Wanawake wengi wa siku hizi hawajui kupika

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Tofauti na miaka ya zamani wakati tunakua,wazazi wetu walikuwa wakipika chakula watoto mnafurahia chakula kutokana na mapishi mazuri.

Kwa mfano, wa mama na wa dada wa zamani(waliozaliwa miaka ya 60 kurudi nyuma) wengi wao walikuwa wapishi wazuri kwenye familia zao kiasi kwamba wakipika chakula mfano pilau, wali, samaki,chapati,maandazi,n.k, wanafamilia chakula mnakifurahia tofauti na siku hizi.

Hivi sasa unaweza kuta mwanamke mrembo ila akipika chakula,unaweza kula tu kwa kumuonea aibu na hali hii ni hata kwa ma-house girl wa siku hizi ambae ukimleta kwako inabidi umpe darasa la kupika chakula chenye ladha.

Kwenye migahawa na wa mama ntilie na kwenye nako hali ni hio hio.Mtu unaagiza chakula kula unashindwa na bado ukibadili mgahawa hakuna guarantee kwamba unakohamia kuna unafuu (afadhali).

Inawezeka mfumo wa maisha ya kisasa ndio unachangia hali hii kwa kiasi kikubwa na hasa kwa waloizaliwa kuanzia ya miaka ya 80 mwishoni na kuendelea.
 
Mwanamke asiyejua kupika maana yake hajui chakula kitamu na siyo mroho, ukiwa mroho kama mie lazima ujue kupika, kuna kipindi nlikuwa nipo mikoani naagizisha viungo vya vya nyama, kuku, samaki, mchuzi wa aina zote, supu, biriani, ndizi mpaka cowboy chapati dar, mchele wa basmati n.k.
NB:ukitaka kujua asiyejua ingia jikoni kwake au fungua friji lake ukikuta maji na savanna tu toka baru.
 
wengi wao wakipika ugali utafikiri makande, yaani hawajui kabisa kupika hasa wasomi na kujifunza hawataki.

Ila sababu kuu ni malezi, unakuta mtu tangu anaanza shule ya awali mpaka anamaliza form six anasoma boarding schools, na hata akifika chuo chakula chake ni cha kwenye migahawa. Mtu kama huyu ni vigumu sana kuwa fundi wa mapishi
 
Mwanamke asiyejua kupika maana yake hajui chakula kitamu na siyo mroho, ukiwa mroho kama mie lazima ujue kupika, kuna kipindi nlikuwa nipo mikoani naagizisha viungo vya vya nyama, kuku, samaki, mchuzi wa aina zote, supu, biriani, ndizi mpaka cowboy chapati dar, mchele wa basmati n.k.
NB:ukitaka kujua asiyejua ingia jikoni kwake au fungua friji lake ukikuta maji na savanna tu toka baru.
Wifi ako wa zaman nilimleteaga nyama ya kitimoto Mbichi aipikee.

Dah, nilikuta limchuzi kajaza mafutaa mpk nikasema hapa nakufa.

Ilibidi nisingizie tumbo linanisumbua nisile tu.

Mbaya zaidi ukitaka umfundishe kupika hataki, anaona unamdharau sijui.

Nikapiga chini
 
Tofauti na miaka ya zamani wakati tunakua,wazazi wetu walikuwa wakipika chakula watoto mnafurahia chakula kutokana na mapishi mazuri.

Kwa mfano, wa mama na wa dada wa zamani(waliozaliwa miaka ya 60 kurudi nyuma) wengi wao walikuwa wapishi wazuri kwenye familia zao kiasi kwamba wakipika chakula mfano pilau, wali, samaki,chapati,maandazi,n.k, wanafamilia chakula mnakifurahia tofauti na siku hizi.

Hivi sasa unaweza kuta mwanamke mrembo ila akipika chakula,unaweza kula tu kwa kumuonea aibu na hali hii ni hata kwa ma-house girl wa siku hizi ambae ukimleta kwako inabidi umpe darasa la kupika chakula chenye ladha.

Kwenye migahawa na wa mama ntilie na kwenye nako hali ni hio hio.Mtu unaagiza chakula kula unashindwa na bado ukibadili mgahawa hakuna guarantee kwamba unakohamia kuna unafuu (afadhali).

Inawezeka mfumo wa maisha ya kisasa ndio unachangia hali hii kwa kiasi kikubwa na hasa kwa waloizaliwa kuanzia ya miaka ya 80 mwishoni na kuendelea.
yaaan nitakae muoa atapata tabuu sana maana napenda misosi mizuriii....ko akipikaa hovyoo tatzo...nitaingia mwenyewe jikoniii....siku mama ametutembeleaa naingia mwenyewe jikoni ...ili mama ake aone impact ya malezi yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sometimes mnasaidia sio kulalamika tu
Ahsante hubby alinifundisha kupika chapati nzuri hadi Leo nisipopika mie hali, alinifundisha na kupika ugali mzuri usio na mabonge ya unga unga hadi sasa sijamuangusha
 
Uvivu jamani ukiwa mvivu utakuwa mchafu, ukiwa mchafu hata vyakula vyako vitakuwa vya ovyo havina ladha uvivu, halafu ndo hao hao utawasikia oo mimi situmii facebook wakati kule kuna magroup mazuri sana yanafundisha mapishi, kila kitu ni kujifunza na kujaribu hakuna aliyezaliwa anajua..
Ngoja nikuitie wapishi wenza nguli wa humu snowhite farkhina Miss Natafuta Mzigua90 Madame B.
Hadi Miss Natafuta anajua kupika?
 
  • Thanks
Reactions: sab
nobodylikedme sikuhizi tunajifunza mtandaoni, kwenye tv, mimi pia nimesoma boarding miaka yote ila kwa kuwa naelewa umuhimu wa chakula cha nyumbani ninajitahidi kwa kweli nijue, ni aibu kwa mdada au mmama kupika ovyo ovyo kwa kusingizia ulikuwa boarding.
Huwa naona furaha kweli kweli familia yangu kufurahia chakula nlichopika kwa mikono yangu.
 
Back
Top Bottom