Wanawake wengi wakiingia kwenye ndoa wanabadilika kitabia

baptist

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
426
255
Habari za muda huu wadau,

Nimekuja na kichwa hichi Cha habari, kutokana na juzi Kati tulikuwa na washkaji Kama wanne hivi wote tupo kwenye ndoa, kasoro mmoja wetu, single boi.

Tukajikuta katika mada ya kushare changamoto za ndoa zetu kila mtu kwa muda wake,

Katika kushare experience hizo nikagundua mambo yafuatayo;

Wanawake wengi wakishaingia kwenye ndoa wanabadilika Sana hasa kitabia, mwanzo anaweza kuwa alikuwa mpole, mcheshi, utulivu wa kutosha, heshima debe. Akishaingia tu anataka akupande kichwa ukorofi unaanza, maneno yanaanza, kesi zisizo na msingi, madharau, kutokujishusha na kadhalika..🤒🤒

Hii nimekuja kugundua inawagusa Sana wanaume wengi tuliooa kutoka na changamoto hizo, wengi wao wamefikia hatua ya kuwa na kamchepuko at least apunguze mawazo kidogo angalau, wengine kujikuta akitoka zake job anaingia bar kuzuga mpaka mida fulan akirudi akute wife ameshalala.

Wanawake wengi kwenye ndoa Wana tabia ya kutokujiamini, muda wote utakuta anakuhisi tu kwamba una mchepuko hata Kama huna, atang'ang'ana na simu yako ili kutafuta kisichopo ili mradi tu umnyime aongee au ampe akute hata salamu ya kike tu mparangane.

Mwanamke ndoani siku hizi kujishusha hakupo ukipanda naye anapanda, Tena zaidi anakwambia ukinigusa narudi kwetu na anaweza ondoka vile vile kwa jeuri na asirudi. (Hilo mshikaji wangu mmoja lilimkuta, Ila baadaye mwanamke akirudi mwenyewe)..

Ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kwasababu Kama hizi, mafahali wawili kuishia zizi moja haijawahi tokea,.

Mwanamke aliletwa duniani kuja kumsaidia mume wake majukumu, kumuheshimu, kumtii n.k (hata vitabu vya dini vinasisitiza hilo)

Hii jeuri wanawake majumbani wanaitoa wapi siku hizi, sometimes unakuta jamaa mpole kweli lakini bado atakukoroga kichwa akae hapo juu..

Wanaume tunaogopa kuwahi majumbani kupumzika inabidi kunazuga bar, kwa washkaji, vibanda umiza, pengine kuchepuka kabisa( maana hata ratiba ya tendo la ndoa unapangiwa) ili mradi muda uende ukifika tu kula kulala..

Njoo tushare experience hapa na kubadilisha mawazo 😎😎

No offence🚶🚶
 
Title ya uzi ingependeza kama ungeandika 'Tujadili changamoto za kwenye Ndoa'.

Ila kuhusu hoja zako, ni kweli ipo hivyo na hiyo haipo kwa wanawake tu ubabe na kutojishusha upo pande zote za wanandoa na kupelekea upendo kupungua.

Ndio maana wahenga wanasema Ndoa ni chuo cha uvumilivu.
 
Nini kifanyike?

Hivi ni kweli ksbisa mtu tokea mlipojuana, urafiki, uchumba hadi kufikia ndoa.. bado hujamjua tabia yake kweli?? Mbona mimi hatua ya urafiki tu najua ulivyo mwanzo mwisho?
 
Home sweet home
IMG_20200206_070120.jpg
 
Jamani jamani jamani mtusameheee jamani tusameheni na sisi ni binadamu..nyie mna madhaifu yenu nasi pia vivyo hivyo. Nadhani kuzaa kunyonyesha na majukumu ya familia na ulezi watt ni kitu kimoja kigumu sana. Nadhani kupitia hizi hatua kuna some hormones zinaisha au kuongezeka kupelekea tabia zetu zibadilike. Lakini wanawake wenzangu hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kuomba msamaha mimi kuomba msamaha nipo vzr kwa sbb naweza kulipukaaa kama mtungi wa gas ila nikikaa na kutafakari naona kabisa namakosa nitaomba radhi aisee. Yani mm kugombana na Mr au kumletea kiburi na akakasirika huwa inanipa tabu sana yani nijiskia vibaya kama niko uchi so mara nyingi hukumbuka kuomba msamaha yaishe.
 
