Wanawake wafanyakazi ndivyo walivyo katika ndoa?

Wanawake wafanyakazi ndivyo walivyo katika ndoa?

Jiangalie na wewe upo wazi kwake?unamweleza mambo yako yote?mnake nyie nao ndo huwa number1 wakuficha mambo yenu ikiwa hivo hata mie wangu utakua nausikia tuuuuuuu
 
Kwani umemuoa kwasababu atkupe hela zake au ujue pesa zake anafanyia nini? sijui kwa mtazamo wako lakin mimi nimeolewa nafanya kazi lakini kununua kitu nyumbani au chochote ni hiyari yangu sio lazima na wala mume wangu hajawahi kuniuliza napokea kiasi gani wala pesa nimefanyia nini,isipokua ikifika mwisho wa mwezi yeye ndio ananipa pesa za matumizi kama kawaida ya nyumbani na watoto,sasa ni mimi uungwana wangu kusema mume wangu wacha nikusaidie kulipa umeme bills za simu au chochote nnacho jisikia,lakini wewe unalalamika hakwambi,kwanini ulipo muoa hukumwambia nakuao lakini sheria yangu ni 1,2,3 ili ajue kama ataweza sawa hawezi awache... usisahau anafamilia yake vile vile...
kama umeoa basi angalia majukumu yako kama mume ukishindwa kaa na mwenzio chini mueleza mke wangu mwezi huu mamabo sio mazuri tusaidiane ....sio lazima kukusaidia..............
 
Hayo yanaonekana na huhitaji kuambiwa usaidie.
Tatizo ni pale mtu anatoka daily anaenda job ila kila siku analia lia tu kuwa hana pesa kuanzia Jan 1 mpaka Dec 30 na anachofanya cha maana hakuna,Wallah huyu simsaidii labda akae tu nyumbani nijue hajiwezi katika kutafuta anisaidie kupunguza budget ya mshahara wa msichana mie nisimamie show yote yeye akuze kitambi tu!

Nilimuuliza nadhani ....yeye yuko wazi kiasi gani!!!?????
Je mkewe anajua na kuona hela ya mumewe ikifanya kazi!!?????

Ha ha haaaaa we danganya wenzio huku mi unanipaga!!!!!
 
Habari wa JF,

Miezi sita iliyopita nilibahatika kuoa mwanamke mmoja wa kiislam ambapo tulifunga ndoa ya kiislam.

Katika mahusiano ya uchumba nilimuona ni muwazi na ana akili za kimaendeleo ndipo nikatangaza ndoa.

Lakini tangu nifunge naye ndoa sijawahi kuona hata shilingi tano yake.Pia hajawahi kutoa katika benki hata shilingi yeye ana deposit tu.

Nikijaribu kumuuliza yeye atatumia fedha zake kwa matumizi gani?Anasema jukumu la kumlisha ni langu.Sawa sikatai je fedha yeye ataweka wapi ?au atajenga lotion bila mimi kujua!!!

Naombeni mchango wenu,nini nifanye au nimuache?

Mawazo ya wanawake wengi wa kibongo ni tofauti na wale wa nje. Mwanamke wa kibongo ni kumlalia mumewe kwa kila kitu na hela zake yeye anasaidia kwao. ni kweli km ulivosema ni jukumu lako kumtunza, lakini kama hafanyi kazi, ila kama anafanya kazi maisha ya sasa ni kutunzana. Angalia mahusiano ya wanandoa wa nchi za nje, baba na mama lao ni moja, wanatafuta pesa kwa ajili yao na watoto wao, mwanamke ana huruma na mumewe, anaomba kulipa bili za maji na umeme na hata chakula, anamwachia mumewe kodi ya nyumba na ada za watoto na mambo mengine, hata mwanaume una farijika. Mwanamke wa kibongo, mwanaume kwake ni asset, wala usimfikirie vibaya ndo fikra wanazokua nazo tokea wadogo. cha msingi ni kutumia busara tu, hua hawana mapenzi ya dhati, mapenzi yao ya dhati ni kwa wazazi wake, ww kwake ni kama gurudumu la kusukumia maisha, asilimia kubwa ndo hua ni hivo japo wachache sn sn wapo tofauti.
 
