Nasema nanyi wanaume wenzangu

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,799
3,816
Wakuu habari za uzima?

Leo nataka niongee na baadhi ya wanaume wenzangu wanaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwao kana kwamba sisi wanaume hatukosei kwenye jamii wakati maovu yote yanayofanywa na wanawake ni sawa tu na maovu yote yanayofanywa na wanaume.

  • Wanawake wanaochepuka wanaenda sambamba na wanaume wanaochepuka.
  • Wanawake wanaozalishwa bila ndoa/nje ya ndoa wanaenda sambamba na wanaume wanaozalisha bila/nje ya ndoa.
  • Wanawake wasagaji wanaendana na wanaume wasagaji
  • Wanawake wanaopenda kutembea na waume za watu wanaendana na wanaume wanaopenda tembea na wake za watu.
  • Wanawake wanopenda kutembea na mijibaba wanaendana na wanaume wanaopenda kutembea na mijimama.
  • Wanawake waliopo kwenye mahusiano sababu ya pesa wanaendana na wanaume waliopo kwenye mahusiano sababu ya ya mbunye.
  • Wanawake wanaopenda kuhudumiwa kwenye mahusiano wanaendana na wanaume vinga’sti wanaopenda kulelewa.
  • Wanawake wanaowaacha wanaume waliowasomesha wanaendana na wanaume wanaowaaacha wanawake walioanza nao kwenye umaskini.
  • Wanawake wasio watu kwa waume zao wanaendana na wanaume wasio na upendo kwa wake zao.
Tofauti zote hizo siyo sababu ya wanaume kufanya maovu vile wanavyojisikia at kwa sababu tu wao wako juu ya wanawake.

Wapo wengine watasema ati wanaongelea maovu ya wanawake kwa sababu wanawake ndiyo wanapata madhara zaidi kuliko wanaume, wao linapokuja suala la mahusiano hawana cha kupoteza kabisa ila niwaambie tu kuwa hiyo siyo sababu ya wanaume kufanya maovu wanavyojisikia ati ili kuwakomoa wanawake. sasa mbona magonjwa ya zinaa hayaangalii jinsia na yanaua kwa mtindo ule ule?.

Kama hatuna cha kupoteza kwenye mapenzi Kwanini sisi ndio tunaongoza kushinda kwenye mitandao kulalamika kuwaongelea wanawake? Ati tunafanya kwa lengo la kuwasaidia hao wanawake wenye hayo maovu, Kwanini muishie kuongea kwa mdomo si kufanya vitendo?

Unakuta mwanaume anasema “kuna demu nimemtongoza Jana akakubali, muda ule ule na mzigo akanipa siku ile ile” Halafu anamalizia kwa kusema “daah wanawake wa siku hizi wanajirahisisha sana acheni umalaya la sivyo wanawume tutaendelea kuchapa na kusepa”sasa mwanaume kama huyu ni mnafki yaani anajifanya kusikitishwa na wimbi la la wadada kujirahisisha wakati huo huo yeye ndio kinara wa kutongoza kama kweli ana nia na hapendi wanawake kujirahisisha Kwanini asiache kutongoza na kuwaomba mzigo?

Kama baadhi ya wanaume wana nia ya kuwasaidia wanawake na mmeona maneno hayasaidii Kwanini msifanye vitendo kwa kuacha kuyafanya mambo yanayowafanya wanawake wajirahisishe??

Halafu wanaume wengi utasikia “Kwanini mwanamke ukitongozwa ukubali” badala ya kuuliza “ Kwanini mwanaume anatongoza pasipo kuwa na nia ya dhati?

Yaani tunalazimisha ionekane kama mwanaume kutongoza si kosa ila mwanamke kukubali ni kosa. Wakati kinachoanza ni kutongoza Halafu kinafata kukubali au kukataa,
Mwanaume anayetongoza na mwanamke anayekubali wote wana makosa.

