Wanawake wafanyakazi ndivyo walivyo katika ndoa?

Wanawake wafanyakazi ndivyo walivyo katika ndoa?

msapwata

Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
57
Reaction score
12
Habari wa JF,

Miezi sita iliyopita nilibahatika kuoa mwanamke mmoja wa kiislam ambapo tulifunga ndoa ya kiislam.

Katika mahusiano ya uchumba nilimuona ni muwazi na ana akili za kimaendeleo ndipo nikatangaza ndoa.

Lakini tangu nifunge naye ndoa sijawahi kuona hata shilingi tano yake.Pia hajawahi kutoa katika benki hata shilingi yeye ana deposit tu.

Nikijaribu kumuuliza yeye atatumia fedha zake kwa matumizi gani?Anasema jukumu la kumlisha ni langu.Sawa sikatai je fedha yeye ataweka wapi ?au atajenga lotion bila mimi kujua!!!

Naombeni mchango wenu,nini nifanye au nimuache?
 
Ndoa ina stages pia kama vitu vingine hapo sasa unaelekea kukomaa na ndoa yako!!!

Kama pesa yako inaonekana inaenda wapi hakika mkeo wa ndoa mliooana kwa mapenzi bila shuruti hawezi kushindwa kukusaidia!!!!

Ila kama yako unabana na yake hata harufu hutosikia, by the way majukumu yako ni pamoja na kumtunza we senti zake unataka za nini????!!!

Nunua kiwanja au fungua biashara mkubaliane we unakomaa na projects ye akusaidie mambo ya hapo ndani na aone hela yako inafanya kazi kweli lakini sio ujanja ujanja @work.

Akizingua na hapo usiitishe hata kikao we timua tu na hutojuta
 
mke ni mali yako.Hata alivyonavyo ni mali yako.Cha msingi matumizi yawe yenye manufaa kwa familia nje ya hapo uliyenaye alipaswa aoelewe na mtu mwingine.
 
habari wa JF.
miezi sita iliyopita nilibahatika kuoa mwanamke mmoja wa kiislam ambapo tulifunga ndoa ya kiislam.
katika mahusiano ya uchumba nilimuona ni muwazi na anaakili za kimaendeleo ndipo nikatangaza ndoa.
lakini tangu nifunge naye ndoa sijawahi kuona hata shilingi tano yake.pia hajawahi kutoa katika benki hata shilingi yeye ana deposit tu.nikijaribu kumuuliza yeye atatumia fedha zake kwa matumizi gani?anasema jukumu la kumlisha ni langu.sawa sikatai je fedha yeye ataweka wapi ?au atajenga lotion bila mimi kujua!!! naombeni mchango wenu.nini nifanye?au nimuache?
Ukitaka rose/waridi vumilia miiba.
kazi njema
 
Ila lakini kiuhalisia na utamaduni wetu nani anahudumia familia,.
Halafu hapo chini umesema anataka atengeneze lotion yake?
 
Kaa chini umchunguze vizuri wengi wanawake dizaini hii ni wale ambao walishawahi kumpenda mwanaume mpaka ikafikia kumuamini kwenye mambo ya fedha kama vile kumnunulia nguo na hata kumkabidhi ATM lakini mwishowe akaishia kusalitiwa.wanawake wa aina hii huwa wagumu sana kumwamini mwanaume kwenye maswala ya pesa
 
habari wa JF.
miezi sita iliyopita nilibahatika kuoa mwanamke mmoja wa kiislam ambapo
tulifunga ndoa ya kiislam.
katika mahusiano ya uchumba nilimuona ni muwazi na anaakili za
kimaendeleo ndipo nikatangaza ndoa.
lakini tangu nifunge naye ndoa sijawahi kuona hata shilingi tano
yake.pia hajawahi kutoa katika benki hata shilingi yeye ana deposit
tu.nikijaribu kumuuliza yeye atatumia fedha zake kwa matumizi
gani?anasema jukumu la kumlisha ni langu.sawa sikatai je fedha yeye
ataweka wapi ?au atajenga lotion bila mimi kujua!!! naombeni mchango
wenu.nini nifanye?au nimuache?
kwani dini inasemaje kuhusu hili?
 
Kaa chini umchunguze vizuri wengi wanawake dizaini hii ni wale ambao walishawahi kumpenda mwanaume mpaka ikafikia kumuamini kwenye mambo ya fedha kama vile kumnunulia nguo na hata kumkabidhi ATM lakini mwishowe akaishia kusalitiwa.wanawake wa aina hii huwa wagumu sana kumwamini mwanaume kwenye maswala ya pesa

Aaaanh kaumizwa huko alete hayo mpaka kwenye ndoa????!!!!!
Mbona kigozi kachania mbali ndoa kaipata huku, historia sio zote zinakumbatiwa!!!!

Tutashindwana kama kila mtu akikumbatia historia yake!!!
 
Ni kweli jukumu la kulisha mke ni lako tatizo we ulimuoa kwa kuangalia kazi na mshahara wake.
Anavyofanya ni sawa wanaume mna matatizo ,wanawake wengi wamefanya maendeleo na wanaume wameishiwa kuumizwa ndio maana wanawake wamekuwa makini siku hizi.
Halafu wanaume sikuhizi nani kawaloga mtu anaoa kazi ya mwanamke na mwanamke mwenyewe.
Aendelee hivyo hivyo ningekuwa namfahamu ningemshauri kama akitoa atoe hela yake kama akitaka kununua nyama,sahani au nguo bali cement/mabati no kama huwezi shauri yako.
 
Wengi wanahitaji heshima tu ya kuwa wameolewa lakini Mara nyingi hawapo pamoja na wauume zao .
 
Mimi utakaa nyumbani niwe nakupa vihela utavyokuwa unavipata huko
 
Back
Top Bottom