Wanawake wafanyakazi ndivyo walivyo katika ndoa?

Wanawake wafanyakazi ndivyo walivyo katika ndoa?

kumekuwa na tabia hii ya ajabu lakini ipo nguvu nyuma yake inayochochea haya wadadawa kikristo wamekuwa wakiolewa sana na wakaka wasio wakristo mwisho wa siku wengi wao si mzuri hii tabia inakua kwa kasi sana si tabia nzuri ni heri kuvumilia kuliko kuchanganya imani watoto huangaishwa sana na pia haipendez.

Maskini we ni mgeni kwenye mambo ya maisha! kwa taarifa hilo halina cha ukristo wala uislam ni msimamo wa mwanaume kwenye familia!
 
habari wa JF.
miezi sita iliyopita nilibahatika kuoa mwanamke mmoja wa kiislam ambapo tulifunga ndoa ya kiislam.
katika mahusiano ya uchumba nilimuona ni muwazi na anaakili za kimaendeleo ndipo nikatangaza ndoa.
lakini tangu nifunge naye ndoa sijawahi kuona hata shilingi tano yake.pia hajawahi kutoa katika benki hata shilingi yeye ana deposit tu.nikijaribu kumuuliza yeye atatumia fedha zake kwa matumizi gani?anasema jukumu la kumlisha, ni langu.sawa sikatai je fedha yeye ataweka wapi ?au atajenga lotion bila mimi kujua!!! naombeni mchango wenu.nini nifanye?au nimuache?

Pole sana, huyo dada hana hatia kwani hayo ndio mafundisho ya imani yake. Mume anabeba majukumu yote ya kumuhudumia mkewe.
 
Yawezekana wanawake waliowengi akilizao nikama zahuyu mmama.Kweli jukumu lakutunza familia nilamwanaume ila kama mnafanya kazi wote majukumu mnagawana
mfano mwanaume mambo muhimu kama kulipa bill zote kusomesha chili nijukumu lako mahitaji ya ndani yawe ya mama kama kununua mboga nyanya vyakula kwa ujumla ingawa nawewe baba waweza saidia kiasi.
Kama hataki Fanya njia moja nunua unga 50 kg maharage 20kg Nguo mnunulie Mara m bili kwa mwaka mahitaji muhimu sana mtimizie baada ya hapo fedha yako Fanya maendeleo tena hatakiwi kuhusika kwakuwa haimuhusi kinachomuhusu yeye nikutunza tuu

Mkuu hivi unajua maana ya baba wa familia???
Hata bible inasema Mwanamme atakula kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu.....Hebu msikimbie majukumu yenu....
Mtunze mkeo....yaan mwanamke anavohakikisha ww unakula Unalala.....watt wanaenda shule ....afanye kila kitu....n zaid ya uto tuhela twako twa matumizi Sema hua wanavumilia na ndo maana mama atabaki kua mama tuuu no one like her!!
 
Ulikosea tangu mwanzo sasa ndo unajuta.hawa inatakiwa uwabane mapema ukichelewa ndo haya yanayokukuta sasa.na ww goma kutoa zako.

Yaan wazazi wangu wamenilea kwa shida....nmesoma kwa shida......nmetafuta kaz kwa shida atiiii mtu aje anioe na kunipangia matumiz ya mshahara wangu kisa et kanioa na katoa tu mahar twake twa tulaki nane???????? Haaa Haaaa mtasubir sana
 
Mkuu hivi unajua maana ya baba wa familia???
Hata bible inasema Mwanamme atakula kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu.....Hebu msikimbie majukumu yenu....
Mtunze mkeo....yaan mwanamke anavohakikisha ww unakula Unalala.....watt wanaenda shule ....afanye kila kitu....n zaid ya uto tuhela twako twa matumizi Sema hua wanavumilia na ndo maana mama atabaki kua mama tuuu no one like her!!

Kweli mkuu mi huwa namkumbuka mama alivyokuwa akinihangaikia! sema wanawake wengine wavivu sana hayo majukum yao wengine wanayakwepa na kuwaachia mahouse girl!
 
Why? Sasa angetaka kujua siangeshaniuliza kama jamaa yetu hapa

Saa nyingine tunafanya ya kuwaridhisha ili amani iwepo sababu tunajua kila mwanamke hupenda kuona mumewe akiwa financially stable na njia moja wapo ni kuhakikisha hatuulizi pesa zenu unless it is extremely necessary!!!!

Ndio maana nikasema hiyo happiness yeye naye angesema ingekuwa safi sana kuliko wewe kusema "we are happy"!!!!!

Kuna dada kawahi kulia baada ya kukuta mumewe anadaiwa mtaani kwa kashfa pesa ambazo yeye kaziweka tu kwa akaunti hana kazi nazo kwa muda huo akajutia kuwa kama mumewe alikuwa kakwama si angemuomba yeye...watu wakamuuliza kipato cha mumeo na maisha yenu vinalingana????!!!!

Kilio kikaongezeka mara dufu; ndoa zina mengi sana hakikisha mwenza wako anakuambia yeye kuwa ana furaha sio wewe kudhani ana furaha sababu tu halalamiki we are differently wired!!!!
 
Shukrani dada wa mimi!!!!!
Mi nadhani kuna baadhi ya wanaume wanachukulia wanawake for granted na hapa ndio kuna tatizo, mtu asomeshwe na wazazi wake na kukesha elimu ilivyo ngumu eti ukimuoa tu kila kitu kiwe chini yako???!!!

Yaani kama msukule tu ye awe fuata upepo!!!!????

Tulipoambiwa wanaume tuwe viongozi ni pamoja na "financial discipline" kuanzia utafutaji mpaka matumizi!!!!!!

