kwetumasoko
JF-Expert Member
- Aug 24, 2016
- 866
- 510
Wana jamii
Kuna mwanamke mmoja nimezoeana nae sana kwa issue za kiofisi, lakini huwa tunapiga story mbalimbali kama dada yangu ambaye namuhushimu sana na pia kama mteja na yeye mara nyingi huwa anakuja ofisini kwangu kwa ajili ya huduma mbalimbali. Kwa kweli tumezoeana sana
Wakati mwingine anakuja, ananiambia nina shida sina pesa ya ada kwa ajili ya mtoto, huwa nampa. Mara ooo sina pesa ya matumizi nampa. Mara nikopeshe pesa kwa ajili ya kupeleka VICOBA, huwa nampa na wala harudishi.
Sasa juzi kaniomba nimkopeshe pesa, na anadai kuwa atanipa baada ya mwezi mmoja, mi nikamwambi kwa sasa pesa sina, ningekuwa nayo ningekupa. Nimefanya hivo kwa sababu najua nikimpa tu ndo imekwenda hiyo, hairudi tena.
Tulipoonana, naona mtu kanuna wala hataki kunisalimu kabisa. Nkajiuliza ina maana tatizo ni pesa? Hapo sina mahusiano naye kabisa ya kimapenzi, ingekuwa hivo si anaweza kunitoa roho!
Hivi wanawake hiyo ni tabia yenu mpaka mnajisahahu kana kwamba imefikia mahala rafiki tu kiume unamfanya kama mpenzi wako jamani au mmeo?