Wanawake punguzeni makasiriko. Mjitathimini kama nyie hamna kasoro

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
1,177
2,281
Leo nataka kuongea na wanawake wote popote mlipo. Kwa nini siku zote ktk mahusiano au ndoa lawama ni kwa wanaume tu?

Wanawake wote wanaolalamika juu ya wanaume eti ni mbwa, hawaridhiki hata uwafanyie kitu gani bado atakusaliti. Niwaambie tu kuwa siyo kweli nyie mnaolalamika ni kuwa too much selective. Mnataka wanaume wenye sifa nyingi utadhani ni bidhaa. Lakini km unamuomba Mungu akupe tu mume mwema (tabia njema) kamwe huwezi kujutia maishani mwako. Lakini ukiwa mtu wa kwenda kuoga na kujipapasa papasa mwili na kujiona mrembo na una umbo zuri na kuona huwezi kuolewa na mtu wa chini au asiye na sifa unazohitaji lazima ulie na kujuta maisha yako yote.

Siyo wanaume wote ni Malaya au hawaridhiki, tatizo una kutana na wanaume ambao wana sifa unazotaka wewe na wao wanakutana na wewe usiye na sifa wanazotaka wao. Hapo sasa inakuwa kuwindana ili mmoja akosee kidogo tu songombingo lianze.

Niwaambie tu kuwa mwanaume wa kweli wa moyo wako kamwe hataangalia sura wala shepu au miguu au midomo, ataangalia upendo wa dhati na akili yako njema km ulivyolelewa na wazazi. Wanawake niwaibie tu siri kuwa huwa mnapoteza muda mwingi bure kujipodoa, kujichubua, kujitengeneza shepu, na kuvaa mawigi kwani hivyo vyote huwa siyo vipaumbele vya mwanaume wa kweli muoaji.

Achaneni na vigezo viiiingi utadhani maonbi ya kazi, just be simple na ujikubali wanaume wa kweli (siyo mabishoo) watakuja na mtaishi kwa amani. Hayo yote mnayofanya kwa sasa ni mbwembwe tu na sku hizi mmeweka kigezo Cha "God fearing" ha ha ha ha nyie mtafika mbinguni mmechoka sn. Ndoa siyo maigizo wala fasheni.
 
Kwa matusi tunayoona humu kwenye huu Uzi ndiyo aina ya wanawake wanaolia Kila siku eti wanaume wote ni mbwa hawaridhiki na blaaa blaaa kibao. Yani wewe mwenyewe mdomo hauna break wala uvumilivu alafu utegemee mwanaume bora. Never.
 
Kuna Kauli Yao wanawake huwa sielewi kabisa mkuu waulize Kisha unipe jibu.Wanaposema nimempa Kila kitu lakini amenisaliti au hata umpe Nini haridhiki Huwa wanaanidha kitu Gani wanetoa?
 
Labda atokee mwanaume wa android mwenye kichwa ndani Kuna snapdragon 8 gen 2 mwenye sifa ya;

kufanya yote anayotaka mwanamke.

Lakini na kuhakikishia hata akitokea mwanaume anayemtimizia mwanamke yote anayotaka Bado atamchoka maana ataona anaishi na zumbukuku.

Kiufupi Fanya unayoweza kama mwanaume usiyoyaweza achana nayo usije ukapata matatizo ya kiafya.
 
Back
Top Bottom