Kama kila jinsia imeshindwa kubadilika kwa nafasi yake na kusubiria Ati jinsia nyingine ianze kubadilika hapo tutakuwa tunasubiri meli kwenye uwanja wa ndege

Ninyi endeleeni kupiga na kusepa tuone mwisho wake, kama sio kuongeza vibarua viwandani, magenge ya uhalifu, na mambo ambayo kwa kizazi kwa taifa lijalo hayana ustawi .

FROM: instagram.
 
Wakuu habari za uzima?

Leo nataka niongee na baadhi ya wanaume wenzangu wanaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwao kana kwamba sisi wanaume hatukosei kwenye jamii wakati maovu yote yanayofanywa na wanawake ni sawa tu na maovu yote yanayofanywa na wanaume...
Kwanza mleta uzi wewe sio me ni ke kwasababu lafudhi ya maneno yako ya kike! Laaasivyo we ni shoga. Hivyo huu uzi hauna mashiko
 
Who cares about perfection?

Even the moon is not perfect, it is full of craters, the sea is incredibly beautiful but salty and dark in the depth.

The sky is always infinite, but often cloudy so everything that is beautiful isn't perfect. It is special

Therefore, every woman can be special to someone. Stop being perfect but try to be free and live, doing what you love not wanting to impress others.
 
Wanaume wasio mashoga wanaongelea sana makosa ya wanawake kwasababu wao huingia kwenye mahusiano na wanawake

Hivyo hivyo wanawake wasio wasagaji wanaongelea sana makosa ya wanaume kwa mantiki hiyohiyo

Iko hivyo
 
maovu ni vitendo vilivyokinyume na matarajio ya jamii.

Kitendo kinaweza kikawa kiovu kwa mwanamke ila kisiwe kiovu kwa mwanaume.

Kwa hiyo jamii ina standard zake kwamba mwanamke anapaswa kufanya nini, na mwanaume anapaswa kufanya namna gani.

Kwa hiyo malalamiko ya wanaume kwa wanawake huwezi kuyapuuza kirahisi kwa kuwa eti na wanawake nao wana maovu yao, hali kadhalika malalamiko ya wanawake kwa wanaume huwezi kuyapuuza kwa kigezo kwamba na upande wa pili nao wana yao.

Mfano, jamii inafahamu kwamba ni wajibu wa mwanaume kumuhudumia mkewe na familia.

Sasa huwezi ukapingana na malalamiko kwamba kuna wanaume hawawajibiki kwa kuwa eti pia kuna wanawake hawawaheshimu waume zao.
 
maovu ni vitendo vilivyokinyume na matarajio ya jamii.

Kitendo kinaweza kikawa kiovu kwa mwanamke ila kisiwe kiovu kwa mwanaume.

Kwa hiyo jamii ina standard zake kwamba mwanamke anapaswa kufanya nini, na mwanaume anapaswa kufanya namna gani.

Kwa hiyo malalamiko ya wanaume kwa wanawake huwezi kuyapuuza kirahisi kwa kuwa eti na wanawake nao wana maovu yao, hali kadhalika malalamiko ya wanawake kwa wanaume huwezi kuyapuuza kwa kigezo kwamba na upande wa pili nao wana yao.

Mfano, jamii inafahamu kwamba ni wajibu wa mwanaume kumuhudumia mkewe na familia.

Sasa huwezi ukapingana na malalamiko kwamba kuna wanaume hawawajibiki kwa kuwa eti pia kuna wanawake hawawaheshimu waume zao.
Nafikiri hata hujaelewa alichoandika Embu msome tena
 
Eleza ulichokielewa.

Point ya msingi ametoa ulinganisho wa malalamiko baina ya wanaume na wananawake.

Wewe umeelewa nini?
Usichoelewa ni kwamba neno uovu ulilosema wewe bado liliwekwa kwa mfuno dume.
Unaelewa nini maana ya tafsiri neno uovu?

Mbona kaeleza vitu simpo😂😂
 
Back
Top Bottom