Ukweli ni kuwa wanawake kama wewe wachache sana na hata wanaume wanao tambua thamani ya msamaha ni wachache wengi wanaishi kwa kukomoana
 
Hamkuzungumza tabia ya vijana Kuonyesha wana uwezo wa kupata pesa ya kuendesha familia ila akishaoa anaanza kuruka ruka viunzi na kupenda kitonga.
Kweli kabisa nadhani hii ni miongoni mwa sababu wanawake wanawaona wanaume tatizo.

Na wao wamezidi tamaa za vitu inabidi washikaji watumie mbinu za kitapeli kuwanasa....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za muda huu wadau,

Nimekuja na kichwa hichi Cha habari, kutokana na juzi Kati tulikuwa na washkaji Kama wanne hivi wote tupo kwenye ndoa, kasoro mmoja wetu, single boi.

Tukajikuta katika mada ya kushare changamoto za ndoa zetu kila mtu kwa muda wake,

Katika kushare experience hizo nikagundua mambo yafuatayo;

Wanawake wengi wakishaingia kwenye ndoa wanabadilika Sana hasa kitabia, mwanzo anaweza kuwa alikuwa mpole, mcheshi, utulivu wa kutosha, heshima debe. Akishaingia tu anataka akupande kichwa ukorofi unaanza, maneno yanaanza, kesi zisizo na msingi, madharau, kutokujishusha na kadhalika..🤒🤒

Hii nimekuja kugundua inawagusa Sana wanaume wengi tuliooa kutoka na changamoto hizo, wengi wao wamefikia hatua ya kuwa na kamchepuko at least apunguze mawazo kidogo angalau, wengine kujikuta akitoka zake job anaingia bar kuzuga mpaka mida fulan akirudi akute wife ameshalala.

Wanawake wengi kwenye ndoa Wana tabia ya kutokujiamini, muda wote utakuta anakuhisi tu kwamba una mchepuko hata Kama huna, atang'ang'ana na simu yako ili kutafuta kisichopo ili mradi tu umnyime aongee au ampe akute hata salamu ya kike tu mparangane.

Mwanamke ndoani siku hizi kujishusha hakupo ukipanda naye anapanda, Tena zaidi anakwambia ukinigusa narudi kwetu na anaweza ondoka vile vile kwa jeuri na asirudi. (Hilo mshikaji wangu mmoja lilimkuta, Ila baadaye mwanamke akirudi mwenyewe)..

Ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kwasababu Kama hizi, mafahali wawili kuishia zizi moja haijawahi tokea,.

Mwanamke aliletwa duniani kuja kumsaidia mume wake majukumu, kumuheshimu, kumtii n.k (hata vitabu vya dini vinasisitiza hilo)

Hii jeuri wanawake majumbani wanaitoa wapi siku hizi, sometimes unakuta jamaa mpole kweli lakini bado atakukoroga kichwa akae hapo juu..

Wanaume tunaogopa kuwahi majumbani kupumzika inabidi kunazuga bar, kwa washkaji, vibanda umiza, pengine kuchepuka kabisa( maana hata ratiba ya tendo la ndoa unapangiwa) ili mradi muda uende ukifika tu kula kulala..

Njoo tushare experience hapa na kubadilisha mawazo 😎😎

No offence🚶🚶
Mlishashauriwa msioe wanawake walioajiriwa, mkadai ooh kusaidiana pumbavu sana mkone mwanamke alieajiriwa atakupanda kichwani tu hawana adabu niwakorofi VIBURI NA JEURI wanajazana maujinga uko makazini usawa bla bla 50/50 anaweka kupanga ratiba ya kuosha vyombo leo yeye kesho wewe na ukigoma matusi kama yote ukimkaripia anakwambia kesho anakwenda dawati ya jinsia na kweli ataenda.
 
Kwa sasa nasoma madesa na maandalio ya seminar, oa anaekupenda wewe na nafsi yako na si cheo, elimu, fani, aina ya kazi na kipato chako mama fursaz. Asiwe mchanyato wa mashine. Akupe vyombo bila hiana na awe mchokozi yeye kwenye shoo. Mbuu salale
 
Ngoja azae watoto wawili,ndoa utaiona ndoano,ataanza kukuchonganisha na hao watoto.
 
Back
Top Bottom