Wanawake wengi hawawataki wanaume maskini

Sasa hv kila mtu apambane ki mpango wake ukitegemea mwanaume umekwisha maana na wanaume sasa hv na sisi hatutaki demu masikini dadeki
 
Ata mimi ninapokutana naye najua hana mia mbovu na si-expect kuona gari au nyumba kwake! Sio kila mwanamke anategemea kuona hivyo vitu kama maendeleo kwa haraka haraka! Kuna watu tunaaanza nao moja ndio tumemaliza chuo mnasindikizana mpaka interview zote, mambo yanagoma mnaanza biashara ndogondogo! Unauza mpka mama ntilie ili tu mfikie lengo!

Ungejitahidi kuweka ujinsia na chuki kwa mwanamke kando, tungeelewana sana! Ila shida unashikilia sana mambo ya gender.. hapo hata nikuelezee siku tatu utakazania mwanaume ndio anaonewa
 
Point hapo sio kumsubiri mwanaume point ni kuachwa baada ya mafanikio, mtu kufanikiwa akakuacha sio kwamba wewe ndio hunaga maisha mengine unasubiri atoboe aje maishani mwako unaweza kuwa na kazi pia ila point ni mtu kwanini akijipata asepe?
 
Hmm u went too far! Kwani hujawahi kuona binti yako ana kakijana hakaeleweki na huoni wakifika popote? Hata mtaani tu hujakutana na binti anayekaribia kuharibiwa maisha ukasikia ukakasi na hata hakuhusu?

Achana na wale waliojitambua wakaanza maisha wameamua kuingia ndoani, kuna mwanga unaouona kama mzazi
 
Vijana wajinga wa JF hawataki single mother, lakini wanataka watoto wakali wakati hali zao ni makapuku jazz band
Hata wakiwapata hao wasio singo maza wanashindwana nao wanazidi kuliongeza kundi tu, watoto mpaka wa 2005 saiz ni masingo maza!
 
Point hapo sio kumsubiri mwanaume point ni kuachwa baada ya mafanikio, mtu kufanikiwa akakuacha sio kwamba wewe ndio hunaga maisha mengine unasubiri atoboe aje maishani mwako unaweza kuwa na kazi pia ila point ni mtu kwanini akijipata asepe?
Hivi hakuna wanawake waliojipata wakawaacha wanaume wao pia?
 
Uko sahihi alafu wanaume watulivu wakiwa hawana ela wapate ela sasa ndo utaona rangizao
Hili labda liwe pamoja na sababu zingine, ila mwanaume mliyekutana mkiwa masikini mkapata pamoja, ni ngumu sana kukuacha.

Lakini kama mwanamke ana tabia za hovyo, hawezi kuwa sababu ya kutokuachwa hata kama mmetafuta wote
 
Yani nikomae nae mpaka tunadharaulika na kila mtu, halafu aokoteze viela vya kubadili mboga ndio aanze kula pembeni! Uweeeh! Siwezi..
Huwezi kushindana na nature ya mwanaume kubadili mboga. Kipato kikiongezeka na matumizi huongezeka.

Hakuna mwanamke aliyewahi kushinda hiyo ligi. Usiseme fulani mbona hana, sema hajadakwa tu.
 
Point hapo sio kumsubiri mwanaume point ni kuachwa baada ya mafanikio, mtu kufanikiwa akakuacha sio kwamba wewe ndio hunaga maisha mengine unasubiri atoboe aje maishani mwako unaweza kuwa na kazi pia ila point ni mtu kwanini akijipata asepe?
Kwanini wewe unafikiri mwanaume akijipata hana haki ya kukuacha? Una tangiable value yoyote uliongeza kwenye hustles zake mpaka ujione upo entitled kwenye mafanikio yake?
 
Sisemi kwamba mwanaume anaonewa, offcourse yoyote ambae ana nguvu ya kufanya maamuzi lazima atakua ruthless. Power don't meant to be polite.

Ninachotaka kukiongea hapa ni unrealistic expectations mlizonazo wanawake. Ukipita huku utasikia mahari yangu milioni 500,ukipita kule utasikia mwanaume mwenye kipato chini ya milioni mbili asioe. Unabaki kujiuliza hawa wanawake wanaongea haya kwa kufanya rejea ya uchumi huu huu wa bongo au wanafanya rejea ya uchumi wa monaco ambapo wanaishi matajiri tu.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…