Wanawake na maradhi ya urembo inasikitisha sana

Hata mimi nimekuwa naaminishwa kuwa waafrika pekee ndio wanapenda vitu artificial...kuna siku nimeenda kwenye duka moja popular kununua wigi nikashangaa mama wa kizungu yuko busy kuchagua; wazungu wengi wana nywele mbaya, wengine ni za kuhesabu ...wenye nywele nzuri ni Latin Americans.
 
Tatizo la Tz bado hatujawa na professionals wa urembo. Unakuta salon nzuri huduma zero; mengine ni kujifanyia mwenyewe; unaingia you tube unajifunza.

Ahsante! Umeongea kitu cha muhimu sana...thatz why hata mimi nawasisitiza dada zangu wa MMU au mtu yeyote yule anaependa mambo ya urembo kuwa aendapo kufata huduma yoyote salon ajitahidi awe mtu wa kuhoji kabla hajafanyiwa huduma...uwapo salon usiruhusu mwili wako uwe wa majaribio kama vile wewe ni mdoli.

Pia katika huduma za salon hakuna kitengo ambacho mastaff wake wanatakiwa kuwa very serious kama kitengo cha beauty clinic. Kitengo hichi ndiyo kinabeba huduma za Kope,Detoxification,face facial,waxing nk.
 
Mbona mi siwekagi hayo ma kope na nywele zangu kama Amber Rose lakin mupenz kazimika kaoza kwa vitu natural,bado kina Sepetu,,uwoya
 
Wanaukumbi.

Ama kweli hujafa hujaumbika, mrembo Khadija Omar, mkazi wa Kigogo, Dar amepata pigo kufuatia kupofuka macho alipokuwa akiwekwa nyusi bandia katika saluni moja iliyopo maeneo hayo,


Tukio hilo lilitokea Novemba 14, 2013 na kuvuta hisia za watu wengi waliosikia na kushuhudia mkasa huo.
Akizungumza na paparazi juzi huku akimwaga machozi, Khadija alisema siku ya tukio saa 11 jioni alikwenda kwenye saluni hiyo iliyopo jirani na anapoishi kwa lengo la kubadili mwonekano wake wa macho kama akina dada wengine wanavyofanya.

“Mara tu baada ya kunibandika kope nilianza kuona giza, nikawaeleza akina dada waliniweka lakini wakanipuuza na kuniambia mimi ni mwoga.
“Muda mfupi mbele hali yangu ikawa mbaya zaidi, ikabidi wazibandue kope lakini juhudi zao ziligonga mwamba kwa sababu walitumia gundi kali, ikabidi nirudi nyumbani,”alisema Khadija.
Akaongeza: “Nikiwa njiani macho yaliniuma sana na kuzidi kupoteza uwezo wake wa kuona, ghafla nikaanguka chini. Akatokea msamaria mwema na kunipeleka nyumbani,” aliongeza.
Khadija Omar, mkazi wa Kigogo.
Khadija alisema kesho yake alikimbizwa Hospitali ya Amana, Dar ambako alipatiwa dawa bila ya kutolewa kope hizo na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
“Nilipofika nyumbani hali ilizidi kuwa mbaya nikalazimika kupelekwa Hospitali ya Macho ya CCBRT (Msasani, Dar) ili kupatiwa ufumbuzi wa tatizo hilo,” aliongeza Khadija kwa majonzi.
Alisema kule CCBRT alijikuta akiangua kilio baada ya madaktari kumwambia kope hizo haziwezi kutolewa mpaka zikatwe na mkasi.

Baada ya zoezi hilo kufanyika, Jumapili iliyopita Khadija aliweza kufungua macho kwa mara ya kwanza tangu alipotokewa na hali hiyo lakini bila kuona sawasawa.
Jumatatu iliyopita Khadija aliruhusiwa kurudi kwake lakini akiwa hana uwezo wa kuona na kutakiwa kurejea tena hospitalini hapo baada ya wiki tatu kwa uchunguzi zaidi.
Daktari mmoja wa CCBRT ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake gazetini alisema: “Khadija anaweza kuona kama zamani lakini itamchukua muda mrefu kutokana na madhara ya gundi ya ‘supa glu’ iliyotumika.
Taarifa zaidi zinasema, Jane na Koku wafanyakazi wa saluni waliomuweka kope hizo Khadija walikamatwa na Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar na kufunguliwa jalada la uchunguzi namba MGN/RB/13021/2013.

Hii inaweza kuwa fundisho kwa kinadada wengi wa mjini wakiwemo mastaa wa filamu, muziki na mitindo ambao ni watumiaji wakubwa wa urembo huo unaodaiwa kuwa na madhara makubwa kwa mtumiaji yakiwemo hayo ya kuwa kipofu.




Vipi Umekuja kupunguza stress huku maana kule watu wana hasiraa utafikir wameibiwa wake zao lol
 
Nampa pole sana huyo dada. Lakini pia akina pia liwe fundisho kwa wengine. Ni kweli kwa akina dada wengi urembo sasa ni maradhi.
 
Mambo mengine ni kujitakia kwani ni lazima kubandika hayo makolokocho? Pole yake lakini.......hujafa hujaumbika natumaini itakuwa ni fundisho kwa wengine (UZURI NI JINSI ULIVYO VIPODOZI MBWEMBWE TU)
 
Inasikitisha sana. Hizi fani watu huzisomea, wengine wanafikiri ni mchezo mchezo tu.
 
Kwanza unajua maana ya BL? ni vigumu sana kwangu kuielezea hapa. Ila kama kuna mwana MMU yoyote anaeijua basi kwaniaba yangu ningependa akuelezee what is BL waxing.

Bikini Line Waxing........mbona kitu cha kawaida sana......
 
Back
Top Bottom