Mtu ana account zaid ya moja lakini mkewe hana hata kujua moja wala mbili kuhusu zote yaani ukiumwa ndio muanze kuambiana password uko kwenye machela njiani kwenda chumba cha upasuaji aibu gani hiii????!!!!

Kama serikali tu inaingia PPP we mkeo ndani hajui hata salary slip yako ikoje????!!!
Halafu unataka kukodoa macho juu ya kipato chake, ubinafsi sana huu!!!!!

Mke ni rafiki, partner, mpenzi wako wa kufa na kuzikana kaeni pigeni story mbona waelewa sana tu wanawake kama na wewe mwenyewe unasomeka!!!!!

Umetishaaaaa .......... hivi hakuna nafasi huko hata ya mke wa sita kaka Olesaidimu???? Mwanaume wa hivi ni diamond trust me!
 
Umetishaaaaa .......... hivi hakuna nafasi huko hata ya mke wa sita kaka Olesaidimu???? Mwanaume wa hivi ni diamond trust me!

Duunh mie huyu????!!!
Nna maboko yangu labda ukiyasikia hutotaka hata kuniona sura!!!
 
moja ya vigezo vya mke nilivyo vizingatia ni kazi na kipatochangu ni chetu na chakwake ni chetu. nashuru alifuzu jaribio hilo, hadi sasa mwaka 10 swala la mapato na matumizi sio siri kwetu. nawashauri msilewe na mapenzi ya awali, unavomwanaza ndivo anavoamini maisha yenu. poleni wahanga.

Mkuu tuko pamoja hapa. Hayo mawazo eti mwanamke anaolewa ili atunzwe na mwanaume yamepitwa na wakati kwani kuna wanandoa ambao mwanamke ndie anakipato kikubwa kuliko bwana, sasa hapa tusemeje? Kwa kifupi suala la kipato cha mwanamke imekuwa kikwazo kwa ndoa nyingi. Ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu kuna wanawake wenye mawazo kwamba kipato chake hakimhusu mume. Haya ni makosa. Kabla ya kufunga ndoa ni vizuri kuzungumzia mgawanyo na matumizi ya kipato chenu kwa ujumla. Bila hivyo, ni matatizo huko mbeleni.

Kwangu mimi, hakuna kificho cha kipato unaweza kunikuta na ATM za mwenza wangu au yeye na za kwangu. Lakini pia tuna run joint account. Lugha ya hii ni pesa yangu hii ya kwako tuliisha isahau kabisa.

Tiba
 
Ha ha haaaa wengine tukikasirika tunahamia hoteli kabisa! !!!

Mbona siyo tatizo? Si zikiisha unarudi? Napenda mwanaume kiongozi meaning anajua yeye ni kiongozi na my hero!
Kwanza kabla hujaenda hotel mi faster nshaomba sorry ya vitendo!.... Huendi ng'ooo au twaenda wote!
 
habari wa JF.
miezi sita iliyopita nilibahatika kuoa mwanamke mmoja wa kiislam ambapo tulifunga ndoa ya kiislam.
katika mahusiano ya uchumba nilimuona ni muwazi na anaakili za kimaendeleo ndipo nikatangaza ndoa.
lakini tangu nifunge naye ndoa sijawahi kuona hata shilingi tano yake.pia hajawahi kutoa katika benki hata shilingi yeye ana deposit tu.nikijaribu kumuuliza yeye atatumia fedha zake kwa matumizi gani?anasema jukumu la kumlisha ni langu.sawa sikatai je fedha yeye ataweka wapi ?au atajenga lotion bila mimi kujua!!! naombeni mchango wenu.nini nifanye?au nimuache?

Anayefurahia ndoa siku zote ni mwanamke, furaha ya mwanamme timamu hukoma pindi anapofunga pingu za maisha yaani ndoa na furaha ya mwanamke huanza pindi anapoolewa. Ndio maana wanaume wengi wanaogopa ndoa wakati kwa wanawake wanapenda ndoa.
Siku zote amini usiamini kipato cha mwanamke ni chake ila chako ni cha wote, hata mwanamke akikuzidi mshahara lakini bado atakuomba hadi hela ya kiberiti.
 
Anayefurahia ndoa siku zote ni mwanamke, furaha ya mwanamme timamu hukoma pindi anafunga pingu za maisha yaani ndoa na furaha ya mwanamke huanza pindi anapoolewa. Ndio maana wanaume wengi wanaogopa ndoa wakati kwa wanawake wanapenda ndoa.
Siku zote amini usiamini kipato cha mwanamke ni chake ila chako ni cha wote, hata mwanamke akikuzidi mshahara lakini bado atakuomba hadi hela ya kiberiti.

Ndo hivyo boss kwani usipompa atapewa na wengine!
 
Mbona siyo tatizo? Si zikiisha unarudi? Napenda mwanaume kiongozi meaning anajua yeye ni kiongozi na my hero!
Kwanza kabla hujaenda hotel mi faster nshaomba sorry ya vitendo!.... Huendi ng'ooo au twaenda wote!


Matured you!!!???
 
ni wewe mwenyewe hukutaka kujipanga kabla ya kuoana.mlitakiwa mjadiliane malengo yenu ya kimaisha yatakuwaje.kama ulimwonyesha kwamba unayaweza yote wewe mwenyewe,basi mkeo akaona haina haja ya mchango wake sasa kaa nae kwq upole elimishaneni kwa utaratibu na sio amri au kususiana.kila mtu achangie wazo la namna ya kuboresha maisha yenu kama familia.la sivy
o huyo yuko mguu mmoja ndani na mwingine nje
 
Back
Top Bottom