huyo dada, na kuna wanawake wana kinyaa vile vile hawezi kuvumilia zaidi. Utamlaumu wakati ulipewa nafasi, hata maneno ya BIBLIA yanasema watu wasiachane isipokuwa kwa sababu ya uzinzi na hili ndio janga la wanaume wa kizazi hiki.
Ushetani uko wapi hapo? Nani atawanyanyasa watoto mikononi mwanamke mama yao?

Nithibitishie kama wewe ni mkristo nikuelekeze ni wapi na kwanini kutokusamehe hakumfurahishi MUNGU.
 
nina tatizo la kutokusamehe
Mungu anisaidie
yaani hata kitu kidogo tu napata wakati mgumu kusamehe,

jikaze usiposamehe huwa kunaibua na ugomvi mwingine usio na sababu unajihisi kuumia tu muda wote.jitahidi mwaya
 
Nithibitishie kama wewe ni mkristo nikuelekeze ni wapi na kwanini kutokusamehe hakumfurahishi MUNGU.

Hakumfurahishi Mungu na yeye ambaye hajasamehe huwa hajafurahi kutokusamehe, ndo hali imemkuta. Ndio maana niliandika mwanadamu aombe neema ya Mungu ili aweze. Sijasema popote Mungu anafarahia. Ndo maana nikasema kijamii sio kiimani, hamna mwenye haki ya kumlazimisha mtu kwa jambo lililomgusa yeye binafsi.
 
Labda niweke vizuri hoja yangu,kwenye ndoa kuna mambo mengine ambayo hata kanisa linatoa baraka za katika kuachana yaani kutoa talaka japo MUNGU anachukia talaka(soma malaki 2:16a) lakini kwa ajili ya uasherati talaka imeruhusiwa kibiblia(soma Mathayo 5:32 na 19:9).Sijajua tatizo la hawa ndugu ila kwa mkutadha huu Dada hasa Kama yeye alishasamehe Mara ya kwanza kisha jamaa akarudia tena yale yale,anaweza kugomea kusamehe.Kupigiwa inauma sema labda haijakukuta.

Okey vizuri ngoja tustik hapahapa na swala la ndoa kwanza,ni kweli kwa habari ya uasherati talaka yaweza kutolewa,lakini bado kusamehe ni swala lingne,inaweza kuwa ni mara moja ukaamua iwe ni talaka,inaweza kuwa mara mbili,tatu hata 20 ukaamua kusamehe,yote yapo mikononi mwa mtu.

Inapofikia swala la kutengana(talaka) unaweza kutengana na mtu lakini katika hali ya kusameheana na kuachana kwa amani kabisa kwamba hapa tulipofika hatuwezi enda njia moja tena ila katika amani,na kuna sababu za msingi kabisa juu ya hilo na mtenda kosa anaridhia kabisa kiasi kwamba anajiona anastahili kuyavuna hayo. Kusamehe hakukwepeki kabisa ingawaje kuna mahali mtu anabidi alipie gharama ya yale alotenda.
Nipo kwenye ndoa siyo kwamba sielewi neno kuchapiwa linavyouma,katika ndoa tunapitia mengi ambayo hata wakati mwingne unajiuliza hivi hata katika hili nimepitaje?yote juu ya yote ni upendo,uvumilivu na kuchukuliana bila kusahau kumshirikisha Mungu katika yote.
 
Unaelewa maana ya Mungu kusema kama mbingu ilivyo mbali na ardhi ndivyo mawazo yangu (akili/utashi) yalivyojuu ya wanadamu.
Uwezo wa Mungu katika mambo yote ikiwemo kupenda na kusamehe si sawa na tunavoweza binadamu ndo maana nimetofautisha kosa kati ya wanadamu maana kosa langu kwa mwanadamu mwingine sio necessarily likawa ni dhambi. Hivyo mwanadamu anahitaji kuomba neema ya Mungu aweze kusamehe na kusahau kosa kubwa alilotendewa. Tukiongelea kijamii ukiacha ya kiimani, huwezi kumlazimisha mtu asamehe na kumlaumu asipokupa nafasi nyingine maana hujui amejeruhiwaje.
Hizo ni tabia za Mungu na sisi kama wanadamu aliotuumba yatupasa kuwa nazo,KUTOKUSAMEHE NI DHAMBI haijalishi ni kosa kubwa au dogo umetendwa,katika dhambi karibu zote hakuna dhambi tunazomtenda Mungu moja kwa moja bali ni sisi kwa sisi wanadamu tunatendana na hatimaye inakuwa ni dhambi kwa Mungu na kwa huyo mwanadamu mwenziyo.

Mtu halazimishwi kusamehe au hawezi kulaumiwa kutomsamehe mwenzie ila jua kutosamehe ni dhambi, kijamii tunasemehe kwa afya roho na mwili na faida ni nyingi za kusamehe kuliko madhara ya kutokusamehe.
 
r.i.p rob
ila marehemu alifanya kosa gani mi najua wanawake huwa wanavumilia kubaki ili kulea watoto hata kama mapenzi yashaisha huyo hadi akaacha watoto mmh!!!
 
