ShalomP
Member
- Jun 14, 2019
- 97
- 154
Ndio maana mnapofunga ndoa mnaulizwa swali mpo tayari kuvumilaana kwenye shida na raha? Kama unaona mwanaume unaonewa na mke wako sheria zipo wazi mpeleke hata kwa viongozi wa dini yako wapate kuwashauri au hata kwa mjumbe au balozi au kwa wazazi wake au kwa mzee mwenye hekima aloyewazidi umri ili awashauri.Sasa mwanaume unapoamua kirudi usiku ukiwa umelewa eti unamkomoa kwa kumuoneshea jeuri hapo utakuwa utatui tatizo ndio utazidisha tatizo.Tatizo halikimbiwi angalia njia Bora ya kutatua.Tatizo Kuna baadhi ya wanaume mnapigwa mpaka na wake zenu lakini mnaona aibu kusema mnajikaza kisabuni na Tai shingoni eti kamanda sheria zipo wazi kuwalinda wote.Changamoto katika ndoa ni kawaida ndio maana Kwenye ndoa unapewa cheti mapema mtihani unafuata.Maandiko yanasema Wanaume ishini na wake zenu kwa akili haya maneno yana maana kubwa Tena sanaaa.