Naunga mkono hoja yako, unachokisema ninakishuhudia kila uchao.
 
Mwanamke wa wakati wa uchumba ni tofauti kabisa na akisha ingia ndani ya ndoa sijui wana nini hawa!
 
Mimi nawafahamu wanawake kibao wamenunua viwanja na wanajenga kimya kimya bila waume zao kujua.ukiwauliza wanakwambia sio lazima kila unachokifanya mumeo ajue.wakati mwingine unawaza bora uzalishe tu mwanamke then uchukue mwanao yeye akajijue mbele huko.
 
Naunga mkono hoja yako, unachokisema ninakishuhudia kila uchao.

Hawa hua hawajua kama ni tulizo la wanaume, mwanaume hata awe na hasira vipi lakini kama mkewe anataka kumtuliza anamtuliza, mwanamke ni tulizo la mwanaume, yaan mwanaume una stress zako yeye ndo wa kukufariji, lakini wanawake wa siku hizi wao ndo wanakuongezea stress, ukisema usioe bac hautaoa milele wote ndo wapo hivo hivo, cha msingi ni kuonesha uanaume wa kuvumilia tu, ukiona stress zimekua nyingi unamwacha tu mbona wapo wengi sana, unamchukua mwengine ambae ana uafadhali kidogo. Ndoa ambazo zina mafanikio basi ujue mke ni kichwa yaan ana akili sn anamtuliza mumewe kimawazo, mafanikio yanaonekana na hata Mungu anabariki ndoa. lakini wengi hua anachanga hela zake, na zako anabeba anajenga nyumba anaiita yake, ila yako ni ya wote, nyumba kutwa imejaa ndugu zake, ukileta wako kasheshe, ukimtumia mamaako hela ananuna, ila mamaake anataka umtumie kila siku, hawa ni watu waajabu sn, unatakiwa kua mjanja sn na akili kubwa kuishi nao hawa ni majanga.
 
Habari wa JF,

Miezi sita iliyopita nilibahatika kuoa mwanamke mmoja wa kiislam ambapo tulifunga ndoa ya kiislam.

Katika mahusiano ya uchumba nilimuona ni muwazi na ana akili za kimaendeleo ndipo nikatangaza ndoa.

Lakini tangu nifunge naye ndoa sijawahi kuona hata shilingi tano yake.Pia hajawahi kutoa katika benki hata shilingi yeye ana deposit tu.

Nikijaribu kumuuliza yeye atatumia fedha zake kwa matumizi gani?Anasema jukumu la kumlisha ni langu.Sawa sikatai je fedha yeye ataweka wapi ?au atajenga lotion bila mimi kujua!!!

Naombeni mchango wenu,nini nifanye au nimuache?

Oa kipa. Kila kitu anangoja kudaka tu. Hivi hii world cup inaendelea bado hujaona kipa wa kuoa? Una matatizo wewe.
 
mi bado sijaoa

mimi sio wa dini hiyo hivyo sheria na maudhui ya ndoa za kiislam siyajui, lakini kwa wakristo ndoa inawaunganisha wawili kuwa mmoja ,hivyo ni kosa/ dhambi mwanamke kufanya hivyo.
 
Mie kuna mtu kama ningeolewa naye asingeona hata mia yangu. Lakini kwa sasa salary slip mezani, account balance mezani.

Kama hakuna connection ya mahusiano, huwezi mwamini mtu. Au ukimweka mwenza wako kundi la mchunaji, lazima ufiche hela zako.

Na ndoa za siku hizi tunabebana tu.kutoa mikosi, hata kama ushamweka kundi la mchunaji.
 
Hapa ndipo tulipofika kama jamii wanandoa kutafuta suluhu ya ndoa zao toka ktk mitandoa ambayo wengi wa watoaji ushauri ni wanafunzi under 20yrs,wasioa/kuolewa ambao wengi wao hawajui misingi ya ndoa.

hahahaaa uwii umenena
 
Back
Top Bottom