Ngoja nichore picha kubwa leo kuhusu ndoa, ni wapi tunakosea mpaka kila siku tunapata kusikia au kuona haya matatizo kila siku kwenye ndoa.
Walio wengi wetu tunasahau ile siku ya kwanza kabisa unaangukia kumpenda msichana kabla ya kuanza uhusiano naye na mwishowe mnakuwa mke na mume. Tulio wengi kikubwa tunaanzaga kuvutiwa ni muonekano wa nje wa mwanamke au mwanamme ndiyo inakuwa chanzo cha kuangukiana kimapenzi. Pale pale anaanza kufikiria watoto wake watazaliwa na muonekano upi?, ukitoka naye kwenye kadamnasi watu watamchukuliaje?, vipimo vya elimu zenu na vitu vingine vingi kama hivyo.
Lakini tukisha gubikwa na yale mapenzi ya maono ya nje huwa tunajikana nafsi zetu na kusahau- kutambua kuwa sisi binafsi tuna ndoto zetu,- nafasi zetu za uwepo wetu hapa duniani, ushawishi wa vitu fulani, uwezo wetu wa kujituma na kikubwa tabia pia. Sasa mkishafunga pingu za maisha kila mtu nafsi yake inarudi kwenye uhalisia na ndipo tunapoanza kutambua kwa mshangao, Amah! Kumbe ndoto zetu tofauti, huyu mwenzangu mvivu na tegemezi sana huyu, sijui tabia yake mbaya sana huyu na mambo mengiii sababu kwenye uchumba mlijikana nafsi zenu wenyewe na kushindwa kulinganisha ndoto zenu, maono yenu, tabia zenu (hususani kwa wanawake wanaficha sana) kama zinashabihiana.
Ndoa ni maisha na kama ukishindwa kupata mpenzi mnayeshabihiana kitabia, misukumo ya kujishughulisha, maono, ndoto, ushawishi na ukampenda tu sababu anamuonekano bomba (hata awe mzuri kama malaika) mpasuko ndani ya ndoa hauepukiki. Mkishatulia tu mkianza kuendeleza maisha yenu misuguano inaanza ndani ya ndoa.
Cha mwisho usitake kuoa tu sababu mke au mume akuletee ukamilifu kwenye maisha yako utaangukia puwa. Pia kama binafsi hauko mkamilifu mpasuko ndani ya ndoa hauepukiki. Hivyo msifate sura na muonekano pekee kama unataka kuishi maisha ya furaha kwenye ndoa nasisitiza lazima tabia, ndoto, maono, na ushawishi vishabihiane- si na kufanana kabisa kila kitu.