Hizo ni tabia za Mungu na sisi kama wanadamu aliotuumba yatupasa kuwa nazo,KUTOKUSAMEHE NI DHAMBI haijalishi ni kosa kubwa au dogo umetendwa,katika dhambi karibu zote hakuna dhambi tunazomtenda Mungu moja kwa moja bali ni sisi kwa sisi wanadamu tunatendana na hatimaye inakuwa ni dhambi kwa Mungu na kwa huyo mwanadamu mwenziyo.

Mtu halazimishwi kusamehe au hawezi kulaumiwa kutomsamehe mwenzie ila jua kutosamehe ni dhambi, kijamii tunasemehe kwa afya roho na mwili na faida ni nyingi za kusamehe kuliko madhara ya kutokusamehe.

Kunawatu wamezaliwa na high conflict personality.Bila drama hamna mapenzi
 
Nithibitishie kama wewe ni mkristo nikuelekeze ni wapi na kwanini kutokusamehe hakumfurahishi MUNGU.

Aliyekuwmbia kuna Mungu ni nani?unajuaje Mungu ni uzushi tu .
 
Hakumfurahishi Mungu na yeye ambaye hajasamehe huwa hajafurahi kutokusamehe, ndo hali imemkuta. Ndio maana niliandika mwanadamu aombe neema ya Mungu ili aweze. Sijasema popote Mungu anafarahia. Ndo maana nikasema kijamii sio kiimani, hamna mwenye haki ya kumlazimisha mtu kwa jambo lililomgusa yeye binafsi.

No god .mungu ni uzushi
 
Hizo ni tabia za Mungu na sisi kama wanadamu aliotuumba yatupasa kuwa nazo,KUTOKUSAMEHE NI DHAMBI haijalishi ni kosa kubwa au dogo umetendwa,katika dhambi karibu zote hakuna dhambi tunazomtenda Mungu moja kwa moja bali ni sisi kwa sisi wanadamu tunatendana na hatimaye inakuwa ni dhambi kwa Mungu na kwa huyo mwanadamu mwenziyo.

Mtu halazimishwi kusamehe au hawezi kulaumiwa kutomsamehe mwenzie ila jua kutosamehe ni dhambi, kijamii tunasemehe kwa afya roho na mwili na faida ni nyingi za kusamehe kuliko madhara ya kutokusamehe.

Hiyo ni level yako, usipanic sio lazima kila mtu awe level moja na wewe. Bado tuko duniani
 
Okey vizuri ngoja tustik hapahapa na swala la ndoa kwanza,ni kweli kwa habari ya uasherati talaka yaweza kutolewa,lakini bado kusamehe ni swala lingne,inaweza kuwa ni mara moja ukaamua iwe ni talaka,inaweza kuwa mara mbili,tatu hata 20 ukaamua kusamehe,yote yapo mikononi mwa mtu.

Inapofikia swala la kutengana(talaka) unaweza kutengana na mtu lakini katika hali ya kusameheana na kuachana kwa amani kabisa kwamba hapa tulipofika hatuwezi enda njia moja tena ila katika amani,na kuna sababu za msingi kabisa juu ya hilo na mtenda kosa anaridhia kabisa kiasi kwamba anajiona anastahili kuyavuna hayo. Kusamehe hakukwepeki kabisa ingawaje kuna mahali mtu anabidi alipie gharama ya yale alotenda.
Nipo kwenye ndoa siyo kwamba sielewi neno kuchapiwa linavyouma,katika ndoa tunapitia mengi ambayo hata wakati mwingne unajiuliza hivi hata katika hili nimepitaje?yote juu ya yote ni upendo,uvumilivu na kuchukuliana bila kusahau kumshirikisha Mungu katika yote.

Nakubaliana na we japo siko kwenye ndoa lakini nimekuwa na amani Sana pale tunapoachana na mtu kwa amani na kusameheana.Nafarijiwa sana na Maneno ya wakolosai 3:12-13,pia waweza soma 1petro 3:1-13 lakini kwa hii mada mstari wa 8 na 9 umeleeza vyema.Nakutakia wkend yenye amani ya MUNGU.
 
Hiyo ni level yako, usipanic sio lazima kila mtu awe level moja na wewe. Bado tuko duniani

Sijapanic na sitapanic maadam bado tupo duniani lazima tueleweshane na kusaidiana njia iliyo bora, na wala sijasema kila mtu awe kama mimi, ila ni ukweli usiopingika hakuna faida ya kutosamehe zaidi ya maumivu, uchungu,hasira,chuki na visasi visivyoisha na zaidi ni kujibebesha mizigo katika maisha isiyo na lazima.
 
Hakuna anayebisha
 
Back
Top Bottom