Wanawake wengi wa siku hizi hawajui kupika

Wanawake wengi wa siku hizi hawajui kupika

Uvivu jamani ukiwa mvivu utakuwa mchafu, ukiwa mchafu hata vyakula vyako vitakuwa vya ovyo havina ladha uvivu, halafu ndo hao hao utawasikia oo mimi situmii facebook wakati kule kuna magroup mazuri sana yanafundisha mapishi, kila kitu ni kujifunza na kujaribu hakuna aliyezaliwa anajua..
Ngoja nikuitie wapishi wenza nguli wa humu snowhite farkhina Miss Natafuta Mzigua90 Madame B.
Dah!!!
amu mada nimeikutia mbali si unajua majukumu shost!!
Ila kiukweli wanawake wasiojua kupika huwa nawashangaa sana.
Kwanza mwanamke unaanzaje kutojua kupika?
Mie bado hainiingii akilini eti mtu mpaka anaingia ndoani, anachoweza kuchemsha ni chai na kupika tambi tu.

Hv unakumbukana sotojo tulilokuwa tunalipikaga enzi zile?
Sie wanawake bhana....unakula huku unajilamba.
Ukuje siku nikupikie mchuzi wa papa wa nazi wenye nyanya chungu na bamia teketeke
 
Uzi una ukweli kabisa, mimi binafsi siku hizi nakula yu ilimradi na wakati mwigine hata plate siimalizi chakula hakija ladha kabisa , sijui ni viungo vya kisasa wanavyo tumia wapishi au vipi
 
M nimejigundua juzi juzi kuwa sijui kupika nilikuwa nyumbani kila ninachopika kasoro kibao.(ugali ndio aibuu)
Hiii ni aibu kubwa sanaaa siku izi najifunza na naona mabadiliko.
 
Back
Top Bottom